Ipi pikipiki imara na madhubuti kati ya Boxer 150 na TVS HLX 150?

Kiboko yao platina iko vizuri zaidi kuliko zote watu waznazikimbia Kwa kuwa zinauzwa bei kubwa na vipuri vyake bei Juu ila ukifunga unasahau,Lita moja 70km
Sio kama boxer BM 150 mkuu, boxer IPO simple sana mlio umetulia, pili tafuta mtu mwenye boxer BM 150 ya miezi 4 af angalia na tvs 150 miezi 4 utagundua kitu. Bt TVS 125 ni nzuri sana Inahimili shida na raha huo ndo uzoefu wangu mkuu
 
Mkuu Wick vipi kuhusu spare za TVS, maana nina hlx 150 nilimpa dogo akamwage oil naona wamenivunjia mfuniko,
Upo mkoa gani!?.. Unajua biashara inatofautiana bei kwa eneo!.
Halafu mfuniko upi wamevunja?, wa tank la mafuta, bampa au kale kastick sehemu ya kufungua kumwaga oil!?..
 
Kwa mtazamo wangu biashara ya boda boda ni biashara kichaa..unanunua chombo cha 2M unapata elfu 7 kwa siku bado kuna service na huduma zingine.

Nb:samahani kwa waliokereka ni mtazamo wangu tu
 
Huo ni mtazamo tu kila biashara ina changamoto Nissan civilian mil40 hesabu kwa siku laki 1 baada ya mwaka mil 36 bado service bado kupigwa bao wastan kwa mwaka unapata 25 mil kila biashara ina changamoto zake dogo au unaijua kuna biashara haina changamoto ni faida tu tuambie na ss.
 
Sio kama boxer BM 150 mkuu, boxer IPO simple sana mlio umetulia, pili tafuta mtu mwenye boxer BM 150 ya miezi 4 af angalia na tvs 150 miezi 4 utagundua kitu. Bt TVS 125 ni nzuri sana Inahimili shida na raha huo ndo uzoefu wangu mkuu
Tatizo la boxer mchina kashafyatua kopi...bado TVS hlx 150 is the best! Hapa sizungumzii ushabiki,boxer zilikua zile za mwanzo.
 
Anayo kuambia shemeji yangu hapo juu, ni nzuri 150 ina hadi sehemu ya kucharg sim,

Boxer ikishaanza kutoa moshi, ndiyo mwisho wa uhai wa hyo pikipiki

Tvs ni kama roho ya paka mweusi
Si kweli, pikipiki inatoa moshi inapoua Piston Rings hapo ni kufunga Rings tu unasahau kikubwa uzivushe service ya oil na kutumia oil bora kama Mogas, Total au Titan sio International Oryqs.
 
Nilitoka kijijini kwetu huko morogoro milimani nikiwa nimeijaza mafuta full tank pikipiki yangu ya TVS hlx 125cc nilipofika Ruvu nikasoma tofauti ya kilomita toka nilipojaza mafuta inasoma 438km , nikaingia kituo cha mafuta kujazia , zikaingia Lita 6 tu ikajaa full...yani hapo kitu imetuia wastani wa km 73 kwa Lita!! Kwa maisha ya sasa inafaa sana kibiashara hata kwa mizunguko mbalimbali kwa gharama ndogo ya mafuta.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom