Ipi tiba ya tatizo sugu la M'BA kwenye ngozi?

Premij canoon

JF-Expert Member
May 27, 2018
1,108
2,473
Wanajamii poleni na msiba wa taifa...

Kama mada inavyojieleza, ni ipo tiba ya m'ba kwenye ngozi, mimi nasumbuliwa na m'ba mara kwa mara.

Yaani ni kama nina allerg ya ngozi, nikitumia dawa za kupaka wanaisha baada ya mida wanarudi tena.

Nimegundua hili tatizo lipo ndani ya mwili inahitajika dawa ya kunywa na kupaka.

Nimechoshwa na matumizi ya dawa mara kwa mara, nahitaji tiba ya kutatua tatizo lisirudi tena. Kwa anaefahamu dawa itakayonisaidia tafadhali naomba msaada.

NB : Ngozi yangu ni ya mafuta.
 
Nenda Kairuki hospital pale nlikua na tatizo hilo kuna daktari wa ngozi nilipewa akaniangalia akanipa dawa za kumeza nlitumia tatizo liliisha ilikua 2017 hadi leo nikikumbuka jina la zile dawa ntaituma hapa
 
Dawa za kunywa ndio nzuri zaidi, nenda hata kwenye pharmacy kubwa kubwa utapata dawa. Zamani zilinusumbua sana, kila ukipaka dawa inaonekana kuna vijisehemu vinabaki, baada ya muda zinarudi. Dawa ya kumeza ilimaliza jumla jumla
 
Nenda kairuki hospital pale nlikua na tatizo hilo kuna daktari wa ngozi nilipewa akaniangalia akanipa dawa za kumeza nlitumia tatizo liliisha ilikua 2017 hadi leo nikikumbuka jina la zile dawa ntaituma hapa

Itakua vyema mkuu
 
Dawa za kunywa ndio nzuri zaidi, nenda hata kwenye pharmacy kubwa kubwa utapata dawa. Zamani zilinusumbua sana, kila ukipaka dawa inaonekana kuna vijisehemu vinabaki, baada ya muda zinarudi. Dawa ya kumeza ilimaliza jumla jumla

Ni dawa gani ulitumia mkuu?
 
Mba walinisumhua sana dah..muda mwingine hata umaskini nao unachangia maana nilikuwa siwezi afford dawa za gharama, nimekuja kupona 2008 na nilipewa dawa za kunywa!

Kama wadau walivyoshauri dawa za kunywa ni best option, cha msingi nenda hospital ya kueleweka na uonane na daktari wa ngozi!
 
Kama ni Fangasi kuna dawa hizo za kunywa, dawa moja inaitwa Griseofulvin. Lakini inatakiwa kupima kujiridhisha kuwa ni fangasi maana yapo magonjwa mengi sana ya ngozi yanakuwa si fangasi bali ya kurithi(genetic)
 
Kama ni Fangasi kuna dawa hizo za kunywa, dawa moja inaitwa Griseofulvin. Lakini inatakiwa kupima kujiridhisha kuwa ni fangasi maana yapo magonjwa mengi sana ya ngozi yanakuwa si fangasi bali ya kurithi(genetic)
Hivi hii dawa kama una fangasi unatumia mwezi mzima au?...
 
Ni kuoga na kujisugua na kitambaa mwilini pia kujikausha maji vzr mimi n8litumia dawa hii imenisaidia ndani ya week 2 zimeisha zote
JPEG_20210427_003804_5987194319604673243.jpg
 
Kama wahusika na matabibu wa asili tunayo mafuta spesho kwaajil ya kutibu tatizo hilo
 
Kwanini wameizuia mkuu..?
Ketoconazole ina side effect mbaya sana..Orally taken.

✓Kwa wanaume inasababisha testosterone kupungua..kwa hiyo inashusha sana nguvu za kiume na kusababisha uhanithi(impotence)..(Anti-androgenic)

✓Kwa wanawake pia inaleta shida kwenye ovaries..kwahiyo uzazi utakuwa wa shida.

✓Inasababisha upara.

✓Inasababisha adrenal gland kushindwa kuzalisha hormone zake kama ilivyozoeleka.

Hii dawa itatumika tu pale faida zitakapozi over-weigh hasara..

Though,shampoo na cream yake ni nzuri na haina shida sana kama ya kumeza.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom