Investigative Journalism in Tanzania:Tatizo ni Umasikini, Katiba na Vitisho!-Jicho Letu Star TV.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,670
119,301
Wanabodi,
Naangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa na Star TV.

Miongoni mwa hoja iliyonigusa ni hii kuhusu uwezo wa media zetu za Tanzania kufanya stories za uchunguzi, ukilinganisha na nchi majirani zetu Kenya ikitolewa mfano.

Wazungumzaji ni Masoor , Edwin Soko, na moderator ni Nguli Dotto Emmanuel Bulendu.

Dotto ameuliza mbona Tanzania hatuna reporter wa Investigative Story kama Muhammed Amin wa Kenya?.

Edwin Soko akasema kikwazo kikuu ni Katiba yetu haina guarantee ya Press Freedom, Katiba ya Kenya imeweka Uhuru wa Habari ndani ya katiba yao, hivyo waandishi wa Kenya wana guarantee ya kuandika habari za uchunguzi bila uoga kwa sababu uhuru huo uko guaranteed, waandishi wanaoandika habari za uchunguzi wanapatiwa ulinzi na government support. Media za Kenya zina uwezo na nguvu ya kiuchumi wa kuchunguza chochote na waandishi wake wamefanyiwa capacity building kufanya investigative pieces.

Mansoor amesema media in Tanzania kwanza inakabiliwa na ukata, ili kufanya a good investigative pieces inahitaji ample resources kitu ambacho media za Tanzania hatuna, hii inamaanisha media zetu ama ni media masikini au ni media njaa njaa.

Mansoor akaendelea kusema kuwa tatizo jingine ni vitisho, media in Tanzania imetishwa, akatolea mfano wa chombo fulani kilichokuwa mstari wa mbele kuripoti migogoro ya wakulima na wafugaji, kimetishwa, sasa hakuna stories hizo!.

Akatolea mfano suala la mchanga wa dhahabu kama Mkuu ameshasema tunaibiwa, ukifanya uchunguzi ukakuta hakuna wizi, media gani itathubutu ku publish hiyo story?.

Soko akasema Muhammed Amin ana resources, anafuatilia uchunguzi hadi nje ya nchi, anaulizi, na ana timu ya kikosi kazi. Hapa media gani zenye resources za kufuatilia hata story ya mchanga tuu wa dhahabu, ili kujua kama tunaibiwa au la, lazima mwandishi aende kule unakochakatwa, na kujua kinachopatikana baada ya uchakataji, sasa kama hatujui hata kilichomo tuu ndani ya content, ile tuu mwandishi kuingia mgodini kushuhudia packing ni issue, itakuwa kufuatilia uchakataji? . Muhammed Amin anaweza kwa sababu ana resources!.

Bulendu akacrush hoja ya resources, akasema mbona tulikuwa na Stan Katabalo na aliweza kwenye Kashfa ya Loliondo bila resources?, mbona Jerry Muro aliweza kwenye rushwa ya matrafick bila resources, mbona mwanahalisi waliweza kwenye kutekwa kwa Ulimboka, sio kila uchunguzi unahitaji resources kivile.

Bulendu akatolea mfano sakata vyeti feki la Bashite, limetokea hapa hapa Mwanza, waandishi wameshindwa kwenda Kolomije, Nyanza Primary, Pamba Secondary, Chuo cha Nyegezi, Kumfuatilia Paul Christian Original, etc etc, wameshindwa nini na walihitaji resources gani?!.

Bulendu akazishangaa media zetu kwenye selectivity ya prominence, na kutolea mfano wa hotuba ya Waziri Mkuu yenye mambo muhimu kitaifa na kiuchumi iliyochukua zaidi ya saa nzima kuwasilishwa, haikupewa umuhimu kama story ya Spika kumuita Mbowe na Mdee kwa kumtukana! . Uzalendo uko wapi?.

Bulendu akasema japo jukumu la media ni kusema kweli daima lakini kwenye kutanguliza mbele maslahi ya taifa in particular situation, media inaruhusiwa kusema uongo mtakatifu unaofanywa kwa nia njema.

My Take.
Kufuatia mimi kuwa ni mwandishi,
1. Tanzania tunao waandishi wengi wazuri wenye uwezo wa kufanya investigative stories za kiwango cha Mohemed Amin ila wanakwamishwa na resources.
2. Media za Tanzania zinakabiliwa na ukata wa hali ya juu sana kiasi kwamba haziwezi kugharimia good investigative stories.

3. Ni kweli kuna vitisho vya viongozi kwa media hivyo media kuingia uoga. When the topman is not happy about any programme, then that program will just die!, hivyo ndivyo "Kiti Moto" kilivyo kufa, sasa kama Mkuu anapenda vipindi kama Shilawadu hadi kunyanyua simu kupiga Clouds TV kuwapongeza kwa Shilawadu, then unategemea nini kama mtu atatengeneza Documentary kuthibitisha Daudi Bashite ni lijizi fulani liliiba vyeti vya Pauli Christian, lilifoji jina, shule, vyuo na kufanikiwa kwa kujikombakomba, what a chance that program will survive na TV gani itathubutu kurusha? .

Tanzania we still have a long way to go.

Nawatakia Jumamosi Njema.

Paskali
 
Dotto ameuliza mbona Tanzania hatuna reporter wa Investigative Story kama Muhammed Amin wa Kenya?.

Edwin Soko akasema kikwazo kikuu ni Katiba yetu haina guarantee ya Press Freedom, Katiba ya Kenya imeweka Uhuru wa Habari ndani ya katiba yao, hivyo waandishi wa Kenya wana guarantee ya kuandika habari za uchunguzi bila uoga kwa sababu uhuru huo uko guaranteed, waandishi wanaoandika habari za uchunguzi wanapatiwa ulinzi na government support. Media za Kenya zina uwezo na nguvu ya kiuchumi wa kuchunguza chochote na waandishi wake wamefanyiwa capacity building kufanya investigative pieces.

Paskali
 
Mansoor amesema media in Tanzania kwanza inakabiliwa na ukata, ili kufanya a good investigative pieces inahitaji ample resources kitu ambacho media za Tanzania hatuna, hii inamaanisha media zetu ama ni media masikini au ni media njaa njaa.

Paskali
 
Wanabodi,
Naangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa na Star TV.

Miongoni mwa hoja iliyonigusa ni hii kuhusu uwezo wa media zetu za Tanzania kufanya stories za uchunguzi, ukilinganisha na nchi majirani zetu Kenya ikitolewa mfano.

Wazungumzaji ni Masoor , Edwin Soko, na moderator ni Nguli Dotto Emmanuel Bulendu.

Wenye nafasi fuatilieni

Paskali

Kamarada Pascal mbona siku hizi umekuwa mpole sana humu? Kulikoni? Nimefurahi kusikia classmate wangu wa SAUT Edwin Soko ' anatiririka ' huku Kaka yangu Kidarasa Dotto Emanuel Bulendu kama kawaida yake akiongoza Kipindi. Kama una contacts zao waambie GENTAMYCINE anawasalimu sana na ninawakubali mno.

Kamarada Pascal nasubiri jibu langu kwanini siku hizi ' umepoa ' sana isivyo kawaida?
 
Mansoor akaendelea kusema kuwa tatizo jingine ni vitisho, media in Tanzania imetishwa, akatolea mfano wa chombo fulani kilichokuwa mstari wa mbele kuripoti migogoro ya wakulima na wafugaji, kimetishwa, sasa hakuna stories hizo!.

Akatolea mfano suala la mchanga wa dhahabu kama Mkuu ameshasema tunaibiwa, ukifanya uchunguzi ukakuta hakuna wizi, media gani itathubutu ku publish hiyo story?.

Paskali
 
Mansoor akaendelea kusema kuwa tatizo jingine ni vitisho, media in Tanzania imetishwa, akatolea mfano wa chombo fulani kilichokuwa mstari wa mbele kuripoti migogoro ya wakulima na wafugaji, kimetishwa, sasa hakuna stories hizo!.

Akatolea mfano suala la mchanga wa dhahabu kama Mkuu ameshasema tunaibiwa, ukifanya uchunguzi ukakuta hakuna wizi, media gani itathubutu ku publish hiyo story?.

Paskali
Hizi sababu zote walizotoa ni kisingizio tu! Investigative Journalism inahitaji will and courage ya journalist tu! Hayo mengine ni ziada!
 
Soko akasema Muhammed Amin ana resources, anafuatilia uchunguzi hadi nje ya nchi, anaulizi, na ana timu ya kikosi kazi. Hapa media gani zenye resources za kufuatilia hata story ya mchanga tuu wa dhahabu, ili kujua kama tunaibiwa au la, lazima mwandishi aende kule unakochakatwa, na kujua kinachopatikana baada ya uchakataji, sasa kama hatujui hata kilichomo tuu ndani ya content, ile tuu mwandishi kuingia mgodini kushuhudia packing ni issue, itakuwa kufuatilia uchakataji? . Muhammed Amin anaweza kwa sababu ana resources!.

Paskali
 
Mansoor akaendelea kusema kuwa tatizo jingine ni vitisho, media in Tanzania imetishwa, akatolea mfano wa chombo fulani kilichokuwa mstari wa mbele kuripoti migogoro ya wakulima na wafugaji, kimetishwa, sasa hakuna stories hizo!.

Akatolea mfano suala la mchanga wa dhahabu kama Mkuu ameshasema tunaibiwa, ukifanya uchunguzi ukakuta hakuna wizi, media gani itathubutu ku publish hiyo story?.

Paskali
......
.....kuukwea Mbuyu ni kazi kubwa inabidi uuzunguke tu hahaha
 
Mansoor amesema media in Tanzania kwanza inakabiliwa na ukata, ili kufanya a good investigative pieces inahitaji ample resources kitu ambacho media za Tanzania hatuna, hii inamaanisha media zetu ama ni media masikini au ni media njaa njaa.

Paskali

Hilo la ukata uliweke vizuri. Siamini kama ni financial constraints. Nadhani ni ukata kwenye kichwa.
 
Wanabodi,
Naangalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa na Star TV.

Miongoni mwa hoja iliyonigusa ni hii kuhusu uwezo wa media zetu za Tanzania kufanya stories za uchunguzi, ukilinganisha na nchi majirani zetu Kenya ikitolewa mfano.ratee

Wazungumzaji ni Masoor , Edwin Soko, na moderator ni Nguli Dotto Emmanuel Bulendu.

Wenye nafasi fuatilieni

Paskali
Tatizo letu hapa si KATIBA, VITISHO, na UMASKINI.
Tatizo la issue nzima INVESTIGATIVE journalism hapa Tanzania ni WOGA na UMBEYA na UZUSHI.
Kuna tofauti kati ya Real investigative journalism na UZUSHI.

Hata huyo Mohamed Alli wa Kenya amewahi KUTISHWA si mara moja. Na si SERIKALI bali ni wale watu he WRONGLY rubbed shoulder with.

Maana yale anayoibuaga huwagusa wasiogusikaga kirahisi.
Na yale aliyokuwa akiatoa mengi yalijaa UKWELI.

Penye KWELI huwezi KUKAMATWA lakini penye UONGO hapo simpi mtu yeyote guarantee!
 
Bulendu akacrush hoja ya resources, akasema mbona tulikuwa na Stan Katabalo na aliweza kwenye Kashfa ya Loliondo bila resources?, mbona Jerry Muro aliweza kwenye rushwa ya matrafick bila resources, mbona mwanahalisi waliweza kwenye kutekwa kwa Ulimboka, sio kila uchunguzi unahitaji resources kivile.

Bulendu akatolea mfano sakata vyeti feki la Bashite, limetokea hapa hapa Mwanza, waandishi wameshindwa kwenda Kolomije, Nyanza Primary, Pamba Secondary, Chuo cha Nyegezi, Kumfuatilia Paul Christian Original, etc etc, wameshindwa nini na walihitaji resources gani? .

Paskali
 
Soko akasema Muhammed Amin ana resources, anafuatilia uchunguzi hadi nje ya nchi, anaulizi, na ana timu ya kikosi kazi. Hapa media gani zenye resources za kufuatilia hata story ya mchanga tuu wa dhahabu, ili kujua kama tunaibiwa au la, lazima mwandishi aende kule unakochakatwa, na kujua kinachopatikana baada ya uchakataji, sasa kama hatujui hata kilichomo tuu ndani ya content, ile tuu mwandishi kuingia mgodini kushuhudia packing ni issue, itakuwa kufuatilia uchakataji? . Muhammed Amin anaweza kwa sababu ana resources!.

Paskali
Mkuu Pascal Mayalla kama nilivyosema kwenye post #9 kuwa hivi vyote ni visingizio ambavyo watanzania ndio umekuwa utamaduni wetu! Investigative journalism sio lazima uanza/ufanye investigation ya mambo makubwa na yanayohitaji resources kubwa! Kuna vitu simple sana vinavyotokea hapa hapa Bongo. Kama nilivyosema hizo sababu zao ni kisingizio tu.
 
Mohammed ali anaweza kuchukua nafasi za waandishi wa habari wote hapa kwetu. Naona kama kenya ndio kuna hatari kuliko tanzania miaka yote lakni Mwandishi wa habari huyu amefukua makaburi kwa ujasiri unaovuka kaburi.
Sio Drugs, Westgate anawasema hadi wajeda, Fake pastors, Illigal Immigrants, Uhuru, kila kona ukiangalia makala zake unasisimka dakika ya kwanza hadi maandishi ya mwisho

waandishi wetu wakina Paskali mtusaidie ili mpate tunu kwa Mungu na Kwa wanadamu.
 
Sasa hiyo courage utaipata wapi bila kuhakikishiwa usalama na uhuru wa kufanya kazi?
Ohooo my God! mtanzania utamjua tu! Mkuu ni hivi: Kwanza nianze kukuuliza: Unajua maana ya neno courage? Nadhani utakuwa unajua kwani linakaribiana na neno ujasiri! Sasa ukishazungumzia neno ujasiri usitegemee tena kuhakikishiwa usalama wako. Ujasiri ni ile hali ya kupambana na jambo la hatari kwa kutumia mbinu bila kuogopa. Ukishahakikishiwa tena usalama na uhuru wako hapo hakuna ''courage'' au ujasiri. Na mara zote investigative journalism zinafanyika kwenye mazingira ya hatari na bila uhuru!
 
Back
Top Bottom