Ipi inafaa.? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ipi inafaa.?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kobe, Aug 13, 2009.

 1. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  HELLO JF, mi nimetatizika na hili jambo la ndoa kati ya kimila na serikali hivyo ningependeza kujua maana kwa faida na hasara zipatikanazo katika ndoa hizi ili niwe makini nisije kutengeneza bomu la ndoa manake mi bado bachela.! wenye kujua tafadhali mniweke wazi.
   
 2. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Njoo kwa YESU kuna majibu yote ya matatizo ya wanadamu ikiwemo tiba ya ndoa. Utapata mwenzi atokaye kwa MUNGU, nawe utaifurahia ndoa yako. Karibu.
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  KWa mtazamo wangu kwa maisha ya duniani zote ni sawa kuonyesha watu kuwa umefunga noda.
  Lakini kwa Mungu nyie bado ni wazinifu hamjafunga ndoa takatifu, Mungu hajawaungannisha bado mmeunganishwa na mila na serikali.
   
 4. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Nina mashaka na mtazamo wako, vipi kuhusu wasio na dini? wote watakwenda Jehanamu kwa kuwa tu walifunga ndoa kimila/kiserikali? Vipi kuhusu mababu zetu ambao waliishi kabla hizi dini hazijaletwa kwetu na Wazungu na waarabu? nao walifanya uzinifu?
   
 5. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  na ndio kitu kinachonitatiza sana,manake walikufa kabla ya hizo dini kuwafikia je kwa kuwa hawakuungama hapo kabla,watahukumiwa kwa sheria gani na bwana Mungu.????
   
 6. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Kwa kawaida kijana wa kike na wa kiume wanapofuata taratibu za kuoana ( yaani ikiwemo kupata ridhaa ya wazazi wa pande zote mbili na bila kufanya uasherati) tayari hiyo ni ndoa kamili mbele za MUNGU hata kwa wapagani.

  Ila walio katika BWANA yawapasa waoane katika BWANA tu na ndoa zao zifungwe kanisani nafikiri hapa ndo kwenye pointi ya dada Joyceline. Kinyume na hapo ni dhambi mbele za MUNGU.

  Na issue ya kwenda Jehanamu kwa wapagani (wasiokuwa na dini) si katika suala la ndoa bali ni kwasababu wamemkataa YESU kuwa BWANA na Mwokozi wao.

  Na kwa wale waliokufa kabla ya YESU kuja watahukumiwa sawasawa na sheria zilizokuwepo wakati huo (Warumi 2 :12-16).

  Warumi 2:12-16

  12. Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa, wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria.

  13. Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.

  14. Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.

  15. Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;

  16. katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.
   
Loading...