Ipi bora zaidi kati ya Kitochi 4G Smart ya Tigo au Vodacom

Nakiwazia hichi kitochi ila bado sijapata info za kutosha kunishawishi
 
Wadau habari za majukumu, naomba kuuliza kwa wanaojua au ambao tayari wameshatumia simu hizi zinazopigiwa promo kwa sasa na makampuni ya Vodacom na Tigo maarufu kama Kitochi 4G Smart.

Napenda kujua ipi ni bora zaidi japo naona zinafanana ila tofauti kulingana na maelezo yao na battery capacity ya Vodacom ni 1400mAh na Tigo ni 1900mAh. Kama kuna zingine nijuzeni na ubora wake nataka ninunue. Asanteni.
Chukua ya TIGO mkuu, hotspot inafanya vyema kwenye macbook, pia battery life ni superb, bei yao pia rafiki sana ukilipia kwa tigopesa.
 
Nokia 3310 ni nzuri zaidi!
Hakika mkuu nami naisalute ninayo hapa..
IMG-20191219-WA0002.jpeg
IMG-20191219-WA0003.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nataka nikanunue cha voda , ila siko motivated na FACEBOOK,WHATSAPP NA INSTAGRAM. Nijuze je kuna uwezekano wa kuzi uninstall hzo system apps. ?
 
Hizi azumi l4k za voda line zote 2 zinasoma 4G ila lazima uweke voda kwenye slot no 1
Mimi yakwangu laini ya voda nikiunga bundle nikijihostpot kwenye simu nyingine naweza ku access social media tu siwezi kuingia google wala kudownload document whatsapp ila line 2 nafanya vyote sasa sijajua ni yangu tu au wew yako ipo vipi??
 
Back
Top Bottom