Introducing: Farida

Status
Not open for further replies.
Heshima zenu wakuu,

Namtambulisha Admin mpya; dada yetu Farida, natumaini mtampa ushirikiano wa karibu katika utendaji wake.

Ahsante

NAOMBA NIJUE umri wake, kama kaolewa na kama anapatikana kwa kuongea na kucheka" live"
 
duhh wabongooo!!!!!mwee ngoja nikaage kimya mie
mie nakukaribisha sisteri farida
kingine naomba nijulishwe je huyo farida yeye ni bubu wa kutype??au ndo anawajibu woote wamuulizao maswali hapa kwa kuwa pm??
 
...shauri zenu, "penye urembo pana ulimbo!", ...hongera Farida kwa majukumu mapya.
 
Heshima zenu wakuu,
Namtambulisha Admin mpya; dada yetu Farida, natumaini mtampa ushirikiano wa karibu katika utendaji wake.

Ahsante

Moyo meshikwa ganzi, mwili damu nazunguka
Nimejawa na simanzi, mwili jasho lanitoka
Watu wapenda uzinzi, Kuna gonjwa sotibika
XP Nawaeleza wazi, yasije yakawafika

Shikeni wasia wangu, Muuhifadhi moyoni
Fateni njia za Mungu, Mtaongoka duniani
Msiache omba Mungu, kwa rehma na amani
Fanyeni sana ibada, Najua nyinyi watu wa Dini

Dada Farida Pokea Pongezi zangu za dhati
Mimi ninakuombea Huwe makini na chati
Sichelewe kugundua Kashfa na chafu Hati
Najua kazi waijuwa Penye kosa kosoa

Moyoni nina Furaha Dua nina kuombea
Mungu akupe Jaha, Na busara kukuenea
Akuepushe na Karaha Na kila lenye udhia
Fanyakazi Fanyakazi Waepuke mabazazi
 
karibu Farida..........najua PM yake imshajaa sasasa hivi sio watu kubanana huko.....
 
---Da' Farida, karibu jamvini... i hope utaweza kujibu pm zangu zilizonyingi kwa mamods...

---Nami kama Kithuku, sitosema mengi. Niwaachie wenzangu waoshe vinywa vyao, naona wakina Mkjj walishaomba na namba za simu tayari. Penye urembo pana ulimbo - Mchongoma ameshataja hapo juu!

Karibu na Hongera kwa Majukumu Mapya Farida!

SteveD.
 
Karibu dada, tunaomba urithi huo moyo wa invisible. Maana kwa kweli amefanya mengi ambayo ni Mungu tuu ndo atakaye mrudishia. Warmly welcome.
 
---Da' Farida, karibu jamvini... i hope utaweza kujibu pm zangu zilizonyingi kwa mamods...

---Nami kama Kithuku, sitosema mengi. Niwaachie wenzangu waoshe vinywa vyao, naona wakina Mkjj walishaomba na namba za simu tayari. Penye urembo pana ulimbo - Mchongoma ameshataja hapo juu!

Karibu na Hongera kwa Majukumu Mapya Farida!

SteveD.

Aretha-Franklin-Here-We-Go-Again-119290.jpg
 
Karibu dada Farida!

Mtu wa nyanda za kati, salama huko mliko?... nipo Mysore kwa muda baada ya shughuli fupi nitarudi zangu Ukingani.

Mkulu, sasa nikuulize wewe gwiji la mitandao na mawasiliano.... huyu da'Farida tunayemkaribisha mpaka leo hii kwenye profile yake nimecheck hajaweka hata post moja, na inaonekana alishakuwepo hapa muda mrefu.... kwa experience zenu hapa, je mnakumbuka post yake yoyote ambayo labda imefutwa tu?!! (na kama ilikuwa quoted pahali itakuwa bomba sanaa) just curiosity man... hope it won't kill me!!! lol

Baadae, Wasalimu huko
 
FARIDA,naadhani unaelewa,kwamba JF,sasa hivi ni worldwide,tumetapakaa on all 4 corners of the earth,hivyo kimila na tabia,obviousily tutakuwa tunatafautiana sana,huku nilipo mimi,unofficial protocol inasema,any appointment etc etc one has to acknowledge in the form of eg thanks or tuko pamoja etc etc,as such we are still waiting to hear from you.at least this will assure us albeit in a tiny way ,kwamba tuko pamoja
 
dada farida karibu kwenye uwanja wa midahalo natumaini utaongeza nguvu kwenye hili jeshi la wapiganaji
 
Sidhani kama nimechelewa sana kukukaribisha na kukutakia heri kwenye mafanikio yako,,

huko kenya bado kuna watu wanafanya sherehe za kushinda ubunge na uwaziri so usijali!
 
Farida upo kimya sana dada...hata salamu tu?
Siku moja moja tunapenda japo salamu yako.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom