Ipo haja ya bunge letu lijalo kutupia macho kipengele ndani ya katiba kinachoruhusu mikutano ya vyama kufanyika hovyo hovyo.

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
13,292
2,000
Wakuu asalama alykum......Nadhani ipo haja kwa sasa bunge letu tukufu kuangalia ni jinsi gani litaweza kuondoa baadhi ya vifungu ndani ya katiba vinavyoruhusu watu kufanya shughuli za kisiasa kila wakati ili kuongeza utendaji kazi wa watanzania badala ya shughuli za kisiasa kufanyika kila wakati na kila pahala,Naomba katiba ieleze wazi wazi shughuli za kisiasa zitakuwa zikifanywa mwaka mmoja kabla ya chaguzi au miezi kumi na miwili kabla ya uchaguzi husika, Na hili livibane vyama vyote no matter kuna ccm au chama gani chochote na kama kutakuwepo na shughuli za ufunguzi wa matawi au vikao vidogo basi vikao hivyo visizidishe zaidi ya watu 15 huku wakiomba vibali katika mamlaka pendekezwa.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
38,575
2,000
Ukipitia humu JF utagundua kuwa Watanzania wengi wanasumbuliwa na tatizo la akili fupi.Tatizo ni mfumo wa elimu yetu au ni nini?

Unaelewa kuwa mikutano ya kisiasa ni mojawapo ya freedom of expression?Unaelewa umuhimu wa freedom of expression?

Unaelewa kuwa ili Serikali iwe efficient and effective katika kutimiza wajibu wake ni lazima wananchi walioipa dhamana wawe wanaikumbusha majukumu yake mara kwa mara na kuikosoa mara kwa mara na hii hufanyika kupitia freedom of expression?

Unaelewa kuwa wananchi wanapokuwa limited katika ku-exercise freedom of expression ni kwamba wanailazimisha Serikali yao kulala fofofo katika kutimiza wajibu wake?Unaelewa kuwa serikali iliyolala fofofo katika kutimiza wajibu wake ni Serikali mfu?Yaani wewe unataka itungwe sheria ya kuwalazimisha wananchi kutengeneza serikali mfu?
 
serekali yetu ilishasema inapokea ushauri kwa mtu yoyote hata kukosoa lakini kukosoa huko kuwe kwa kistaarabu na si kutukanana sasa sijui ni uhuru gani tena unaoutafuta
 
mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
669
1,000
Hivi serikali inaogopa kukosolewa kwani yenyewe ni perfect? Mbona Mungu anakosolewa seuze serikali ya mwanadamu ambaye pua yake inaelekea ardhini?
Ccm ni kama wale watu walioonyeshwa kwenye filamu ya SALO: 100 days of Sodom ya mwaka 1974 na serbian film ya mwaka 2010.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
38,575
2,000
serekali yetu ilishasema inapokea ushauri kwa mtu yoyote hata kukosoa lakini
Serikali haina wajibu wala haki ya kudai au kusema kuwa inapokea ushauri kutoka kwa watu au inapokea kukosolewa kutoka kwa watu kwa sababu ni haki yetu kikatiba kuikosoa serikali.

Pia ni wajibu wetu kuishauri serikali.Sasa kama ni haki yetu kuikosoa serikali how comes wao waanze kudai kuwa wanakubali kukosolewa?Yaani suala la kuexercise haki zetu ni suala ambalo serikali inapaswa kukubali au ni suala la lazima?Yaani wanataka kutupangia jinsi ya ku-exercise haki zetu?WTF!!!
kukosoa huko kuwe kwa kistaarabu na si kutukanana sasa sijui ni uhuru gani tena unaoutafuta
Taifa huwa linaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria.Tunakosoa kwa mujibu wa katiba na sheria.

Kama kuna watu wanakosoa au kutoa ushauri kinyume na katiba na sheria zetu si washtakiwe kwa mujibu wa sheria zetu badala ya Serikali kulalamika?Tatizo liko wapi?Tokea lini suala la uvunjifu wa sheria za nchi likawa ni suala la serikali la kulia lia na kulalamika badala ya kuchukua hatua za kisheria?Maana yake Serikali imeshindwa majukumu yake,si ndo hivyo?WTF!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom