munirah
JF-Expert Member
- Mar 13, 2015
- 551
- 218
Wanajamvi habarini!
Nimelazimika kuuleta uzi huu hasa baada ya kuona blah blah za kisiasa zinavyozidi kuendelea hapa nchini ikiwemo upinzani kuusema vibaya utawala na jingine upinzani kuusema upinzani!
Katika mkutano wa ACT pale Mwembetogwa mjini Iringa ZZK ananukuliwa akisema kati ya wagombea wa urais kwa tiketi ya UKAWA na CCM hakuna anayetufaa kwa kuwa hawakuwa mstari wa mbele kupambana na rushwa na ufisadi kama Escrow Buzwagi Richmond nk!
Siasa inahadaa umma! Leo ZZK akiyasema haya huku akisahau kuwa chama chake kupitia kauli zake kimesema hakitasimamisha mgombea wa URAIS! ZZK anasahau alikuwa akimkaribisha ENL ajiunge na ACT ikiwa atakuwa tayari kuuanika utajiri wake! Haikuishia hapo ZZK alisikika akifanya imfluence katika audio kuwa vijana wa ACT waliopo ARUSHA waji organise na kumfata ENL na kumkaribisha chamani baada ya mh enl kukatwa Dodoma!
Bado sijaijua sera ya uzalendo wa wana ACT ambayo wao wenyewe hawajaisimamia kwa kuonyesha mfano halisi! Nionavyo mimi.....kitendo cha ENL kuwapa ACT mgongo na kitendo cha ACT kugomewa kujiunga na UKAWA imekuwa mwiba kwao sasa wanasahau kutoa sera zao na kuushambulia upinzani ambao hata hivyo hawatoa majibu!
ZZK nafahamu upo katika wakati wa mpito katika hatua za kuijenga ACT bora ambayo unataka kuwaaminisha watanzania kuwa viongozi wake watakuwa wazalendo hapo baadae! Kwakuwa bado ACT haijawa mpinzani au kwa kuwa bado ni chama kibichi kabisa......nadhani sasa mjipange katika kutoa elimu ya uzalendo kwa raia na pia mtambue kuwa wote mko katika boti moja na wanaUKAWA no matter what!
Unapotuambia wagombea hao hawafai leo hii wakati hauna alternative kutoka chama chako ni sawa na unatuhadaa wananchi! Nina imani kwamba ENL angejiunga na ACT kusingekuwepo kauli hizi za msimu!
Kupitia audio rec ZZK aliskika akisema yupo na mzee Mallah ambae ni mmoja wa madiwani aliyefukuzwa CDM kwa kashfa ya rushwa kule Arusha tena wakati zzk akiwa bado mwanachama hai wa cdm na inawezekana alichangia utimuliwaji huo wa madiwani hao! ACT imempokea Mallah na ZZK anatanabaisha kuwa wapo nae DAR wakiandaa mipango mikakati ya ACT.
Sasa nashindwa kuiona azma ya wana ACT katika kueneza uzalendo kwa kuwa watangazaji wa siasa za kung'ata na kupuliza! Hapo hapo zzk atamsema mgombea wa ccm na hapo hapo wa ukawa akisahau kuwa alikuwa tayari kumkaribisha!
Wazalendo pia wanataka mabadiliko lakini hawaeleweki wapo upande gani! Kauli za Prof KITILA ambaye ni ACT damu katika kipindi cha mwanzo wa ENL kuhama ccm zilipongezwa sana hasa baada ya kusema UKAWA wamesajili mshambuliaji hodari alipohojiwa BBC swahili lakini baadaye akaja kugeuka kuwa upinzani umefanya makosa makubwa kumchukua ENL katika video amesimama mbele ya vendor!
Nitumie rai hii kuwashauri wanasiasa wachunge sana kauli zao na wawe na maono ya mbele kuona kwamba kauli atakayoitoa leo inaweza ikachukuliwa kawaida lakin watu wa leo hawasahau tena! Wanaelewa sana na wanafatilia siasa kwa hamasa kubwa! ACT msiwe mpini wa kuua upinzani bali mjijenge kwa misingi ya uzalendo ambao mnataka kuuaminisha umma kwamba mnautetea! ZZK jitahidi kuzichanga karata zako upya ili mkiwa chama cha upinzani chenye ushawishi hapo baadae muweze kusimamia mlichokiamini!
AMANI IWE NANYI WANAJF WANA-ACT WANA-CCM NA WANA-UKAWA MASLAHI YA TAIFA MBELE ITIKADI BAADAE