Ipi tofauti kati ya mauaji ya East Timor na Myanmar

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,900
30,235
Utangulizi
Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ni kijana hodari mwenye kujua kuchagua maneno yake vyema. Hapo chini ameandika masikitiko yake kuhusu Tanzania kukataa kupiga kura kulaani mauaji ya Waislam Myanmar. Katika maandishi yake neno, ''Waislam,'' halipo. Lakini dunia nzima inajua kuwa wanaouliwa Myanmar ni Waislam si suala la kuuliwa ''wananchi.''

Iwe itakavyokuwa Zitto Kabwe kaeleza masikitiko yake ili Watanzania wajue nini kimetokea. Kwa sera ya Tanzania kuhusu msimamo wake wa kusimamia haki duniani kote kitendo haya ni mabadiliko makubwa sana katika msimamo huo uliowafikisha Watanzania kupigana Msumbiji bega kwa bega na Frelimo na kutoa misaada kote kulikokuwa na dhulma sawa na kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliposema, ''Tunataka kuwasha mwenge uangaze kote na kuleta matumaini kule watu walikokata tamaa.''

Hii sera mpya ya kushindwa kulaani mauaji ya Waislam wanaouliwa Myanmar huenda hii ikawa ni sera mpya ambayo kwa sasa ndiyo inaongoza Tanzania na uhusiano wake na mataifa mengine. Ndiyo kusema kuwa sasa Tanzania haijali tena dhulma bali inaongozwa na maslahi yake mengine ambayo kwa bahati mbaya kwa sasa hayajakuwa bayana.
Tanzania ilianza na kurejesha uhusiano na Israel uliovunjwa na Baba wa Taifa mwenyewe nusu karne iliyopita.

Leo Tanzania imeridhia kutopiga kura kwenye mauaji ya kimbari ya Waislam wa Mynmar.
Wachunguzi wa siasa wanasubiri kutazama nini lingine litafuatia. Labda hilo litatoa mwanga zaidi kuonyesha nchi yetu imesimama upande gani na kwa nini.

Swali la kujiuliza ni hili: Ingekuwa ni kura ya East Timor na wanaouliwa ni Wakatoliki Tanzania ingekaa pembeni ikaacha kupiga kura?

Jibu unalo wewe ndugu msomaji wangu.









Unaweza kusoma historia ya Tanganyika na Palestine hapo chini:
Mohamed Said: BAADA YA KUONDOKA BABA WA TAIFA TANZANIA BADO INAUNGA MKONO PALESTINA? SIKU YA QUDS - STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR
 
Tuwe wakweli tu sera yetu ya Mambo ya nje imepwaya sana.

Tulianza na kumkaribisha kiongozi wa Morocco wakati inajulikana toka enzi tunawaunga mkono Polisario


Heshima ya Nchi nje ya mipaka yake ni pamoja na kuwa sera stahiki za Kidiplomasia na zinazozingatiwa.

Nini kimemsibu Mahiga anayeijua Nchi yetu na Diplomasia ya Dunia kindakindaki?
 
Hoja nzuri,
Lakini kwanini pia tusilaani mauaji ya kutisha na ya kikatili yanayofanywa na magaidi? Hamas, Islamic State, al qaida,boko haram, n.k?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom