Ipi siri ya kanisa Katoliki kujimilikisha ardhi kubwa kwa jina la Vatican?

Burundi, Mozambique, DRC, Congo Brazaville, Afghanstan...hawa hawana waislamu eeh? Anyway, mimi ninavyojua kutafuta excuse ni kujifariji nafsi ila sio dawa ya tatizo.
Na Tanzania je? Kenya? Rwanda? Hii mada unavyoiweka inaonyesha tatizo lile lile linalotusumbua...ufinyu wetu wa fikra. Na kufikiri dawa ni kubadilisha wananchi wote tuwe dini moja ya kiislamu.
Hilo halitakaa kutokea. Maendeleo tuamue tuyatafute kwa nguvu kama raia. Tukianza kuendekeza inferiority complexes zetu, tutakuwa tunajidanganya nafsi.
By the way, hizi dini zipo toka karne na karne na wamepigana vita kama vyote na hakuwahi kutokea mshindi. Unafikiri ni kwanini? Fanya kazi ndio msingi wa maendeleo. Muabudu mwenyezi Mungu ndio chanzo cha hekima na maarifa. Nyingine hizi hadithi ambazo hazina mbele wala nyuma
Mpaka india yaan ule umaskini ni catholism ujue nimeshtukaa.. anasema uongooo..
 
Kwani hio google imetengenezwa na bibi yako Chato.......google ni kama bahari,ambapo vessel yeyote inaweza kuflow,......by the way unataka Tanzania iwepo wakati ,ina wakatoliki wachache wapo sana Mtwara,Kagera,Songea,Morogoro sehemu zinazojulikana kabisa kua na masikini wa kiwango cha SGR.........au unadhani Zanzibar,Dsm sio Tanzania?
Mbona hutaji kilimanjaro aisee arguement yako kiboko...
 
wew hiz data unazitoa wap? Wakati USA Kila waliko wamarekani watano mmoja mkatoliki.


Bado hujaenda Germany,France, Belgium nk Tena Hawa ndo wameleta ukatoliki Africa.

Bado Spain na Portugal huko ukatoliki Kama wote

Yaan unajua amenishangaza sana jamaa. Halaf ameshupaza shingo balaa... kisa anaona watu yooh yooh ndo anajua si wakatoliki? Ama anafikiri anapajua yeye tu. Tuna familia na jamaa zetu na wnaapenda mnoo maendeleo hao. Na makanisa ya catholic hasa wakati huu wanatoa misaada balaa huko. Makanisa mengine unaambiwa wanabagua kwelikweli.

Unajua tatizo ni kwamba kanisa katoliki huwezi wakuta wanabrag ovyo kwa lolote liwe kubwa ama dogo. Hata siku moja. Na huduma kwa jamii ndo jadi ya kanisa... and its amongest the powerful institutions in the world...
 
Shida moja naiona ni kwamba kanisa limewekeza sana kwa watu maskini na nchi maskini limejenga huko huduma za jamii kama mashule,vyuo,hospital,na mambo mengine mengi,kanisa kanisa lisingeenda kufanya hayo maendeleo maeneo sijui hali yao ingekuwaje ,kwa uhakika hao watu lazima wakatoliki kwa ndio waliopo hapo(minus catholic investments=zero development in that specific area) baadaa ya wanasingiziwa wao sasa kwamba ndio wamepeleka umaskini,chukulia maeneo maarufu ya mission Tanzania hii wengi tunayajua,then assume unaondoa kila kitu walichofanya wao since then,pangekuwa na nini?kumbuka maeneo hayo kwa sasa ndio yanaongoza kwa kutoa wasomi wengi,je serikali ingewekeza sawa na ilivyo sasa katika maeneo hayo hayo?

Mtu akikupa elimu kakupa kila kitu. Najiuliza, sisi tumesoma na kuelimika? Tunapambanaje na changamoto zetu za kila siku kama wasomi? Mbona kama ndio worse kuliko wasiosoma?
Hapo shida sio dini...shida tunayo wenyewe
 
Kanisa Katoliki kwa miaka nenda rudi wamekuwa na utamaduni wa kujilimbikizia maeneo makubwa ya ardhi nchi mbalimbali, na ardhi hiyo huwa inasauiliwa Vatican kama milki yao halali.

Kanisa limekuwa likifundisha kwamba tusijiwekee akiba duniani, lakini lenyewe ndio kinara wa kujilimbikizia ardhi.

Mathayo 6:19-20​

“Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba. Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba."

Haya mafundisho naona yanakinzana na kile ambacho kanisa linakifanya. Sasa ningependa kujua nini dhamira ya kanisa kumiliki haya maeneo makubwa? Kijijini ni mfano tu, kanisa linamiliki zaidi ya heka mia mbili, za nini zote hizi kama sio ulafi tu na ubinafsi?

Hebu tujulishane nyuma ya mpango huu kuna nini kilichojificha?

Kwanini ardhi isajiliwe kama ni mali ya Serikali ya Vatican?
1. Unapolituhumu Kanisa Katoliki "kujimilikisha ardhi" inabidi uwe na mifano halisi ili hoja yako isimame yenyewe.
2. "Kujimilikisha ardhi" ni dhana hasi - "land grabbing" - kuchukua ardhi ya mtu au ya umma bila kuwa na haki ya kufanya hivyo.
3. Kanisa Katoliki katika sehemu mbalimbali duniani inamiliki ardhi kihalali - 1) ama kumiliki ardhi kwa sheria ya kimila (mfano, kufyeka pori ambalo halijatumika, ambayo kisheria ni njia mojawapo ya kumiliki ardhi) au 2) kumiliki ardhi kwa kupata hati miliki (title deed).
4. Ardhi yote inayomolikiwa na Kanisa Katoliki si mali ya papa, kardinali, askofu, padri, katekista, kiongozi etc, bali ni mali ya walei na ni kwa ajili ya mahitaji ya huduma za kanisa - kujenga shule/chuo, hospitali, vituo vya kulelea watoto, karakana kwa ajili ya mafunzo stadi ya vijana na pia kwa ajili ya makazi ya wananchi wanaozunguka eneo la Kanisa. Mfano, wakazi wengi wa maeneo ya Kanisa Katoliki wamepewa ardhi na kujenga makazi yao na kama siku moja kanisa litahitaji kuchukua ardhi kama hiyo, litawafidia hao wananchi kwa muda wote ambao wameendeleza ardhi yao.
5. Ardhi inayotolewa kwa Kanisa Katoliki haitolewi na kumilikiwa na Vatican, bali na kanisa parokia au jimbo (kanisa mahalia).
6. Huna ushahidi wowote unaoonyesha kwa mfano hivi karibuni tumemilikishwa ardhi ya kujenga kigango maeneo ninapokaa hapa Dar es Salaam na kwenye hati hakuna jina la Vatican.
7. Yesu aliposema 'msijiwekee hazina hapa duniani' (Mathayo 6:19-20) hakuwa na maana kwamba watu au Kanisa lisimiliki ardhi, bali kwamba umiliki wao wa ardhi usije ukawa chanzo cha kumsahau Mwenyezi Mungu (mfano anayepora ardhi ya watu kwa masilahi binafsi amemsahau Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu anataka utende haki na siyo kuwaibia au kuwanyonya watu).
8. Badala ya kujenga hoja inayoeleweka, hapa umeamua kutulisha 'matango pori' kwa sababu umeshtumu tu na hujaonyesha kwa ushahidi ni kwa jinsi gani Kanisa limewapora watu ardhi au limepora ardhi ya umma kwa kutumia Vatican. Hivyo, yako ni "hoja zoa zoa".
 
1. Umeongea vizuri mwanzoni,
2) lakini umeweka ugolo mwishoni.
3. Wewe siyo Mungu ujue ni nani atakayeokoka na ni nani hataokoka.
4. Yaani, unataka kusema Wakatoliki wote duniani wapatao bilioni 1.2 hawataokoka, isipokuwa wewe tu na wenzako.
5. Wewe kwa kuwa 'obsessed' kwamba Wakatoliki wanaabudu masanamu tayari unaabudu sanamu. 'Kuabudu sanamu' maana yake kuwa 'obsessed' na kitu au jambo fulani to the extent kwamba umesahau au umeshindwa kabisa kumwabudu Mungu wa kweli isipokuwa hiyo 'obsession' yako inayokuzuia kuona mema wanayotenda Wakatoliki.
 
Kagera,Mtwara,Ruvuma mbona hujaziweka kiongozi?
Hiyo mikoa itakuwa na sababu zake lakin sio ukatoliki



Mkoa Kama kagera kwa mfan mkoa huu una sehemu zenye wakatoliki kibao mfano muleba, bukoba,misenyi, karagwe na kyerwa na ndo wilaya zenye maendeleo mpaka vijijini Kuna shule, hospital Kama zote kuliko zenye wakatoliki wachache Kama biharamulo na ngara


Mkoa wa kagera una hospital 15 za kikatoliki serikali Kuna moja tu

Njoo kwenye shule wilaya ya muleba ndo yenye shule nyingi nchini baada ya Moshi ambayo nayo inawakatoliki Kama wote.



Hiv kwa akili yako maendeleo yaliyoko vijijini huko bukoba unaweza linganisha na vijiji vya pwani, Lindi,Tanga au mtwara?
 
Lileta mada ni popoma! Mbona Mali zetu zimeandikishwa kwa jina la jimbo? Hujaona hata shule huwa wameanza na Diocese of ....., hakuna mahali hati milki zimeandikwa kwa jina la Vatican! Umeandika ujinga mwamba!
 
1. Umeongea vizuri mwanzoni,
2) lakini umeweka ugolo mwishoni.
3. Wewe siyo Mungu ujue ni nani atakayeokoka na ni nani hataokoka.
4. Yaani, unataka kusema Wakatoliki wote duniani wapatao bilioni 1.2 hawataokoka, isipokuwa wewe tu na wenzako.
5. Wewe kwa kuwa 'obsessed' kwamba Wakatoliki wanaabudu masanamu tayari unaabudu sanamu. 'Kuabudu sanamu' maana yake kuwa 'obsessed' na kitu au jambo fulani to the extent kwamba umesahau au umeshindwa kabisa kumwabudu Mungu wa kweli isipokuwa hiyo 'obsession' yako inayokuzuia kuona mema wanayotenda Wakatoliki.
Husda tu
 
Sio kweli kwamba ardhi ya katoliki huwa mali ya vatican. mali miliki ya vatican ni pale tu kwenye embassy yao, na hiyo ni diplomatically. kwingien kote kanisa hili limesajiliwa na hadhi sawa tu kama makanisa mengine na wanapomiliki humiliki kama NGOs zingine tu. isipokuwa, ujanja wao huwa wanafanya ni kwenda pembezoni mwa mji mapema kabisa wanawekak mission huko na baadaye mji huwa unawafuata ndio maana unaweza kuona kama wanamiliki maeneo makubwa, ni kwamba wanakuwa waliyapata mapema maeneo ambayo ninyi mlikuwa mnayadharau na kuyaona ni bush. wanajenga kanisa, shule n.k. mimi sio mkatoliki lakini kati ya makanisa yanayoleta maendeleo ya kweli wakatoliki ni namba moja. pamoja na kwamba hawajaokoka na hawatakuja kumwona Mungu hadi waache kuabudu sanamu na maria.
Hata ubalozi ulipo huenda siyo Mali ya Vatican. Yawezekana wanapanga. Siyo lazima wajenge. Nchi yingi hizo ardhi makanisa walipewa na serikali bure ili watoe huduma mbalimbali. To complement govt services. Nchi yingi wana vyuo, mahospitali, shule etc. nashangaa bongo wanalipa kodi. Nchi zingine serikali hulipa makanisa kwa kutoa huduma hizo. Mixture of private and public services.
 
kwani imani zingine au makanisa mengine yamezuiwa kumiliki ardhi? si yapo yamekazana tu kufufua wafu? badala ya kujenga shule na kununua ardhi?
 
Wait wait. Sisi wakatoliki tunaabudu sanamu na Maria? Sikujua hilo pamoja na kusoma seminary miaka 10
utajuaje wakati ufahamu wako umefungwa? nakuombea kwa Mungu ufunguke kwa Jina la Yesu Kristo, na baada ya kufunguka ukawafungue na wenzako wote waliobaki huko, kuanzia muumini wa kawaida, kadinali hadi papa.
 
Kwani walokole ndo wanamuona Mungu? Nani alileta feedback toka huko kwa Mungu?
wamwabuduo halisi humwabudu Mungu katika Roho na Kweli, na hao ndio Mungu anaowatafuta. sio kuabudu kimwili hivyo. Mungu ni Roho.unaweza kumwona kiroho kama utaishi maisha ya kiroho sio ya kimwili.
 
Hongera kwa kuwa umekwishaokoka hapa duniani na hauna dhambi, hivyo utamwona Mungu!
ukiokoka sio kwamba hautakuwa na dhambi, maana yake umeingia mkataba na Mungu wa kumfuata kwa njia ya Yesu Kristo, ili nguvu za Mungu zikusaidie kushida dhambi na ukitenda dhambi bado unakuwa na mwombezi kwa Baba Yesu Kristo anayesimama kama wakili wetu. tunampokea wakili/advocate wetu kutuombea kwa Baba ambaye bila huyo hautamwona Mungu. wasiookoka hawana advocate hivyo wapo chini ya laaana na mauti kwasababu hawajampokea mkombozi wa maisha yao katika mioyo yao. hio ndio maana ya kuokoka. tunaposema muiokoke ni kwamba mumkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi, na muamini mioyoni mwenu kwamba Mungu alimfufua katika wafu na kwamba yeye pekee ndiye njia kweli na uzima wa milele. baada ya hapo mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye ndiye Mungu huyohuyo mwenyewe, ili akikaa ndani yenu muishi maisha ya kiroho ya kuongozwa naye.

maandiko yanasema "awaye yote asiyekuwa na huyo Roho wa Kristo, huyo sio wake", maana yake kama huna Roho Mtakatifu wewe sio mali ya Mungu, ni mali ya Shetani. na tunajua kama tunaye Roho pale tutakapomwona anajidhihirisha maishani mwetu physically, na ishara mojawapo ni kunena kwa lugha mpya au lugha ya malaika, pale anapokuwa anakusaidia kuomba kwasababu kwa akili zetu hatuwezi kuomba ipasavyo, ila Roho mwenyewe hulia kwa kuugua ndani yetu akisema "aba" yaani Baba, na huweza kupresent mambo ambayo kwa akili yetu tusingeweza. nyote mnaoomba kwa akili siku zote huomba kwa kufuata tamaa zenu za mwili tu, magari, nyumba, mke watoto n.k, wakati Roho anajua mnahitaji zaidi ya hivyo. Mungu akusaidie.
 
utajuaje wakati ufahamu wako umefungwa? nakuombea kwa Mungu ufunguke kwa Jina la Yesu Kristo, na baada ya kufunguka ukawafungue na wenzako wote waliobaki huko, kuanzia muumini wa kawaida, kadinali hadi papa.
Ndo akawaambia.nyie.ndo mtaenda.mbinguni?
 
Back
Top Bottom