Ipi ni nafasi ya siasa katika maendeleo ya nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ipi ni nafasi ya siasa katika maendeleo ya nchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Exaud J. Makyao, Apr 30, 2009.

 1. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi najiuliza umuhimu wa siasa lakini bado sijapata jibu.
  Tena nahitaji msaada wa kujulishwa kama siasa ni lazima katika kuendesha nchi.
  Naona siasa kama porojo zinazopingana na utaalamu.
  Maamuzi ya kisiasa yamejaa jazba,hisia na mitazamo ya watu.
  Siasa haijali taaluma bali hukumbatia itikadi.
  Ipi ni nafasi ya siasa kwa maendeleo ya nchi?
   
 2. j

  jrm Member

  #2
  May 1, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hapo nami umenikuna, maana nilikuwa na najiuliza swali hili hili! Nadhani twaweza endelea bila mbunge lakini mwalimu asipoingia darasani kufundisha kwa siku ni hasara kubwa sana kwa nchi. Acha waganga na manesi wasiingie hospitalini itakuwaje kwa wagonjwa? Lakini cha ajabu mbunge alipwa hela kibao wataalamu wanalipwa kiduchu! Ndo maana wataalamu nao wanakimbilia kwenye siasa na kuacha fani zao. Najiuliza Tanzania kwa baadae tutakuwa wapi? Viongozi wanakazana eti wanfunzi someni masomo ya sayansi. Yanini kutesa kichwa unasoma sayansi halafu mwishoni mtu wa sanaa ndie atakula kuku kwa mrija!?
  Natabiri huko twendako tutafika mahali kuomba wataalamu watoke nje kuhudumia nchi wakati wazawa tunakimbilia masomo ya sanaa ili twende kwenye siasa. MASIKITIKO MAKUBWA...
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii mada umelenga kwenyewe haswaa..

  Tangia nipate umri wa kuanza kutafakari bado sijapata bado sababu ya msingi ya hiki kitu kinachoitwa siasa na application yake. Pengine tatizo letu ni suala zima la kuiga kila kitu tunachokisikia wenzetu wakikifanya. Wkaianzisha wimbo fulani sisi kazi yetu kuitikia kiitikio na hadi kupitiliza kabisa.

  Kwa mtazamo wangu mimi nadhani tunahitaji nchi iongozwe na jopo la wataalamu mbalimbali ambao wataweza kumonitor progress kwa kutumia taalauma zao. Mfano wachumi wanakaa pamoja na watu wa afya, miundo mbinu, michezo etc..yaani mambo yangekuwa mswano.
   
 4. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Makyao,

  Siasa ni utaratibu wa kugawa madaraka katika jamii. Siasa ipo kuanzia ngazi ya familia, ngazi ya mtaa, shuleni, kazini na mpaka ngazi ya taifa. Watu wengi wanapozungumzia siasa huwa wanaona siasa ya ngazi za kitaifa tu ambapo kuna vyama vinavyogombea kutawala taifa.

  Lakini ukienda hata darasani kulikuwa na uchaguzi wa monitor, high skul kulikuwa na uchaguzi wa kaka/dada mkuu, kanisani mtachagua mweka hazina, kwenye kikao cha harusi mtachagua mwenyekiti, katibu, mweka hazina, etc.

  Hiyo yote ni siasa.

  Sasa hebu fikiria tena kisha tuambie kama siasa haina umuhimu katika maendeleo.

  Siku njema
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Siasa ni kila kitu mpaka mambo ya kikubwa ni siasa.Angalia wanawake wa Kenya wameamua kutumia mkakati gani kushinikiza wanasiasa wabadilike ili wawe na utawala bora.
   
 6. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena mkuu
   
 7. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MILLIONAIRE,
  Kwa nini unaita utaratibu wa kugawa madaraka katika jamii ndiyo siasa?
  Unamaana hata tukitaka kumpata DAKTARI MKUU WA UPASUAJI katika hosipitali fulani tupige kura kama kumpata monitor wa darasa?
   
 8. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Utaratibu unaweza kuwa tofauti - kwamba kura si ya wazi sana kama kwenye siasa za kidemokrasia - lakini siasa iko pale pale.

  Sina uzoefu na sekta ya utabibu lakini mfano kwenye makampuni ukitaka kupanda ngazi uwe mkuu wa idara au kuwa managing director kabisa usijidanganye eti elimu yako au utendaji wako makini ndio utakupa cheo hicho.

  Ni lazima upige kampeni za chini chini (ambayo ndio siasa yenyewe) ili wanaofanya uchaguzi au uteuzi wakupe hicho cheo.

  Bila siasa, kwa mfano, kwenye private sector utaishia kuwa junior staff tu. Kwenye public sector nasikia sera ni umri kwa hiyo ukiwa mfanyakazi wa siku nyingi zaidi ndio unapewa madaraka.

  Kujibu swali lako la msingi - nini nafasi ya siasa kwenye maendeleo ya nchi? - labda kuliweka sawa zaidi swali ni nini nafasi ya siasa kwenye maendeleo ya jamii maana katika kila ngazi ya jamii kuna siasa.

  Maadam siasa ndio inagawa madaraka jiulize ni nini nafasi ya viongozi kwenye maendeleo ya jamii. Viongozi wanatoa muongozo (vision) na kusimamia utekelezaji. Kwa hiyo kiongozi anayefaa ni yule unayeona ana muongozi sahihi kwa jamii yako - na hapo ndio nafasi ya siasa ilipo katika maendeleo ya jamii.

   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Siasa kama siasa ni nzuri sana. Tena ni somo ambalo kila mtanzania na mwanajamii yeyote anapaswa kutumia muda wake kulifanyia kazi.
  Shida haipo kwenye siasa wanandugu, bali kwa WANASIASA(Politicians). Hawa watu wanaacha maagizo ya taaluma ya siasa, na kugeukia ubinafsi wao, wakilenga kupata faida na ziada kutokana na nafasi walizo nazo.
  Lakini , labda pia nikwambie bwana Makyao kwamba, Siasa pia ni Sayansi! Utasema huyu jamaa vipi!! Ndiyo! Ni Sayansi! Ni sayansi inayohusu au kushughulika na UPATAJI NA UTUMIZI wa MADARAKA.
  Katika Tanganyika yetu, kama Upataji huo na Utumiaji wa Madaraka ungekuwa katika hali ya unyoofu, hakuna mtu ambaye angelia na hilo. Hicho choote kilichoandikwa tangu mwanzo wa mada hii, na hata kikakusababisha wewe ndugu kuhoji uhalali wa uwepo wa SIASA, ni utumizi wake mbovu. Kwa Tanzania yetu, jiuluze maswali yafuatayo:
  1.Je Raisi wetu alipatikana katika misingi ya haki kabisa?
  2.Je anatumia madaraka inavyopaswa? anateua viongozi kwa kufuata taaluma zao au urafiki?
  3.Anasimamia vizuri keki ya taifa?-hakuna wanaopunjwa na kulalama?
  4.Je anadhibu pale anapoona kiongozi amtenda kinyume na kiapo chake, au anamhamisha wizara au idara/
  Kuna MASWALI mengine mengi unayoweza kuhoji ili kujua kama nchi yako inaenda katika unyoofu, kulingana na katiba ya nchi.

  Hapo nilitaka nikuonyeshe tu Bwn. Makyao na wengine kibao mliosupport kuwa SIASA haina uhalali wa kuwepo. Ni kwamba inahitajika, ili mradi tu iwe safi, kam ambavyo Julius Nyerere alisema.
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Bwana Makyao na wengine; je mpaka hapa mnadhani siasa ni nini? kama mkijua siasa ni nini na kutwambia siasa ni nini hasa, hapa ndipo tuanze kujadili mada hii vizuri.
  Yupo rafiki yangu mmoja siku moja mwaka 1995 nilimtonya kuwa nataka kuingia kwenye siasa za nchi hii, na alinipa tahadhali kubwa sana na nilipomuuliza kwa nini hapendi nijiunge na siasa aliniambia hivi, "No politician will reach/see heaven".
  Je sasa siasa ni nini? je is it devil? Naomba mnisaidie nielewe hii siasa ni nini hasa? May be inaweza kuwa na maana au isiwe na maana, lakini mpaka tujue siasa ni nini?
   
 11. j

  jrm Member

  #11
  May 1, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa kwa ligha ya kigeni ni "Polytics" na ni kilatini ikiwa ni muunganisho wa maneno mawili, poly and tics. Poly maana yake ni wingi na tics ni wadudu wanaofyonza damu ya wanyama kama ng'mbe.
  Hivyo kama "Mchukia Fisadi" alovyotahadharishwa kuwa akiingia kwnye siasa hataiona mbingu ndo hii. Wanasiasa wanatunyonya kama kupe tena wengi.
  Kama wengine walivyosema siasa ikitumika vizuri ni nzuri na ni muhimu, lakini kwa hapa Tanzania imekuwa ni balaa. maana imechukua nafasi kubwa kuliko utaalamu
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huwezi kujibu swali hili vizuri mpaka ujibu swali la "Siasa ni nini?"

  Ukimsoma Karl Marx katika "Das Kapital" utaona sehemu ya siasa inafungamana na uchumi.

  Ukimsoma Dale Carnegie katika "How To Win Friends and Influence People" utaona sehemu ya siasa ni mahusiano ya jamii.

  Ukisoma Biblia utaona sehemu ya siasa inafungamana na dini.

  Ukisoma "The Art of War" cha Sun Tzu utaona sehemu ya siasa ni mbinu za vita.

  Ukisoma "The Prince" cha Machiavelli utaona sehemu ya siasa ni hadaa.

  Ukisoma "Don Quixote" cha Miguel Cervantes na "Azimio la Arusha" utaona sehemu ya siasa ni kuamini visivyoaminika (idealism)

  Ukisoma .... ah,

  Siasa inaingia katika kila nyanja ya maisha, ukitaka kwenda sinema unapolipia serikali inakukata kodi kulingana na asilimia ya kodi iliyowekwa, siasa ishakuingilia hapo.

  Ukitaka kuoa, inabidi uoe kidini au kiserikali na upate kutambulika kiserikali, siasa zishakuingilia hapo.

  Hata ukisema uende kuishi msituni kama Thoreau katika "Walden" kesho keshokutwa serikali ikipata muwekezaji anataka pori hilo, serikali hii inaweza kutumia sheria za "eminent domain" kukuondoa, kwa sababu ardhi yote ni ya serikali na mwananchi hata kama ana hati anakodishwa tu.

  Hakuna jambo linaloenda bila siasa, wakomunisti wa kweli walivyompindua Tsar Nicholas II walitaka kujenga jumuiya ya ma-soviet isiyokuwa na serikali wala siasa, wameshindwa, mwishowe wametoa mfumo uliokuwa na siasa kuliko mfumo mwingine wowote.

  Unless unataka anarchy, siasa ni lazima, kwani hata katika familia kuna siasa na protokali za kufanya mambo.
   
 13. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MCHUKIA FISADI,
  Msaada unaohitaji ndo wengi tunauhitaji pia.
  Katika uwanja wa hiyo siasa, watu wameuawa, watu wamewekwa kizuizini, wasio na utaalamu wamepewa nyadhifa kubwa za kitaalamu, n.k

  Kwamba ni shetani sijui.

  Bado ninahaja ya kujua kuwa dhana hii "siasa", ni nini umuhimu wake hasa?
   
 14. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Makyao,

  Ungetoa mifano basi ni kina nani hao ambao unasema hawana utaalam lakini wamepewa nafasi za kitaalam.

  Kikubwa ni kwamba usichanganye nafasi za uongozi (menejimenti) na zile za kitaalam. Mfano mtu ambaye hajasomea udaktari anaweza kabisa kufanya kazi ya kumeneji madaktari. Mtu ambaye si wakili anaweza kabisa kuwaongoza vizuri tu mawakili, etc.

  Na kama alivyosema raisi wetu ni kwamba uraisi hausomewi ndani ya chumba cha kuta nne chini ya mwalimu fulani ... hivyo usishangae ukikuta wenye madaraka katika ngazi tofauti kwenye jamii "hawajasomea".
   
  Last edited: May 3, 2009
 15. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Someni kisa hiki ..ndipo mtajua siasa ni nini:
  little John goes to his dad and asks, "What is politics?" Dad
  says, "Well son, let me try to explain it this way. I'm the
  breadwinner of the family, so let's call me Capitalist/Entrepreneur/Taxpayer. Mommy is the administrator of the money, so we'll call her the
  Government. We're here to take care of your needs, so we'll call you The People. The nanny, well, consider her The Working Class. Your baby brother, we'll call him The Future. Now go think about
  this and see if it makes sense."

  So the little boy goes off to bed thinking about what Dad has
  said. Later that night, he hears his baby brother crying and
  runs to his room only to find that his diapers are very soiled.
  So the little boy goes to his parents' room. Mom is sound
  asleep. Not wanting to wake her, he goes to the nanny's room.
  Finding the door locked, he looks through the peephole and sees his father in bed with the nanny. He gives up and goes back to bed.

  The next morning, the little boy says to his father, "Dad, I
  think I understand what politics is now."

  "Good son, tell me in your own words then what politics are."

  The little boy replies, "Well, while Capitalist is screwing the
  Working Class, the Government is sound asleep, the People are
  being ignored and the Future is in deep shit."
   
 17. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  WomenofSubstanc
  You've decided to confuse me totally.
  Come up with open answer.
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  :):D
  Good answer dear. Je hii ndio maana ya siasa hasa? hukueleza zaidi ingawa nimeelewa jibu la yule mtoto kwa baba! Nauliza hii ndiyo siasa?
   
 19. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wana - JF
  Naona inakuwa ngumu kupata ufumbuzi kuhusu siasa.
  Wanasiasa mko wapi?
   
 20. H

  Haika JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  NAOMBA KUTOA HOJA,
  Nimevumilia nimeshindwa, baada ya kuona kuwa hata watu niliokuwa nawaamini hapa JF wameingia mkumbo.

  Watanzania wenzangu, tusiwafaidishe hawa mafisadi kwa kuposti habari za kuwatetea au kuwaponda kwa stori za mtaani.
  Nimenote kwamba kila stori ya ufisadi siku hizi inazidi kupungua 'objectivity' yake, inakuwa kama vile huyo mwandishi ana personal agenda either ya kutetea au kuangamiza.
  Hawa jamaa tukubali waliamka mapema ndio tulikuwa tumelala wakaiba mali yetu, hivyo ni more in touch na hali ilivyo kuliko sie, (at least kwa wakati ule) They are not dumb people, hatuwezi kuwatishia nyau!!

  1. Kwa kuwa wanajua kuwa kila habari imejichanganya ukweli na uongo, kwa hiyo hawana haja ya kubabaika, wanajua hakuna mashtaka.
  2. Kwa kila tunayemsema humu, tunamkweza adui yake, tunauficha ukweli wa wizi wenyewe.
  3. Kwa kila ukabila tunauousema humu, tunaelekea kwingine, yani mafisadi ambao sio wa hayo makundi wanaendelea kuiba tuuuu

  Wote tunajua kuwa fedha zetu nyingi sana zimepotelea kwa hawa mafisadi, waliotajwa na ambao bado hawajatajwa,
  Mimi binafsi niliupenda mtindo wa mashtaka ya EPA ambao, jumla ya fedha za wizi zilikuwa traced mpaka wakakamatwa waliokamatwa, kakuna umbea wala nini. wengine wahindi, wengine wachaga, wengine nk.

  Kama inawezekana mabishano hapa ya ku-trace fedha zilikoenda, sio sura zilikoenda.

  si ajabu wengine wetu humu ndani japo hawavumi lakini wapo!!

  mfano:
  Ubinafsishaji wa ................(kampuni yoyote) ulikwendaje?
  Tuanze na kampuni kubwa kubwa na maarufu, kwa mfano mzuri kwa sasa ni haya
  makampuni (YOTE) ya simu za mkononi, na
  TTCL,
  makampuni ya vinywaji,
  Utilities kama umeme na maji,
  Makampuni ya madini,
  makampuni ya imports na exports.

  Watanzania wenzangu, tusiyumbishwe na baadhi ya watanzania humu wenye kupenda kupoteza uelekeo wa mada

  Mada kuu ni uwajibikaji katika kutumia rasilimali zetu
  Zazima wote wawajibishwe.

  Inauma sana pale unapokuta kuwa hawa wachache tu maarufu ndio wameshikiwa bango, wengine huko wanaendelea kuzoa kwa kwenda mbele!!

  Hebu tuamke,
  Kama VODA, ZAIN, ZANTEL, TIGO zilianzishwa kinyume basi wote wawajibishwe,
  I HATE HATE POLITICS, THEY ARE CHEAP
   
Loading...