Invitation Letter: help please! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Invitation Letter: help please!

Discussion in 'Matangazo madogo' started by The Spit, Mar 11, 2009.

 1. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  nina rafiki yangu dar es salaam ambaye anatafuta passport kwa vile anategemea kunitembelea mwezi wa saba huku nilipo nje ya bongo,sasa kule uhamiaji anatakiwa aambatanishe barua ya mwaliko,naomba mwenye idea na jinsi ya kudraft barua kama hiyo na mambo ya muhimu ya kuandika au kama kuna mtu ana copy ya barua ya aina hiyo anisaidie!

  thanks alot!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 11, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ingia google halafu type "letter of invitation" au "invitation letters"
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Anwani yako ulipo


  To Whom It May Concern

  Ministry of Home Affairs
  Immigration Department
  Passport control office
  Dar es Salaam


  Dear sir/ Madam


  Re: Application for Tanzanian Passport for Kingwendu

  Kindly refer to underlined caption above.

  Kingwendu Mwamlima is my son aged 3 years, with great honor I would like to submit his application for Tanzanian passport. At the moment am doing boxes in US at some point I would like my family to visit me in the US. As one of the requisite for visa inquiry Kingwendu will need a Tanzanian passport.

  With this application I have attached relevant copies of my passport to support the application process.


  Sincerely yours


  MR Kibakuli Maharagwe


  Hapo mzee unaweka na copy za passport yako halali, jamaa ajaze form na kulipia 50,000 atachukuliwa alama za vidole na atapewa passoprt sawa mazeee....wabongo mnapenda sana dezo wewe ulipataje yako? ama ulitafutiwa? usije uliza visa atapataje lol
   
 4. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  thanks alot Masanilo,i do appreciate.
  mimi ya kwangu haikuwa na usumbufu wowote kwa maana ilikuwa inashughulikiwa na wizara ya elimu moja kwa moja kwa vile ilikuwa ya mwanafunzi,hivyo haikuhitaji tena kuwepo na barua ya mwaliko.
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  .............ha ha haaaaaaaaa, Masanilo bwana, anyway kwanza unamshari mtu, pili unamdongo kwa uvivu wa kufikiri....safi sana.........ha ha haaaaaa
   
 6. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Kwanza aende ofisi ya uhamiaji achukue fomu aijaze halafu ambatanishe na vitu vilivyotajwa katika fomu;na gharama ya fomu ni Tshs10,000/=tu.
  Pamoja na hayo,pia asisahau kubeba vifuatavyo:vitambulisho vyake;cheti chake cha kuzaliwa;cheti cha kuzaliwa cha baba/mama.
  Vinginevyo itamuwia vigumu;atalazima kwenda kuapa mahakamani/kwa mwanasheria aliyesajiliwa(Wakili/advocate).
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Inashangaza. Hivi ni kweli kuna umuhimu gani wa invitation letter ili kupata passport ya TZ? Passport ni haki ya kila TZ citizen.
   
 8. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Hapa inawezekana kabisa kuna mambo mawili yamechanganywa (Visa na Passport). Passport huwa hahihitaji barua ya mwaliko ila kuna swali la kizushi linalouliza kuwa 'KWA NINI UNAHITAJI PASSPORT' ila kama unahitaji visa ndio mambo ya barua ya mwaliko, kama ni kwa ajili ya masomo utahitajika admision letter n.k
   
 9. Mtimti

  Mtimti JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 912
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 60
  ndg yangu kwa hilo la watu uhamiaji kutaka barua ya mwaliko usilikatae,hawa jamaa huwa hawaeleweki,nakumbuka rafiki yangu walimtaka barua ya chuo,nikamtengenezea barua ya uongo na kweli WAKAIKUBALI,
   
 10. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Nadhani ukipita au akiomba kwa njia halali passport inaweza kuchukua mwaka mzima hajapata maana hao watu sijui hata nisemeje kwa kweli,ila kama unataka shortcut inaweza kutoka kwa one day na hata wasitake hiyo barua.....Yangu ni hayo tu!!
   
 11. M

  Mkubwa Dawa Member

  #11
  Mar 14, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Lakini sijui tatizo ni nini pale Uhamiaji kwani wameandika Pasipoti ni haki yako Mtanzania na bado kuna vikwazo mbalimbali kuipata wakati ukitumia shortcut ndani ya cku mbili au tatu inakuwa ishatoka! Bongo kaazi kweli kweli!
   
 12. I

  Ikena JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 482
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 60


  Mkuu hapo kwenye ya king'wendu na kibakuli ungemtaadharisha asije aka-paste kama yalivyo. Nakumbuka kuna mshikaji nilisomanaye na sasa ni kigogo serikalini aliniigiliza mtihani wangu mpaka na jina kabisa.

  Barua kama hii huyo mshikaji akimtumia ndugu yake wa Dar salaam atamuona kichwa kishenzi, kumbe amedesa sehemu,,,,,,
  Don't quote me seriously.
   
 13. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,793
  Likes Received: 6,304
  Trophy Points: 280
  Kupata passport uhamiaji haiihaji invitation letter. yoyote. Kama aliaambiwa hivyo labda ilikuwa wanamtaka atoe rushwa.

  Kama angekuwa anatafuta visa, hapo sawa. Au mzee ulikuwa una maana ya visa??
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kama kitu hujui kaaa kimya, uhamiaji lazima uonyeshe kithibitisho cha kuwa unataka kusafiri na nje ya nchi ndo wanakupatia passport baada ya kupitia taratibu zao! kama unakwenda shule, safari ya kikazi, ama hata kama kutembelea mtu unaonyesha na viambatanisho vingine unapata passport
   
 15. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kaka,

  nenda google halafu seach for "sample invitation letter to UK" hapo utapata kila aina ya sample invitation letter.

  Lakini pia inashangaza sana kuona kwamba Serikali yetu inaweka vikwazo vingi kwa ajili ya wananchi kupata passport. Kupata passport is a frustrating business leave alone kupata VISA ambapo hapo napo ni kihunzi cha futi elfu.

  Kwa nchi za wenzetu mfano Nigeria, Ghana, Ethiopia Senegal kazi za waziri wa mambo ya nje ni kulloby wananchi wao wapewe visa ili wende nje ya nchi kwani wanaamini wakienda huko itasaidia sana katika kupata mwanga na hata opportunities mbali mbali kwa ajili ya ujenzi wa wanachi wao wenyewepe personaly au hata kwa ajili ya mataifa yao. ndio maana kw awale waliobahatika kwenda nchi za watu, karibia kila muafrika unaekutana nae ni Mnigeria ua mtuu kutoka Ghana au mtu kutoka west Afrika, sana sana ukikuta ni kutoka East Afrika basi utakuta ni kutoka Kenya. Watu hawaifahamu Tanzania kabisa kabisa. Wachache wanafahamu mlima kilimanjaro ambao wanajua upo Afrika Kusini au Kenya.

  Sisi huko nafikiri Waziri Membe yeye zaidi ya kufurahia safari zake za nje akiongozana na Kikwete sijui kama anajua umuhimu wa kupigania Watanzania wapewe Visa au masharti yalegezwe kidogo au la?

  Au sujui waziri Marsha analifahamu hili la umuhimu wa wananchi kupata passport kwa ajili ya kusafirinje ya nchi.

  Ukiliangalia hili jambo kwa upana pia unapata jibu kwanini hata Air line business kwa mfano ya Air Tanzania itaendelea kudidimia kwa sababu wao zaidi ya kufikiria local flights (kilimanjaro -Dar-Mwanza) hawana mpango wowote wa kuwa na International Expansion kwa sababu Watanzania wanaosafiri nje ni wachache sana hivyo hawawezi hata kufikia malengo ya kupata idadi ya kutosha ya abiria wanaosafiri nje so kunakua hakuna sababu ya ku-invest on International Routes, na hivo kubakia tukiwalaumu Wakenya (Kenya Airways), kumbe wao wanatuacha kwa mambo madogo madogo ambayo sisi wenyewe hatuyaoni au tunayafumbia macho kutokana na Ukiritimba na Urasimu uliokidhiri.

  Samahani kwa kupitiliza nje ya hoja but i thought its better hili suala likaangaliwa kwa upana na marefu yake not just "an invitation letter"
   
 16. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mwambie huyo ndugu yako akazane anapokwenda kule uhamiaji hahitaji barua ya mualiko kuomba passport wanatafuta njia ya kuomba rushwa hao,aombe kuonana na supervisor wizi mtupu Bongo.Sijui tutaendelea lini sisi aibu tupu.Nilizani haya mambo ya kipumbavu yamekwisha kumbe bado tu hatubadiliki.si lazima uwe na safari kuwa na passport.Kwa wenzetu passport unajaza fomu posta na unaituma hata huyo ofisa wa uhamiaji humuoni sisi mlolongo kibao ....Think Twice.


  SAHIBA,
   
 17. Chocolate

  Chocolate Senior Member

  #17
  Mar 16, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Nadhani hayo ni mambo ya zamani lakini kwa sasa nawapongeza watu wa uhamiaji kwasababu ndani ya siku tano tu unapata passport yako na unalipa gharama halali za serikali tu hakuna cha rushwa wala nini wala sijaona usumbufu wowote labda foleni siku ya kuchukua ambacho ni kitu cha kawaida!
   
 18. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hongera Uhamiaji siku hizi hakuna shida jamani, huna passport ni ukihiyowako.

  Kuna watu wanapenda rushwa bila kutoa hawana amani. ila si watu wa uhamiaji wanataka.
   
 19. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Passport unapewa kwa sababu ni haki yako, its not a must uwe unasafiri. Barua yako inachemka labda kama unataka kutuma hiyo barua ubalozi wa marekani wakupe visa.
   
Loading...