Ipi ni sehemu muafaka ya kukutana na mume/mke

Kumekuwa na mijadala mingi ya kuwa ni sehemu gani hasa ambayo unaweza kukutana na mtu ambaye huenda akaja kuwa mke/mume. Katika mjadala huo kumekuwa na misemo mingi baadhi yake ikiwa;
Utakapokutana na mke wako ndipo mtakapoachania (kama ni baa then mtaachania baa)
Mke/Mume mwema hutoka kwa Mungu nk.

Katika mapinduzi ya teknolojia nayo yameibua njia nyingine mpya ya kukutana kwa watu na baadae kuanzisha mahusiano, MTANDAO. Njia hii imekuwa inasemwa sana kwamba mahusiano yake huwa hayaaminiki sana (Dhana hii imewekwa na wahusika wenyewe) Hivyo kusababisha mahusiano mengi yanayoanzishwa na njia hii kuwa ya muda mfupi or "oneoff"

Sasa hebu tuambizane kidogo kwa mitizamo yetu ni wapi hasa au njia ipi ukikutana na mtu huko then anaweza kuwa mume/mke mwema.....


hapo inategemea na wewe upoje na huyo partner wako yukoje, yaani kifani zaidi, kama ni mpenda disco mtakutana disco, kama ni mlevi mtakutana baa, kama ni cha Mungu mtakutana kanisani/msikitini.
 
Hi JF members,

Sehemu nzuri ya kukutana na mke/mume ni popote pale. Mke/Mume anatoka kwa Mungu. Hivyo kwa kuwa suala la mke/mume ni mpango wa mwenyezi MUNGU, Mungu anaweza kuwakutanisha popte pale mfano katika Bustani!
 
Hi JF members,

Sehemu nzuri ya kukutana na mke/mume ni popote pale. Mke/Mume anatoka kwa Mungu. Hivyo kwa kuwa suala la mke/mume ni mpango wa mwenyezi MUNGU, Mungu anaweza kuwakutanisha popte pale mfano katika Bustani!
Mh wengine tunaishi maeneo yasiyo na bustani zaidi ya zile zilizoko majumbani kwetu, sasa hapo inakuwaje?
 
Back
Top Bottom