Interview with Jakaya Kikwete, president of Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Interview with Jakaya Kikwete, president of Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alpha, Mar 14, 2009.

 1. A

  Alpha JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  FT.com / UK - Interview with Jakaya Kikwete, president of Tanzania
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Samahani wanaJF. Kwa wale watanzania, kwa keli hatuna presedent. Yale yale tuliyokuwa tukiya jadili juzi tu juu ya mikakati ya tanzania/Africa kupambana na economic down turn ndio yamejidhihilisha katika mahojiano haya. JK kathibitisha kuwa hana plan B au mpango mwingine wakupambana na economic down turn. Nionavyo mimi, kitita cha economic stimulus package kinawatoa mate viongozi wa Africa hivyo wanaona ni hakiyao na wanatakiwa kuwa part ya mgao huo. LoL. Alitakiwa aulizwe pia ''Ilikupambana na hali hii ya kuyumba kwa uchumi anafikili Africa inahitaji kiasi gani?'' hapo ndipo tungedhihilisha zaidi kuwa hata chakufanyia hizo pesa hakijafikiliwa. Jamani hivi hakuna washauri kweli wa Rais Tanzania?. Anyway Umoja wa Africa hauna kamati ya kuzungumzia mambo haya mpaka JK anapresent vitu vya ajabu kiasi hiki?. Hapa kazi tunayo na kama ndio mwendo huu mpaka 2015 basi watz tuandike maumivu.
   
 3. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Lately I had one burning question. After this crisis, some 1st world countries said that there's a need for world financial reform. African countries have always voiced that they have been left out on world matters. So my question is:

  Is this what our leaders going contribute if they are involved in any world reforms?

  All they know is HEADLINES, "The world is in financial crisis". What are they doing, nothing, "WE NEED BAILOUT". What's their plan, "STIMULATE ECONOMY"

  They have know idea what they are talking about. I think they need VIA@#% to stimulate their @#$%&.
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  I am sorry ukichukua ile panel tulipomwona mheshimiwa rais na vocabulary yake na ukiangalia majibu hapa, utajua kuwa intrview hii FT wamei-rekebisha na kuweka terminologies to make our president sound more than he is... I mean it is not a strong interview as it is but in comparison to the video feed, this is better than what he is capable of....
   
 5. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kama mpaka leo Raisi wetu hana plan na aliulizwa wakati wako BOT atafanya nini cha tofauti hana la kujibu? Kweli? Halafu eti huwa anaongea na wananchi kila mwezi, kama kweli anaongea kila mwezi mbona hana update za yeye afanye nini? Duh!! labda angeomba kuwepo na mkalimani wa Kiswahili yaani angeongea Kiswahili, inaweza kuwa tatizo ni lugha. I dont know!?
   
 6. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Lusajo, hii excuse ya lugha siwezi kukubali especially kwa sababu alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10! He doesn't know what he is talking about - alafu anadai kuwa ni mchumi! Aibu!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280
  bm21, nimeshasema mara nyingi hapa kwamba Kikwete hafai tena kupewa Urais kwa kipindi kingine cha miaka mitano kuanzia 2010. Huyu jamaa hana sifa yoyote ile ya kutuongoza Watanzania na kuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha hilo katika kipindi cha miaka minne alichokaa madarakani.

  Itakuwa ni kosa kubwa sana kumrudisha tena Kikwete madarakani na na kama atachaguliwa tena itaonyesha jinsi Watanzania tulivyo kichwa cha mwendawazimu. Kiongozi asiyefaa afanye kipi zaidi ya yaliyofanywa na Kikwete hadi tumuondoe madarakani. Miaka yake mitano inamtosha kabisa sasa ni wakati wa kuanza kutafuta kiongozi mwingine kabla ya uchaguzi wa 2010. Kikwete hatufai na hiyo siyo siri.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280
  Ndiyo Susuviri, maana kuna Wachumi na mchumi. Anaweza kabisa kuwa ni 'mchumi' maana kila mwaka pale UDSM alikuwa anaingia darasa jipya tu bila kujua chochote alichokifanya mwaka uliopita. Hata hotuba zake za kiswahili zina walakini mkubwa sana. Miaka mitano inamtosha kabisa kurudi bagamoyo kulima minazi.
   
 9. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  This election 2010 is a huge oportunity for the opposition, they should not blow it! Wale wagombea wa siku zote wakae pembeni (kina Lipumba, Mrema etc) watoe nafasi tuone sura mpya ya upinzani
  Getting back to mheshimiwa rais wetu wa sasa, hii sasa imekuwa zaidi ya aibu kwa sababu inaonyesha kuwa he is a puppet na amewekwa madarakani na interest group while he has no idea why he deserved to be president or what got him elected. Anaamini mpaka leo kuwa alishinda ndani ya chama na uchaguzi mkuu kwa sababu alihonga waandishi na aliuza sura! Na his ultimate goal ilikuwa aitwe President but nothing beyond that. Narrow mindedness is the worse type of charateristic in any leader!
   
 10. M

  MohamedSalum200 Member

  #10
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi naona rais anafaa kuendelea hata kwa miaka kumi anajitahidi vya kutosha na kama kuna uwezekano awe rais wa maisha.anaonyesha jitihada ya kutosha kwa wananchi wake viva kikwete na ccm juu tawala milele hamna kama sisi.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,669
  Trophy Points: 280
  Viva Kikwete!!!! kwa kipi alichokifanya!? Naona una faidika kwa namna moja au nyingine na ufisadi na uzembe uliojaa serikalini hadi utake Rais ambaye kazi imemshinda eti awe Rais wa maisha!!!! Mtu mzima hovyooo!!!! Kazi kweli kweli!!!! Kigumu chama cha mafis.....! Kigumu!
   
 12. t

  tk JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii issue ya Marais kufaa au kutofaa!!

  1. Nyerere, ambaye alitawala kwa muda mrefu kuliko wote, aliitwa Mussa, Haambiliki na mpaka alipoondoka akaiacha nchi taaban kiuchumi. Watu vijijini wakawa wakitembea nusu uchi. Lawama kibao kuhusu sera zake za ujamaa na watu kuliwa na simba katika operation vijiji.

  2. Akaja Mwinyi. Akarekebisha sera za uchumi. Akaleta uchumi huria, Vitu vikajaa madukani, fedha mpaka kwenye soksi. Watu wakaanza kumponda mpaka wakamwita Mzee Ruksa, Mswahili etc. kwa kuachia uchumi uendeshwe kwa uhuru. Kaondoka nchi ina neema kuliko ilivyokuwa kwa Nyerere lakini malalamiko kibao.

  3. Kaja Mkapa. Kaimarisha uchumi kwa kukusanya kodi na kubinafsisha kila kitu kwa wageni, ila Kiwira tu ambayo alijipa mwenyewe. Akaubana upinzani na uhuru wa vyombo vya habari na kuwaacha taaban. Ufisadi kibao ukajitokeza, EPA, Meremeta, Mwananchi Gold, Rada, Twin Towers, Deep green etc. Fedha nyingi za nchi akazitumia kulipa madeni ya nje. Kaondoka hali ya wananchi ikiwa ngumu, fedha hamna, watu hawana hamu naye na sasa anaitwa fisadi.

  4.Kaja Kikwete. Kaachia huru vyombo vya habari mpaka leo hii watu wamepata fursa ya kumtukana. Kasinikizwa kuondoa ufisadi na kuanza kuchukua hatua lakini watu bado hawaridhiki. Kajaribu kuimarisha mikataba ya madini ili rasilimali zisiporwe, kajenga uhusiano mzuri na mataifa makubwa, miundombinu inatengenezwa, Kalinda rasilimali za nchi, meli za wavuvi haramu zinasakwa. Hapo hapo kaachia huru economic forces. Hali ya maisha imepanda kutokana na bei za mahitaji muhimu kupanda sana. Karudisha price control kwa baadhi ya bidhaa (fuel) na huduma (daladala). Hata hajamaliza program zake, malalamiko kibao.

  Kwa kweli binaadamu si mwema. Hakuna utakachofanya kikamridhisha. Kila Rais ataendesha nchi kufuatana na hali ya wakati huo. La kushukuru ni kuwa, hakuna Rais aliye liiingiza taifa hili kwenye vita au kuleta mazingira ya kuvunjika kwa amani kwa kushabikia ukabila na udini.
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Awe Rais wa Maisha yako labda...sio. Watanzania.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Susuviri you took the thought out of my head, jamaa wame i polish kidogo. Halafu rais hana detail kabisa, anaulizwa utaenda kusema nini huko anashukuru eti kwa kupata nafasi na ataenda ku stress umuhimu wa Afrika kuhusishwa, goddamn it, umeshapewa platform, toa specificsHata kama unatoa general idea ya specific agenda na uta deal na finer details later lakini toa general idea ya specifics zako, huwezi kusema nitaongelea umuhimu wa Afrika kuhusishwa, umeshahusishwa, hiyo ni kauli ya mtu ambaye hajahusishwa anataka kuhusishwa, wewe unakwenda kwenye meza mwaga vitu.

  Otherwise una sound "I am just happy to be here"
   
 15. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  You are contradicting yourself here - "...a huge opportunity for the opposition and wagombea wa siku zote wakae pembeni...", sasa how does this come come? Wagombea wa zamani ndio hao hao wameshajiweka mkao wa kula na hakuna jipya. Vijana wa oposition kama akina Zitto Kabwe wanajiengua wenyewe kivyaovyao. Frankly speaking I don't see much coming out of the opposition camp - they are becoming a joke. Ule msemo unasemaje: heri jini ulijualo kuliko jini usilolijua......you damn skippy!

  Say whaaaat!!! Are you for real? On what proof are you basing this on, an interview in the Financial Times? Give me a break!
   
 16. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama JK anataka kuongoza tena TZ 2010 ahakikishe anaachana kabisa na lile kundi lake la ubaguzi na mbinu za ushindi wa kutumia fedha za EPA.Aungane na wana CCM waadilifu na wapinzani wenye nia njema na maendeleo ya TZ.Bila hivyo itakuwa ni kuiangamiza TZ kwani kuna kundi la mafisadi linazungua TZ na nje na kutumia mbinu mbalimbali kujisafisha na kuwachafua wengine.WaTZ mpo mjiandae kufanya uchaguzi wa mfano na wa ukombozi kwa nchi yetu.
   
 17. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  Walio wengi tunajua wazi JK hafai, lakini je tuna candidates wengine ambao wanafaa?

  Angalia wale waliogombea 2005, je mnafikiri mwingine yeyote angeshinda kungelikuwa na tofauti kubwa sana na JK?

  Labda Salim angetusaidia kwenye uongozi wa sheria na haki, lakini kwenye nchi iliyojaa mafisadi na majambazi kama TZ, wakati mwingine tunachohitaji sio haki ya wachache wanaofanya makosa bali haki ya walio wengi ambao wanaibiwa. Huenda TZ tunahitaji sticks zaidi ya carrots.

  Kwasasa tunaye huyo JK, labda muhimu ni kuangalia tunawezaje kumsaidia kwa kutimiza wajibu wetu kuliko kumlaumu kwa kila kitu. Uwezo wa kutoa hotuba pekee sio kigezo tosha cha uongozi bora.

  Matatizo ya Tanzania pamoja na uongozi mbovu lakini hata sisi wananchi tumezidi kuwa wajinga. Wengi wetu hatutimizi wajibu wetu halafu tunategemea maajabu yaletwe na rais. Huyu rais wetu ni reflection ya Watanzania wa leo. Hata akija mwingine kutoka kundi hili la Watanzania wa leo sidhani kama atakuwa tofauti sana na JK. Huo ndio ukweli wenyewe hata kama haupendezi.
   
 18. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  In summary ndugu yangu wewe una agenda nyingine kabisa zaidi ya utendaji wenye ufanisi wa viongozi wetu
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Mar 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wasomi,
  Kama wewe ni kiongozi wa Tanzania leo hii Utafanya vipi kujiandaa kupambana na Financial crisis iliyopo..
  Ningependa sana kusikia JIBU ambalo Kikwete alitakiwa kuwa nalo na kashindwa.. hii itatusaidia sisi na hata yeye Kikwete (kama kitaka) kujipanga kwani shida hii sio yake peke yake..

  Swali: Tujipange vipi watanzania ktk hali hii mbaya ya Kiuchumi duniani!..
  naomba kuwakilisha!
   
 20. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Mtanzania nakubaliana na wewe kwa kusema watanzania tumekuwa wajinga. Tumekuwa wajinga kwa sababu tuliowaamini watuamshe wametuuza (wabunge, media na vyombo vingine). Chukulia media, leo hii imejigawa eti wanaopambana na ufisadi na wasiopambana na ufisadi, kumbe ukiwaangalia wote wanapigania maslahi binafsi. Sasa hao mwenyewe nguvu akimuweka candidate atapita. Na hivo ndivyo ilivyotokea 2005 na ndiyo itakavyoendelea kama hatutakuwa makini na watu kama akina Rostam na Mengi. Ambao wameifanya media kiwanda chao cha kufyatua wanaowapenda ili waje wachaguliwe 2010.
   
Loading...