Ipi siri ya "Google Search" Kuyapa kipaumbele kwenye mpangilio mambo ya kipuuzi kuliko yenye tija?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Katika matumizi ya kuperuzi mtandaoni!

Google kupitia uwanja wao wa kutaftia habari ujulikanao kama "Google search"

Ukitafta habari yoyote; Mambo ya kipuuzi ndiyo hutangulia kwanza kuonekana kwenye mtiririko kabla ya mambo yenye tija.

Mfano!

1. Ukitafta kujua kuhusu Nyota za angani ni nini, kitachotangulia hapo ni Nyota za mapenzi, Nyota za biashara, shekh sharifu majini na Nyota n.k baadae sana kwenye orodha ndipo utakuja upate Nyota za angani.

2. Ukitafta habari za RUTHU kwenye Bibilia, utaashanga wanakuletea kwanza Habari za Amba Ruty.

3. Ukitafta Nabii bora ni nani! Kwanza kabisa kabla hujamaliza kuliandika neno lenyewe tayari ya nabii Tito huyu hapa kwanza halafu wengine ndiyo wanafuata.

4. Ukitaka kujifunza vumbi na madhara ya Vumbi kabla hujamaliza wanakuletea Vumbi la Kongo na matakataka kibao.

5. Basi labda ukiona ujifunze mitindo ya kinyozi! Ukiandika tu namna ya kunyoa tayali unaletewa nywele za sehemu za siri na mambo kibao

Kiufupi Google imeyapa sana kipaumbele mambo ya kipuuzi kuliko yenye tija sijui kwanini
 
Ila afrika sijui tulilaaniwa nini.

Yani ukisechi neno african (mwafrika) kwa lugha ya kichina ukiingia kipengele cha images (picha) kiukweli tubadhalilishwa sana kuonekana maskini na mafukara

Hii ndio tafsiri ya mwafrika kwa kichina, copy hata maandishi usechi

非洲人
 
ila afrika sijui tulilaaniwa nini.

yani ukisechi neno african (mwafrika) kwa lugha ya kichina ukiingia kipengele cha images (picha) kiukweli tubadhalilishwa sana kuonekana maskini na mafukara

hii ndio tafsiri ya mwafrika kwa kichina, copy hata maandishi usechi

非洲人
Mbona nimegoogle sijaona cha ajabu au kwasababu ilikuwa Bing
 
Laumu jamii yako na sio gugo. Jamii yako ndio inapenda kutafuta mambo yasiyo ya msingi, yaani jamii yako inawaza upumbavu na kuutafuta huko gugo, nao gugo wanasevu huo upumbavu akija mwingine nae akitafuta kitu cha maana gugu wanampa sajesheni za yale yanayotafutwa(ambao ni upumbavu wa walio wengi)
 
Google wanakupa kulingana na wewe mwenyewe ulivyo wahi search huko nyuma
Na watu wa eneo lako wanacho search...

Kama ni Tanzania ,Daresalaam..Mtu maarufu ni Amber Rutty ..uki search Amber lazima aje Amber Rutty..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom