Introverts tunaishi maisha 'unique' sana

FB_IMG_16366233676616932.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi ni introvert ila nina madem 4 mmoja tu ndo nilimtongoza wengine wote wamenitongoza wenyewe nikaona tu nikubali nisije kukataa nikaonekana mchele coca

Shida ninayopata ni kuwa siwezi kuongea kwenye sim muda mrefu sijui kubembeleza yaani sipo romantic na wasiponitafuta na mimi siwatafuti wameshazoea hata sms kila siku wanaanza wao na hela hawaniombi

ila nina huruma sana sipendi kusikiliza shida zao maana huruma niliyonayo itabidi niwasaidie wakati hela yangu nimewekea malengo mengine
Likewise
 
inaonekana kuna watu wengi hawawajui introvert. hii ni inborn behaviour wala hatujipendei. ukitulazimisha kuishi maisha yako unakuwa unatuburuza na tunateseka. vile tulivyo ndio tunafurahia. tukisema tunakaa ndani tunajifungia usifikiri wote tuna akili za punyeto ambayo hata maextrovert wanapiga. ni kwamba, ratiba yangu yote imejaa. nikiamka asubuhi naenda kazini na consentrate na kazi hadi muda wa kazi uishe, nikitoka hapo sina ujinga mwingine ni kwenda home kufurahi na watoto wangu na mke, kupumzika na kuangalia tv au kama kuna kazi binafsi nafanya. au navaa zangu raba na track suit naenda kufanya mazoezi ya kukimbia au hata mpira. ila huwezi kunikuta ati nafurahia kwenye kwenye sherehe za arusi, vipaimara sijui sherehe za maofisini watu mnacheze mziki, hatuijui night club ipoje. kitu pekee nitafanya ni kwenda church tena sitaki kukaa mbele, nikae nyumba au katikati ya watu nisionekane sana.

kuna jamaa yangu mmoja ana tabia za introvert kama za kwangu, alikuja church, ukimpa mike mwambie aende pale mbele ajitambulishe au ajieleze jambo, utamwonea huruma. kuwa introvert ni kuumbwa ukiwa mtu wa aibu/kutokuwa na uwezo wa kuongea mbele za watu, kutokuwa na uwezo kuexperess sana mbele za watu, wewe ni kufanya mambo yako kimya kimya na kwa mkatomkato. tumeumbwa hivyo. ila kwasababu tunajijua tuna tatizo (kwasababu kiukweli hilo ni tatizo, nimefaight maishani nimeshindwa kuliondoa), huwa tunajaribu kufunika kwa kupiga kazi sana, kutafuta pesa sana ili pesa ituheshimishe. la sivyo, hatuna heshima kwasababu hata kujieleza mbele za watu hatujui yaani, ila kujieleza kwenye makaratasi na kwenye pesa hapo hutupati.
Bien ma nigha
 
Back
Top Bottom