Ipendeni na kuiheshimu mizimu yenu. Hamtafadhaika kamwe

Si yote bali yenye kiasili na wewe... Kuna baadhi ya tamaduni mizima ina nguvu sana.. Na ambayo haina kaliba nawe hupaswi kuidharau kwakuwa dharau yenyewe si jambo jema
Kwahiyo ni nini ukifanya ndio inatambulika kuwa unaheshimu mizimu? na tofauti ya nguvu kwa mizimu ina sababishwa na nini hadi iwe mizimu mengine ina nguvu kuzidi mengine?
 
Mi maisha yangu yapo fresh sana mkuu
Sina shida hata moja hata punje !
Labda mwanangu swalehe anapenda kula kula sana siku hizi
Sawa nashukuru kwa mara ya kwanza kusikia dunia hii kuwa kuna mtu hana shida hata moja ila bado sijajua nikirogwa nawezaje kujua maana mimi naweza kuwa na shida lakini nisijue kwamba shida hiuo ni kwa sababu ya kurogwa ama sivyo.
 
Hakuna kitu kama hicho. Yaani wewe mkuu nakuunga mkono kwenye BMW tuu huku kwingine big NO
Waliowahi kuikana, kuikataa ama kwenda nayo kinyume... Waliipata fresh.... Mizimu ipo na inaishi na ina nguvu... Don't mess with them
 
hahaha..
wiki nne mbona nyingi,ita press conference,,ukisema Mimi Baba Swalehe natangaza kugombea uraisi wa tanzan....
kabla hujamaliza kusema tanzania mara paap unajikuta upo naliendere unapalilia mashamba huko......
Hahahaha 😅😅😅

Mbona membe wameshindwa
 
Kwahiyo ni nini ukifanya ndio inatambulika kuwa unaheshimu mizimu? na tofauti ya nguvu kwa mizimu ina sababishwa na nini hadi iwe mizimu mengine ina nguvu kuzidi mengine?
Makafara ya kifamilia ndio huifisha ama kuipa nguvu
 
Nini maoni ya Kiranga kuhusu mawaidha haya?
Kwanza kabisa, kabla ya kujadili sana, ningependa kuelewa definitions, ili nijadili kitu ninachokielewa.

Mtu anaposema "mizimu" ana maana gani? Ana muktadha gani?

Ana maana ya kitu cha kweli? Kama anasema mizimu ni kitu cha kweli, ana ushahidi gani?

Au anasema katika muktadha wa ngano na mapokeo ya jamii tu?

Kama ana muktadha wa ngano na mapokeo ya jamii tu, habari za mizimu zina tofauti gani na dini nyingine kiasi kwamba mimi niliyekosoa dini nyingine nikubali habari za mizimu?

Mimi sijakosoa Uislamu na Ukristo kwa sababu ni dini za kigeni. Nimekosoa kwa sababu habari zilizomo ndani yake hazina logical consistency.

Sasa nitakuwa mbaguzi wa rangi au kiutamaduni, na kaburu wa kitabia, kama nitakataa dini z auongo za watu wageni, halafu nikakubali dini za uongo za watu wetu.

Haya ni mambo machache ya kufikiri, katika muhtasari unaoelekea kujadili habari hizi.
 
Hao ni wao mkuu, kila mtu ana utashi wake kwa swala la kufika mbali binadamu wote tunaishia hapa hapa. Ukibahatika utafika miaka 70, baada ya hapo ni mavumbini. Kwenye hukumu ya siku ya mwisho ndo utaeleza kwamba ulishirikiana na majini ili uweze kufika mbali, teh..!
Mkuu acha nikuulize swali... Kusengenya, kuchukia mtu, ulevi, uzinzi, uchoyo vyote hivyo vinaweza kumfanya mtu asiende Mbinguni hiyo ni kwa mujibu wa Biblia, (sijajua imani yako) na kama ni MuIslamu kuna tabia zitakuksesha Pepo.

Haya, tunakuja hapa... Mkristo anasema wrote wasiomwamini Yesu hawaendi Mbinguni jumlisha na wale wanaoenda Makanisani lakini wanatenda dhambi.

Je, ni watu kiasi gani wataenda motoni kama ukifanya uchambuzi?

Haya, na Muislamu nae ana madai yake...

Haya mambo ni magumu sana Mkuu.

Yule jamaa pale msalabani alikuwa jambazi maisha yake yote lakini tunaambiwa kabla hajafa alipata tiketi ya mbinguni.

Hili tena... Yesu anasema wote walio wake hawatapotea hata mmoja, Je, unaelewa nini hapo?
 
Ndugu zangu tuachane na habari za mizimu .tumuamini mwenyezi mungu mmoja .yeye mwenye uweza juu ya kila kitu ametuumba sisi na akatengenezea mambo yetu .so tusimshirikishe na chochote ikiwa sisi tunaakili ya sawa sawa
 
Back
Top Bottom