Ipi kauli moja ya watanzania ya unyama wa serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ipi kauli moja ya watanzania ya unyama wa serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjomba wa taifa, Sep 6, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha panapotokea mauaji ya kinyama kwa raia mwenye fani fulani kuona ni jumuiya ya wanafani hiyo tu ndiyo inabebeshwa msiba wa kifo hicho. Utamaduni huu ni mpya kwa jamii ya Kitanzania ambayo tumeishi kwa upendo kwa muda mrefu kabla na hata baada ya Uhuru.

  Inasikitisha kuona Mwandishi wa habari anauawa kinyama na suala hili wanaachiwa waandishi wa habari (wa Iringa) kususia kutoa habari za jeshi la Polisi. Nimesema wa Iringa kwa sababu sijasikia kama wanahabari nchi nzima wamesusia habari za Polisi.

  Hivi karibuni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dr Steven Ulimboka alipigwa na kuachwa nusu mauti na watu wanaodhaniwa ni askari, matokeo yake wananchi walitega masikio kusikia Madaktari wataoa tamko gani. Je watagoma kuwatibu askari?

  Wiki iliyopita kijana muuza magazeti aliuawa na askari polisi pasipokuwa na hatia masikini ya Mungu, bahati mbaya hakuna umoja wa wauza magazeti nchini, ndio maana hakukuwa na mashinikizo ya kususia kuuza magazeti na msiba huo umekwisha masikioni mwa wanatanzania.

  Kwa matukio haya mfululizo ya mauaji hatuoni sasa ni busara kwa watanzania kuona msiba wa mwenzako ni wako pia? Kwanini wananchi wote bila kujali fani zetu tutoe sauti zetu hata kama ni kukutana viwanjani kupinga kwa kauli moja matukio haya! Nadhani watekelezaji wa mauaji haya wamekuwa na kiburi kutokana na kukosekana kwa umoja baina yetu.

  Tukumbuke kuwa kukosekana kwa umoja baina yetu ndiyo chanzo cha kunyanyaswa makazini, kuongozwa kihuni, kuibiwa rasilimali zetu, kubezwa na watawala, kupandishiwa bei za mahitaji kila kukicha N.K.
   
 2. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Unataka umoja gani zaidi ya matamko yanayotolewa kila siku na viongozi au wanaharakati kulaani hicho kifo. Au unataka kila mtu aende maredioni au kwenye TV kutoa maoni yake? Watu wengine bwana.
   
 3. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sio kosa lako, hutofautishi JF na blog zingine za udaku.
   
Loading...