Msomi ni nani

MAGATA

Member
Jan 28, 2012
34
6
Jamani mimi na tatizo na maana ya mtu msomi, mtu kuitwa msomi anatakiwa awe na kiwango gani cha elimu? maana kijijini kwetu ukijua kusoma na kuandika tu wewe tayari msomi.

=====
MSOMI NI NANI AU NI MTU WA NAMNA GANI

Na: Comred Mbwana Allyamtu.


Hivi karibuni nilikuwa na mjadala mzito na na makomled wenzangu kuhusiana na dhana nzima ya mtu kujiita kuwa ni msomi.Chan zo cha mjadala huo ilikuwa ni pale nilipo waeleza kuwa kuna mahali siku ya leo nimealikwa katika meza ya mjadala juu ya mada ya "Msomi ni nani? Au ni mtu gani? Wakati tukiendele kulizungumzia hilo ndipo Comred mwenzangu aliponitaka niachane na biashara niliyoianzisha ili niendelee na elimu ya juu, kwani hapendi kuniona nikibobea katika biashara na binadamu bota ni yule ambaye ni msomi. Basi hapo ndipo nilipoanzisha mjadala wa kutaka kujua kwamba msomi ni mtu wa namna gani? Au je mtu anaweza kupimwa kwa vigezo gani ili aitwe kuwa ni msomi?

Mjadala huo ulikuwa ni mzito na uliochangamsha pale ofisini kwangu kwani kila mtu alipata nafasi ya kuchangia kwa mtazamo wake, na kutokana na mjadala huo nimejifunza mambo mengi sana kuhusiana na hii dhana ya mtu kuitwa kuwa ni msomi.

Hebu niwaulize wasomaji wa kwenye group hili na wanablog wenzangu, hivi msomi ni nani? Kama mtu amesomea taaluma fulani labda tuseme, udaktari, uhandisi au udaktari wa falsafa, Je huyu anaweza kujiita kuwa ni msomi?

Nimeuliza hivyo kwa sababu kama mtu ni msomi kwa maana ya dhana ya usomi tunayoifahamu, basi atakuwa anajua kile alichofundishwa na kukaririshwa tu akiwa darasani, lakini yeye mwenyewe hajawahi kuwa na kitu chochote kipya alichobuni.

Kama ni hivyo basi sioni kama kuna mtu anayeweza kujivuna kuwa yeye ni msomi.Atajiitaje kuwa ni msomi wakati amekaririshwa nadharia za wengine pasipo kubuni kitu chake mwenyewe?Nadhani hiyo inatosha kuvunja dhana ya watu kujiita wasomi.

Hivi ni nini tofauti kati ya msomi na yule ambaye hakuwahi kuingia darasani hata siku moja?

Kwangu mimi tofauti iliyopo labda ni kwamba, mmoja ametembea sana kutoka nyumbani hadi darasani na mwingine hajawahi kufanya hivyo hata siku moja. Huyu aliyetembea sana kwenda darasani kutafua elimu, amevuliwa akili yake na kupewa akili ambayo ni nadharia za watu wengine, zikiwemo zile sahihi na zisizofaa hata kuzitazama. Lakini amezikubali hizo nadharia na hivyo anaitwa kuwa ni msomi.

Kwa mfano ukienda chuo kikuu unafundishwa hata namna ya kulitazama jambo na kulihukumu kwa kutumia akili za watu wengine. Kile ulichokuja nacho, yaani imani na ufahamu wako kuhusu maisha, uchumi na siasa vinaondolewa na kuwekewa ambacho unatakiwa ukiamini na kukitetea kwa nguvu zako zote bila kuhoji, na hiyo itakufanya uitwe labda daktari wa falsafa na kutunukiwa digrii yako ya tatu, na kuanzia hapo utaitwa msomi!

Kumbuka kwamba digrii ni karatasi zaidi kuliko maarifa, ndio maana dunia nzima inasumbuliwa na wimbi la digrii feki.Ninachojua mimi ni kwamba wasomi wengi wa vyuo vikuu na madigrii yao ni wajinga sana kwenye maeneo mengine ya maisha.

Na jambo lingine ambalo linanishangaza, ni dunia hii kuendelea kukumbatia karatasi kama kipimo cha usomi. Unaweza kukuta mtu hajui chochote, lakini kwa sababu ana makaratasi yake yanayosema amesomea Shahada ya Uchumi, basi atapewa nafasi kubwa. Kisa ni karatasi!Halafu baadae mnashangaa, kwa sababu hana anachozalisha.Sasa usomi ni kitu gani, ni karatasi, ni kukariri nadharia za watu wengine, ni kujua jambo kwa undani au ni kujiuliza na kutafuta jibu?

Kuna watu wengi ambao nawafahamu, ambao wamekariri sana elimu ya darasani, wanayo madigrii lakini ukizungumza nao, utafikiri umekutana na mtu ambaye hajawahi kutia mguu darasani hata siku moja. Na wangine wako mitaani hawana kitu,na wamekata tamaa na maisha, kisa hakuna ajira.

Kwa kuamini kwamba karatasi ndizo zinazomfanya mtu kuwa msomi ndio maana sisi vijana wengi huko mashuleni na vyuoni tunajitahidi kushindana kukariri ili tufaulu sana na kupata digrii za viwango vya juu.Tunachotaka ni karatasi ili tupate ajira na wala sio maarifa. Tunapomaliza masomo tunatoka kama tulivyoingia na pengine tukiwa tumechuja zaidi kiufahamu.

Nimewahi kujiuliza swali hili, hivi watu kama Arstotle Sophocles, na baba wa elimu dunia kama Socrate na wale wajuzii wa kwanza kwanza duniani, walifundishwa na nani, walikaa darasa lipi na kupewa vyeti gani? Hadithi za kale utuambia kuwa mgunduzi wa Meli Arichimidis hakuwai kwenda dalasani kabisa lakin nadharia yake huishi mpaka leo na nizaidi ya miaka 1700 iliyopita. Lakini kuna watu kama Galileo Galilaya, Hopecus pia awajilui kabisa kitu kinachoitwa "kukaa dalasani".

Mwasisi wa somo la dhana ya falsafa ya sayansi ya historia duniani Hipecus na mwasisi wa dhana ya daktali duniani Hipocratus ni nani aliowafundisha? Kama msomi shariti lake lazima ukae dalasani?
Hawa hawakukaa darasani, bali walizalisha maarifa baada ya tafakari kubwa na ya muda mrefu. Walijiuliza maswali ili kupata majibu, waweze kuisaidia jamii hapa duniani.

Kwa mtazamo wangu hawa ndio wasomi, kwa sababu utafiti wao unagusa kila eneo la maarifa bila kujali kama ni sayansi, biashara, tiba au sanaa. Kwa mantiki hii msomi sio mtu mwenye makaratasi bali msomi ni mbobezi wa kujiuliza maswali na kutafuta ufumbuzi juu ya maswali yake. Lazima msomi awe na matokeo chanya katika jamii juu ya maarifa yake binafsi sio maarifa ya kukarilishwa kutoka kwenye nadharia za watu ambao ndio walikuwa wasomi.
Msomi ni mtu aliye huru kutafuta maswali kuhusu maisha yetu.

Mtawala wa kwanza wa Dola ya Rumi (Rome Empire) Jurius Kaisal alipo lihutubia Balaza la Seneti (COUNCULIS SENETI) lake la kwanza kabisa alilo buni kama njia ya kurahisisha utawala kwa watu wake karne ya 15th BCE alisema
"Maarifa ni zao la akili linalotokana na ubunifu wa mawazo ambayo mtu ujiuliza kwa kina na kutafuta ufubuzi yakinifu na kisha kutoa matokeo yatakao ishangaza jamii na kimsingi huyu ndio msomi" lengo langu sio kueleza habari za huyu bwana ila nimejalibu kuweka nukuu hii ili tuweze kumjua msomi ni nani?

Sasa DUNIA imekuwa na watu kibao wanaojiita wasomi lakini ndio hao awawezi hata kujipambanua katika yale yanayo wasibu katika mazingira yanayowazunguka. Nakumbukahawa hawa tunao waita wasomi ndio hawa waliotufikisha hapa kwenye wimbi la ufisadi, urafi wa mali za wanyonge, ukadamizaji wa haki za binadamu, ubinafsi, ubaguzi wa rangi, kutetea ushoga, uongo uliokithili, na uchonganishi baina ya binadamu, katika uso wa DUNIA hii lakini bado wameendelea kuitwa eti wasomi sababu wanamiliki mafaili ya makaratasi ya vyeti.

Ndimi
Comred Mbwana Allyamtu

+255765026057
+255679555526
Mbwanaallyamtu990@gmail. Com

View attachment 364492
Nadhani msomi, ni yule aliye ktk mchakato mzima wa kusoma. Tofautisha na mhitimu. Kubwa kabisa. Yule aliejaaliwa kuwa msomi wa kiwango cha kutukuka huwa na sifa ya kutokuwa na dharau. Hususan kwa watu ambao hayuko nao ktk taasisi yake anayofanyia mchakato wake wa kusoma, akitambua kuwa kusoma kwa kiasi kikubwa ni kujifunza kwa kuishi.

Anayetambua, msomi ni yule anaeishi maisha yake yote, akijifunza. Hususan mwenyewe, na akiheshimu wasomi wengine wanaojifunza wenyewe na kazi zao. Shaaban Robert wa Tanzania, ni mfano mmoja, na wengine wengi wapo, msomi hana kibri. Ana heshima, ana ushujaa wa kuukubali ukweli. Kinyume cha hapo, ni kinyume cha msomi. Tuseme ni limbukeni wa kitu kidogo alichomaliza kujifunza na nachobakia anakimiliki kwenye mawazo yake tu.
Habari waungwana!
Nimejitokeza hapa kuuliza ili tuwekane sawa kuhusu hili neno "MSOMI"

Kwa utangulizi kuna mambo yanayopaswa kuzingatiwa, nayo ni kama ifuatavyo:
a) Elimu (Knowledge)
b) Ujuzi (SKills)
c) Uelewa (Understanding) na
d) Umahili (Attributes)

Wengi wanachanganya mambo hayo hapo juu. Wakati nikiendelea kusubiri michango ya mawazo, nawaombeni pia tujikite kwenye ufafanuzi wa kina ili neno hili MSOMI liweze kueleweka vyema pasipo kupotoshana.

Kwa upande wa mimi msomi sio yale makaratasi ya kukutambulisha kwamba umesoma, usomi ni ule utakaokufanya kukubalika tangu a mpaka d...
Wasemaje mwanaJF
Naona uzi unatiririka na waliokimbia umande...poleni
Msomi kwa lugha ya kimombo ni Intellectuals, ni yule aliemaliza hatua zote za masomo hadi kufikia ngazi ya chuo kikuu na kubobea moja wapo ya taaluma zinazotolewa huko......
Kwamba sijui mazingira, sijui kubadili maisha....haina uhusiano...life is how you make it....full stop
1. Msomi ni yule alaienda shule mfano sekondary mpk chuo kikuu...
2. Mwenye elimu huyu ni mtu mwenye uelewa na kitu fulan anaweza kua msomi au asiwe msomi ila akawa na ufahamu na maswala fulan mfano mtu ambae hajasoma lakini ana yajau mambo ya dunia mfano elimu dunia
Je !kwenda shule/chuo ukawa na sifa ya kumliki vyeo vya kisomi ndo unakuwa umeelimika au umesoma?

Hivi kwenda shule then ukaishi maisha ya umasikini je!unakuwa hujui kutumia usomi wako vizuri?

Leo nimeinamisha kichwa nikijiuliza maswali hapo juu na nikaona pia Wasomi ni zao la elimu na kupitia elimu tunapata wasomi,baada ya hapo kwa leo nimepata sifa mbili za wasomi wenye faida nakuzitazama katika jicho lifuatalo.

1.Wasomi ni wale wenye ari ya kuisaidia jamii kukua na kubadilika kimaendeleo(Nyenzo ya mabadiliko). zaidi ya hapo utakuwa ni usomaji na si usomi unaokusudiwa,na Kwa bahati mbaya sana asilimia kubwa katika sisi elimu tunayoipata tunalenga tu kujipatia mahitaji binafsi (private needs),mwisho wa siku inapelekea profesa au daktari nk. anaishia katika kadhia ya ufisadi.

2.Wasomi wanatakiwa wawena uwezo wa kufanya mambo ya sawasawa kwa namna ya sawasawa na kwa wakati wa sawasawa katika mazingira ya sawasawa(hekima),zaidi ya hapo ni msomi ambaye jamii itakuwa inapata hasara kwa usomi wake.

NB:Tunaweza kumtambua daktari mzuri kwa kupata matibabu na sio kwa mavazi ya udaktari,Tunaweza kumpata mpishi mzuri kwa kuonja chakula alichokipika japo sio kila kitu kizuri lazima ukipate kwa kuonja isipokuwa hata harufu nzuri inatosha,kwa namna kama hiyo tunaweza kutambua msomi mzuri kwa matunda yake.

(UTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO)
SIFA 50 ZA MSOMI...JITATHMINI KAMA UNAFITI.


  1. Msomi ni mtu mwenye uwezo fikra huru na mwenye uwezo wa kujitegemea.
  2. Msomi ana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
  3. Mtu mwenye elimu anajua jinsi ya kujifunza.
  4. Msomi anajua kuiandika na kuizungumza kwa ufasaha/usahihi lugha yake ya kwanza na lugha ya kujifunzia.
  5. Msomi anajua namna sahihi ya kutumia rasilimali zilizopo, kuimarisha mchakato unaohitajika ili ajifunze ujuzi fulani, na kujaribu njia zinazofaa.(my take: Hapa wale wanaokosa ajira angali ni wasomi wajitathmini).
  6. Msomi hufanya bidii kuepuka unafiki.
  7. Mtu mwenye ujuzi ana uwezo wa kuwasiliana/kuwasilisha mawazo yake au ya kitaaluma kwa maandishi, kwa uwazi na kwa ufupi; atabainisha chanzo cha ujuzi huo.
  8. Msomi ana uwezo wa kusema vizuri.
  9. Msomi ana uwezo wa kufikiria kwa uchunguzi na kwa kiasi kikubwa.
  10. Msomi ana uwezo wa kufikiria kwa hesabu za KUJUMLISHA,KUZIDISHA na KUTOA.
  11. Msomi ana ufahamu mkubwa juu ya Habari muhimu za Taifa lake,Kimataifa na nyanja za taaluma yake(Current Affairs). Sio tukuulize Profesa M. Assad ni nani hujui hapo tunakufuta usomi. Au nini kinaendelea Venezuela hujui. Tunakufuta.
  12. Msomi hakubali kwa upofu yale anayoambiwa; msomi huenda kuona/kushuhudia yeye wenyewe kile anachoambiwa(ataenda kuona ana kwa ana ama kwa utafiti tunduizi).
  13. Msomi anajua jinsi ya kutofautisha kati ya taarifa zinazofaa na zisizo (anatofautisha kati jambo muhimu na jambo dogo).
  14. Msomi anajua jinsi ya kufanya matumizi mazuri ya maarifa; anajua wapi atapata ujuzi ambao anauhitaji, na ana uwezo wa kuandaa ujuzi huo katika mpango wa utekelezaji unaoelekezwa mwisho wenye hatima chanya.
  15. Msomi anaelewa asili ya mwanadamu na ana uwezo wa kuanzisha, kudumisha, na kuboresha uhusiano wa kudumu na mwanadamu mwenzake.
  16. Mtu mwenye elimu anajua jinsi ya kuanzisha uhusiano na wengine(ku-establish rapport); anajua jinsi wengine wanavyomuamini na kumheshimu kwa sifa yake ya usomi(Si mjivuni kwa usomi wake).
  17. Msomi ana nidhamu (Katika kauli,mavazi,mahusiano,imani,taasisi na serikali).
  18. Msomi anajua jinsi ya kutatua migogoro na/ya wengine.
  19. Msomi anajua jinsi ya kuwashawishi wengine.
  20. Msomi ana uwezo wa kufikiria na kutatua matatizo.
  21. Msomi anajua jinsi ya kufanya maamuzi.
  22. Msomi anaweza kuvuka mipaka ya tahadhari na kuchunguza matatizo na kupata ufumbuzi wake kwa kutumia njia mtambuka.
  23. Msomi ni mtu ambaye amefundishwa kikamilifu: kiubunifu, kiutamaduni, kiroho, kimaadili, kimwili, teknolojia, na kiakili.
  24. Msomi ana elimu ya upana wa sanaa. Ana maoni mazuri ya masomo yafuatayo: sayansi ya asili; sayansi ya kijamii;hisabati; historia; jiografia; fasihi; falsafa; na teolojia.
  25. Msomi ana ujuzi wa kina-yaani, ujuzi maalum - katika fani fulani.
  26. Msomi amefanikiwa kushinda; anajua jinsi ya kufikia malengo muhimu ya muda mfupi na mrefu (Msomi si mtu wa kulia lia anatafuta suluhu kwani jamii inamtegemea atoe majawabu).
  27. Msomi ana uwezo wa kuvumilia na kuvumilia.
  28. Msomi anajitambua; anajua jinsi ya kuzisimamia hisia zake za ndani.
  29. Msomi ana maadili na huyazingatia kwa dhati.
  30. Msomi ana uwezo na nidhamu ya kufanya yaliyo sawa.
  31. Msomi anaufahamu na kuuenzi utamaduni wake mzuri.
  32. Msomi ana heshima kwa kila mtu, bila kujali jinsia, rangi, dini, nchi ya asili, na kadhalika.
  33. Msomi anatambua wajibu wake.
  34. Msomi anaweza kufanya mambo mapya; ana uwezo wa kuzalisha mawazo na kugeuza kuwa ukweli/uhalisia. Msomi ni mbunifu.
  35. Msomi ni mdadisi.
  36. Msomi ana uwezo wa kutambua tabia na tabia zinazohitajika katika jamii husika.
  37. Msomi ana uwezo wa kutambua tabia na sifa za hatari- Mfano ngono zembe.
  38. Msomi ana uwezo wa kuirekebisha jamii.
  39. Msomi hukubali wakati anapokosea na hujirekebisha.
  40. Msomi habishani,bali hutoa hoja (Ukibishana tu ushaondoa sifa ya usomi)
  41. Msomi anaweza kubadilika na anajua jinsi ya kukabiliana na mabadiliko.
  42. Msomi anajua jinsi ya kushughulikia utata.
  43. Msomi ana uwezo wa kuchunguza mawazo mbadala.
  44. Msomi ana shukrani;
  45. Msomi anaweza kufanya moja kati ya kuimba, kucheza vizuri, kucheza angalau chombo cha muziki kimoja, na anaweza kufahamu usanifu, sanaa nzuri, na maneno mengine ya ubunifu wa ubunifu.
  46. Msomi anafahamu umuhimu wa familia na jinsi ya kuimarisha familia kama msingi wa kuendeleza kizazi/vizazi bora.
  47. Msomi ni yule ambae anayo falsafa yake binafsi ambayo itawawezesha kuwa na furaha na mafanikio.
  48. Mtu mwenye elimu ana uwezo na kuhariri wazo katika mfumo wowote wa maandishi au mfumo wowote.
  49. Msomi hadharau elimu mpya inayopatikana kwenye mazingira yake.
  50. Msomi huwa nadhifu.
 
Jamani mi na tatizo na maana ya mtu msomi, mtu kuitwa msomi anatakiwa awe na kiwango gani cha elimu? maana kijijini kwetu ukijua kusoma na kuandika tu we tayari msomi.

Kwa upande wangu mimi nadhani mtu yoyote ambaye anajua kusoma na kuandika ni msomi
 
Hawa ndio wanaharibu hapa jf utani. Wengine tushazoea kabla ya kulala tucheke kidogo kupitia hapa watu wanaandika uj**ga.
Aha shit ngoja nilale mie.
 
Jamani mi na tatizo na maana ya mtu msomi, mtu kuitwa msomi anatakiwa awe na kiwango gani cha elimu? maana kijijini kwetu ukijua kusoma na kuandika tu we tayari msomi.

Yeah! true that!
 
Inategemea mtu ana kiwango gani cha uelewa otherwise kwa baadhi ya vijiji msomi ni yeyote anyejua kusoma
 
Aliye na kiwango cha kuweza kuishi vizuri na watu wa aina, tabia na mazingira yote.
 
Nadhani kuwa msomi ni mtu yeyote aliyepata elim yoyote ile japo elimu yenyewe imegawanyika ktk level tofauti kama elim ya msingi, sekondari, stashahada au shahada na nyinginezo nyingi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom