Elections 2010 Ipi Sahihi: Rais/Mbunge Mteule au mchaguliwa?

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Naoma ufafanuzi wa kutumia neno mteule hasa kwenye chaguzi zetu. Sasa hivi tuna Rais mteule and wabunge wateule. Kwa nini waitwe wateule badala ya wachaguliwa? Kwani wapiga kura waliwateuwa au waliwachagua? Kwa waingereza: A president-elect is a political candidate who has been elected president but who has not yet been sworn in, or officially taken office. Wao wanatumia neno elect ambapo tafsiri yake inaweza kuwa mchaguliwa.

Kuna mdau ametoa maoni sehemu nyingine kwamba "Mteule ni yule anayeteuliwa na mtu au rais kwa ridhaa yake binafsi, lakini anayechaguliwa na wananchi ni Rais, mbunge au diwani mchaguliwa." Mdau mwingine akamjibu kwamba: "Hilo la mtu aliyechaguliwa kwa KURA kuitwa mteule ni sahihi kwa mjibu wa BAKITA. Mbunge mteule = MP elect (in english), rais mteule = President elect (in english). Neno hilo halina tatizo."
 
Mbona jibu liko wazi, uitaji kufikiria. Asilimia kubwa ya wagombe waliotangazwa na tume kwamba wameshinda ni WATEULE sababu wameteuliwa na tume(UCHAKACHUAJI).
 
Back
Top Bottom