Ipo haja ya chadema kuwa na mfumo wa kisasa wa kiintelijensia wa kulinda makamanda wake

Samwemgomba

Member
Mar 25, 2019
35
15
Waungwana niwasalimu kwa jina la muumba wa mbingu na ardhi "amani ya bwana iwe nanyi wote" nimekuwa msomaji wa tu mambo mengi sana humu JF kwa zaidi ya miaka 10 sasa ila Leo nimeona niseme kitu. Kwanza kabisa nasikitishwa Sana na hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini kwetu kwa takribani miaka minne sasa tang kuingia serikali hii ya awamu ya 5. Maisha ya wanasiasa wa Upinzani, wakosoaji wa serikali, wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu pamoja na watu wenye mawazo mbadala yamekuwa shakani Sana!

Hii sio Tanzania tuliokuwa tukiiota! Kimsingi serikali zote duniani zinavyo vitengo maalumu via kuua na kuwapoteza wakosoaji wao wakuu hata hapa Tanzania haya mambo sio mageni, ila yamekithiri sana kwa kipindi hichi. Bado nakumbuka Sana jinsi alivyopotea Ben Saa nane kijana ambae kwa mtazamo wangu alikuwa very smart kichwani, Tukio la Tundu lisu la kujaribu kutoa uhai wake ilikuwa tukio baya Sana analofanyiwa one of the most lawyer mwenye ubongo mzuri kabisa kwa Taifa letu kwa miaka ya karibuni.

Mifano ni mingi ukiachana na tukio la kutekwa na kuteswa kwa akina Yerico, Mdude, kifo cha Alphonce Mawazo na utitili wa vijana wengine na wanaharakati wenye mawazo mbadala. Muathilika Mkubwa wa matokeo haya ya sasa ya utekeji, uuwaji na unnyanyasaji unaofanywa na watu waliopachikwa jina la "WATU WASIOJULIKANA" ni pigo kubwa kwa familia za wahanga ila ni PIGO kubwa zaidi kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kwa kuwa kinaondokewa na vijana wao ambao kwa mtazamo wangu ni very intelligence with bright mind ambao wamgekuja kuwa viongozi wazuri wa chama, jamii na Taifa kwa ujumla.

Iko haja sasa kwa CHADEMA kuwa na mkakati maalumu wa kuwalinda makamanda wao dhidi ya vitendo hivi kwan vikaachwa viendelee sio tu vitawapotezea vijana wao na watu muhimu bali vitawaogopesha vijana wngine smart kuwaunga mkono kwa Kubota yanayowakuta wakina "MDUDE".

Ikiwezekana muombe hata msaada kwa mataifa yaliondelea kiteknlojia jinsi ya kuwalinda all targeted people within your party ili siku yakitokea matukio ya kutekana kipumbavu kama walivyofanya kwa MDUDE muweze kubaini haraka na kuwaweka wazi hao WASIOJULIKANA kwa lengo la kutoa funzo kwa TAWALA DHALIMU.
 
Back
Top Bottom