iPhone 11 Pro: Haiandiki Hello

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,342
10,213
Leo katika pitapita zangu kwenye WhatsApp status nikakutana na video moja ikionyesha jinsi simu aina ya iPhone 11 Pro kutoka Apple, wenyewe wanaiita macho matatu ikiwaka kwenye OS ya Android. Sasa kwenye hiyo video zinasikika sauti za wadada wawili wakiwa wanaongea juu ya simu hiyo huku wakilalamika kwanini haileti neno Hello baada ya kuwaka, nilipoiona kwanza nilicheka sana nikajua tayari mchina ashaingiza bidhaa sokoni.

Nilichogundua ni kwamba mchina kaipiga design ileile ya bidhaa original kiasi kwamba huwezi kujua na ndani imepigwa Operating System ya Android ila sasa ili uingie kingi vizuri imepigwa Boot Animation ya Apple hapa nikakumbuka kipindi hicho niko O-Level nina Tecno P5+ yangu nilitaka kuweka Custom ROM ya Apple ikashindikana nikaipiga boot animation ya Apple nikawa najiona namiliki tunda kabisa.

Hawa wadada inaonyesha huu ni mzigo wa dukani maana inaonekana kila box wanalofungua mzigo ni huohuo na kinachoumiza lazima wameuziwa bei sawa na iPhone 11 Pro.

Inaonyesha hawa wadada hawana information vizuri maana wao ili kujua ni iPhone original walikaa kungojea iandike Hello, mchina mshenzi nyie ngoma ikaleta Android is starting.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MCHINA SIKU ZOTE NI BINGWA WA KU COPY NA KU PASTE, KUNA WATU WANAKUIMBIA MCHINA ETI ANA TECHNOLOGY KUBWA
 
niliiona pia ila sikuiangalia kwa makini
hicho ndicho kinanifanya nisite kununua simu zinazotangazwa Insta kuna Iphone 6 laki 4 ,iphone 7 laki 6 mpk 7

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
niliiona pia ila sikuiangalia kwa makini
hicho ndicho kinanifanya nisite kununua simu zinazotangazwa Insta kuna Iphone 6 laki 4 ,iphone 7 laki 6 mpk 7

Sent from my iPhone using JamiiForums
hapana wewe nunua tu,hao nao utasha wao wa kujifanya wa kishua sana kununua vitu wapi wapi sijui huko ndio wamejikuta wanalala stand mpaka saa mbili asubuhi.
 
Tatizo watanzania ni wavivu wa kitafuta taarifa juu ya kitu wanachotarajia kifanya.
Sasa hapo ukiwa dukan unachukua imei na uki search inakwambia kila kitu kuhusu device hyo lakin mtu anategemea cover ndio limwambie n aina gan ya simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo watanzania ni wavivu wa kitafuta taarifa juu ya kitu wanachotarajia kifanya.
Sasa hapo ukiwa dukan unachukua imei na uki search inakwambia kila kitu kuhusu device hyo lakin mtu anategemea cover ndio limwambie n aina gan ya simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
ugeni kwenye game ni tatizo.

sasa sijui wamelizwa wapi,yaani natamani niinunue kesi.
 
Aisee, hivi hiyo Hello" ndyo ishara pekee kwamba ni Original??, kwani hawakuzikagua before, masista duu wamepatikana🤭
 
niliiona pia ila sikuiangalia kwa makini
hicho ndicho kinanifanya nisite kununua simu zinazotangazwa Insta kuna Iphone 6 laki 4 ,iphone 7 laki 6 mpk 7

Sent from my iPhone using JamiiForums
Nunua tu kifaa original kinafaamika insta wapo wauzaji wa kweli tu . kwa bei hiyo ya 400k kwa iphone 6 ni sawa tu. Inategemea ni gb ngapi zinaanzia 16gb 32gb 64gb 128gb hapo ndo bei inaweza kupanda ila ina cheza hapo 400k au zaidi

Samsung galaxy note 3 snapdragon
 
Back
Top Bottom