Ipi siri ya kanisa Katoliki kujimilikisha ardhi kubwa kwa jina la Vatican?

Hongera kwa kuwa umekwishaokoka hapa duniani na hauna dhambi, hivyo utamwona Mungu!
ukiokoka sio kwamba hautakuwa na dhambi, maana yake umeingia mkataba na Mungu wa kumfuata kwa njia ya Yesu Kristo, ili nguvu za Mungu zikusaidie kushida dhambi na ukitenda dhambi bado unakuwa na mwombezi kwa Baba Yesu Kristo anayesimama kama wakili wetu. tunampokea wakili/advocate wetu kutuombea kwa Baba ambaye bila huyo hautamwona Mungu. wasiookoka hawana advocate hivyo wapo chini ya laaana na mauti kwasababu hawajampokea mkombozi wa maisha yao katika mioyo yao. hio ndio maana ya kuokoka. tunaposema muiokoke ni kwamba mumkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi, na muamini mioyoni mwenu kwamba Mungu alimfufua katika wafu na kwamba yeye pekee ndiye njia kweli na uzima wa milele. baada ya hapo mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye ndiye Mungu huyohuyo mwenyewe, ili akikaa ndani yenu muishi maisha ya kiroho ya kuongozwa naye.

maandiko yanasema "awaye yote asiyekuwa na huyo Roho wa Kristo, huyo sio wake", maana yake kama huna Roho Mtakatifu wewe sio mali ya Mungu, ni mali ya Shetani. na tunajua kama tunaye Roho pale tutakapomwona anajidhihirisha maishani mwetu physically, na ishara mojawapo ni kunena kwa lugha mpya au lugha ya malaika, pale anapokuwa anakusaidia kuomba kwasababu kwa akili zetu hatuwezi kuomba ipasavyo, ila Roho mwenyewe hulia kwa kuugua ndani yetu akisema "aba" yaani Baba, na huweza kupresent mambo ambayo kwa akili yetu tusingeweza. nyote mnaoomba kwa akili siku zote huomba kwa kufuata tamaa zenu za mwili tu, magari, nyumba, mke watoto n.k, wakati Roho anajua mnahitaji zaidi ya hivyo. Mungu akusaidie.
 
Mleta mada kanisa ni taasisi, waliojenga Vatican pia wameshatangulia mbele za haki lakini bado Vatican ipo.

Ardhi wanayomiliki huiendeleza kwa miradi ya maendeleo kama kilimo, shule na hospital. Vatican Ina majengo katika miji yote mikubwa ya dunia na pango la majengo ndiyo inaifanya inatumika kujenga hospital na shule kwenye uhitaji.
Akisoma shule au akienda hospitali za kanisa hasemi chohote
 
Kanisa Katoliki kwa miaka nenda rudi wamekuwa na utamaduni wa kujilimbikizia maeneo makubwa ya ardhi nchi mbalimbali, na ardhi hiyo huwa inasauiliwa Vatican kama milki yao halali.

Kanisa limekuwa likifundisha kwamba tusijiwekee akiba duniani, lakini lenyewe ndio kinara wa kujilimbikizia ardhi.

Mathayo 6:19-20​

“Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba."

Haya mafundisho naona yanakinzana na kile ambacho kanisa linakifanya. Sasa ningependa kujua nini dhamira ya kanisa kumiliki haya maeneo makubwa? Kijijini ni mfano tu, kanisa linamiliki zaidi ya heka mia mbili, za nini zote hizi kama sio ulafi tu na ubinafsi?

Hebu tujulishane nyuma ya mpango huu kuna nini kilichojificha?

Kwanini ardhi isajiliwe kama ni mali ya Serikali ya Vatican?
Sababu ni rahisi kuwa kanisa hili ndilo lililowezesha ukoloni kutamalaki duniani. Hivyo, wakoloni waliolitumia waliona ni vizuri kulizawadia ardhi ili liendelee na ukabaila wake wa kimfumo kama kawa. Kanisa nalo ni taasisi ya kikoloni ambayo wengi walishindwa kuistukia kwa hasara yao.
 
Back
Top Bottom