Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 18,591
- 20,892
Wakuu asalama alykum......Nadhani ipo haja kwa sasa bunge letu tukufu kuangalia ni jinsi gani litaweza kuondoa baadhi ya vifungu ndani ya katiba vinavyoruhusu watu kufanya shughuli za kisiasa kila wakati ili kuongeza utendaji kazi wa watanzania badala ya shughuli za kisiasa kufanyika kila wakati na kila pahala,Naomba katiba ieleze wazi wazi shughuli za kisiasa zitakuwa zikifanywa mwaka mmoja kabla ya chaguzi au miezi kumi na miwili kabla ya uchaguzi husika, Na hili livibane vyama vyote no matter kuna ccm au chama gani chochote na kama kutakuwepo na shughuli za ufunguzi wa matawi au vikao vidogo basi vikao hivyo visizidishe zaidi ya watu 15 huku wakiomba vibali katika mamlaka pendekezwa.