Ipi ni Golden Generation kwa Koffi Olomide?

Roga Roga

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
656
483
Kama mnavyojua tena Koffi Olomide akiwa na kundi lake la Quarter Latin amefanikiwa kutoa album nyingi na nzuri, leo nataka tujue kizazi kipi kwa kofi kilikuwa bora na kilimng'arisha sana kofi.

I. Kizazi cha Miaka ya 90, (1993 - 1999)
Hiki ni kizazi kilichoundwa na wa kali kama Suzuki Luzubu 4 x 4, Sam Tshintu, Babia Ndonga shokoro, Willy Bula, Erick Tutsi, Geco Bourro Mpela ,Mamale Tupac, Pathy Bass, Sunda Bass, Modogo Balongana , mboshi Lipassa, Lebou Kabuya,Nseka Passe-Kossey na walifanikiwa kutoa album moto sana kama Loi , Magie, Ultimatum, V12 (andrada), Koweit Rive gauche, Noblesse oblige, n.k

II. Kizazi cha miaka ya 2000 (2000 - Sasa)
Hiki ni kizazi cha kina Fally Ipupa, Fere Gola, Titna El capone, Montana Kamenga, Jordani Kusa, Brice Malonga , Apocalypse Cendre , Bébé Kerozene, Mboshi Lipassa, Mukusa Ya Mbwa , CNN Alligator,Cindy Le Coeur ,Shella Mputu ,Suzuki Luzubu,Geco Bourro Mpela, Roi-Soleil Wanga ,Gipson Butukondolo, Brigade sabath Rwinga, n.k
Hawa nao wametoa album kama Monde Arabe, Efflakata, Danger de morte, Affaire D Etat, Force De Frappe n.k

Baadhi wameshiriki generation zote mbili, lakini hapa tunaangalia ubora wa kazi zao katika quarter latin na sio kama solo artist.

Kiukweli kabisa hiyo ya 1990-2000 ni generation iliyokuwa kali sana, Willy Bula kaka yake Blaise bulla, Gecko mpela kaka yake Alain Mpela, Babia ndonga, Sam Tsintu, Popolipo, Suzuki, Madogo Abarambwa ............Anga ma ma ma kolela ah (Maneno ya kwenye Magie) huku wimbo bora ni Amein....Ndugu sins cha kuzungumzia kizazi hiki.
 
Nasikia wameungana tena huko Paris.
 
Hiyo ya 90 ilikuwa moto sana mimi album ya ultimatum ilikuwa inamaliza mambo.vibao kama miss nicole ulikuwa unapata burdan kusikiliza na kuangalia wale wanenguaji haya roga roga ahsante
 
Nimesikia wameungana mkuu..na wana onyesho tarehe nimeisahau..
Kuna wakati hawa waliotamba 1990-2000 walijitoa kwa kofi na kuanzisha Quarter latin academia lakini baada ya muda wakaanza kurudi kwa mopao, japo Sam Tshintu ndiye mpaka leo hajawahi kurudi. Waliorudi Gecko Bouro mpela, Madogo Abarambwa n.k
 
Walikuwa wakirudi kweli, ila koffi aliwachezesha kanyaboya bila wao kujua yaani kama huyo mpela mpaka demu wake inasemekana kaliwa na mopao
 
New Generation kuanzia 2001 ndio bora ikichagizwa na Atalaku bora kabisa kina CNN Alligator, Brigadier Sarbati, Apocalypse na Baby Kerozene.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom