Nondoh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 298
- 478
Hi
Nini mtazamo wenu nafasi kwa watanzania UN?
Leo kaapishwa katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ni matarajio atakuja na timu mpya ya uongozi kama ilivyo kawaida kwa katibu mkuu mpya anapochukua uongozi.
Ikumbukwe kuwa katibu mkuu anayemaliza muda wake Ban Ki Moon alipoteuliwa alikuwa na safu yake mpya ya uongozi akiwemo mtanzania Dr Asha Rose Migiro. Miongoni mwa wateule wachache sana ambao waliiashia awamu ya kwanza Dr alikuwemo. Taarifa ya kiofisi ilidai kuwa kamaliza muda wake lakini wachambuzi wanadai ilitumika tafsida ukweli wa mambo ni kuwa uwezo ulikuwa mdogo na alishindwa kuendana na Kasi ya Ban Ki Moon hiyo ikaamliwa kibarua kisitishwe aletwe mtu mwenye upeo mkubwa
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi hasa nafasi ya mtanzania UN hasa baada ya utendaji wa Dr. Asha. Najiuliza hivi ni kweli legacy aliyoiacha ni chafu kiasi kwamba inaleta walakini kwa mtanzania kuteuliwa tena UN. Najiuliza tena kama ni kweli na ukizingatia kashfa ya wasomi vihiyo, kufoji vyeti kulikokithiri, watumishi hewa maofisini yote haya UN wanayajua, hivi kweli kuna mtz ataaminiwa tena UN. Inaweza kuwa kweli alimaliza muda wake na legacy aliyoacha UN ni ya kuigwa lakini maswali mengi yanaongezeka kwa uwezo wa hawa wasomi wa Tz na hizi doctorate zao hasa pale ninapomfikiria Professor wa kitanzani analala ofisini aking'ang'ania uenyekiti wa chama badala ya kulala kwenye research au doctor analia huku akitubu hadharani baada ya kutemeshwa ukuu wa mkoa... Najiuliza sipati jibu.
Great thinkers mnakaribishwa...