Intro

Esta

New Member
Nov 15, 2010
4
0
Jina langu ni Esta. Nimevutiwa na forum hii kwa kuwa na majadiliano na mijadala ya kila aina. Natumai nitajifunza mengi.

Nina issue inanisumbua sana. Nayo ni kuhusu uchafu uliokithiri katika miji yetu ya kibongo. Katika hili nisingependa mtu alaumu. Kama ni makosa yalifanyika na kila mtu anajua. Ninachotaka hapa ni kitu gani kifanyike kwa sasa. Nataka mikakati ya ufumbuzi ili tusiendelee kuisha kama vile nchi haina watu wanaoelewa.

Natanguliza shukrani zangu kwa mchango wenu.
 
Esta, karibu ssana.
Karibu kwenye janvini. na karibu kwenye majukwaa yote, ukiona una-stress karibu MMU. na unakaribishwa kwenye chama - ISC, tuwasiliane kwa maelezo zaidi.
 
Asante sana kwa kunikaribisha (kwa ukarimu wenu). Lakini nitafarijika sana kama tutajadili kwa kina kuhusu usafi. Kuna mmoja amesema hatuna cha kufanya ila tuangalie zaidi maisha ya baadaye. Nakubaliana naye, lakini ingekuwa hivyo, kulikuwa na haja gani mwanadamu kupewa utashi? Si tungekuwa sawa tu na nguruwe? Fikiria, tumepewa akili, pia tumepewa mikono. Ninavyoelewa mimi, binadamu tumependelewa ili tuweze kupambana na mazingira. Cha ajabu, sisi tumeshindwa kuitumia hiyo zawadi. Matokeo yake tumeendelea kujilinganisha na nguruwe, kama vile hatuna akili kama wao. Mbona wenzetu wazungu wako wasafi? Cha kushangaza zaidi, tunapenda sana kuwaiga wazungu karibu kwa kila jambo, mbona usafi hatuwaigi? tunaiga yasiyo na manufaa tu? Angalia, hasa akina mama, mara tujichubue, mara nywele tuzibadili! lakini kwenye usafi, mmmh! Na ukisema tuishi hivyo hivyo tu, ina maana kama utaishi miaka 80 na leo hii una miaka 32, miaka yooote hiyo utaendelea kukaa kwenye uchafu uliokithiri? Kuhusu miji, jiji la Dar ndio kinara wa uchafu Tanzania.
 
Kusema kweli si watanzania, na hasa wakazi wa Dar, inabidii tubadilike saaaaaana. Mi siku zote najiuliza inakuwaje miji mingine kama Bujumbura, Kigali, Nairobi na hata Kampala ni misafi!!? Wenzetu wamesomea wapi kuliko sisi!!? Sasa hivi Dar mvua ikinyesha kidogo tu ni matatizo matupu. Kwa sasa nasikitishwa sana na utupaji hovyoooo wa mifuko ya plastiki. Barabara zote kubwa kwa sasa hazitamaniki kwa uchafu pembeni.

Tatizo ninalo liona ni mfumo mbovu wa uongozi na wananchi kutokuwa na nguvu za kuwasimamia viongozi na hasa wa kisiasa. Wananchi pia wanachangia kwa kiasi kikubwa kwa kukosa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira. Lakini rushwa na uporaji wa mali za umma ndio vimetawala. Nenda kaulize budget za kufanya usafi Jiji Dar; utashangaa!!!!!! Kinondoni ilipitisha sheria ndogo kuhusu uchafuzi wa mazingira na adhabu zake, lakini haifanyi kazi...maana hakuna mfumo wa kusimamia.

Suluhisho ni kuwa na mfumo tofauti wa uongozi. Tuna sheria nyingi sana lakini hazina manufaa kwetu. Moshi wameweza...tujifunze toka hapo.
 
Esther_M, angalau wewe umesema cha maana. Ukitegemea serikali watende, tutaendelea hivi hivi miaka nenda rudi. Unaonaje tukiunda vikundi vya kijamii ambavyo tutasimamia na kuwakumbusha hao viongozi. Nimeanza cha kwangu na ninaendelea kukaribisha wakereketwa. Lakini sitaki wasemaji, maneno matupu ndio yametufikisha hapa
 
Karibu sana jamvini. Taratibu tutafika na hongera kwa mwanzo mzuri wa mawazo mapya na mapana
 
karibu sana,tungekuwa na mabibi afya 1000 kama wewe tz ingekuwa poa sana
 
Back
Top Bottom