Interview Rais Samia na Azam TV, azungumzia safari, Urais, Mikopo ya Miradi ya Magufuli, Ripoti ya CAG

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,455
Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza na Tido Mhando wa Azam TV, leo Mei 4, 2022


RAIS SAMIA: HAKUNA FUNDI WA URAIS, HAUZOELEKI
Rais Samia Suluhu Hassan amesema nafasi ya Urais haizoeleki kwa kuwa kuna mambo mengi.

“Sidhani kama kuna mtu anaweza kusema ni fundi katika nafasi ya Urais, labda kama mimi ni mgeni kwa kuwa nina mwaka mmoja.

“Nilipoteuliwa kuwa Rais mshtuko ulikuwa tukiola msiba haikuwa Urais kwa kuwa nilikuwa Makamu Rais kuna mambo nilikuwa nayajua,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.


SAMIA: TULIKOPESHWA FEDHA ZA MIRADI MIKUBWA
Rais Samia amezungumzia miradi mikubwa ambayo ilikuwa ikitekelezwa wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli kwa kueleza kuwa alikuwa akiijua lakini changamoto ni kwa kuwa ilikuwa ikiendeshwa kwa fedha za mikopo.

“Miradi ilikuwa ya kwetu kwa kuwa nilikuwepo katika Awamu ya Tano na nilikuwemo katika mipango na utekelezaji, changamoto ni ukubwa wa miradi na uwezo wetu wa ndani.

“Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje? Lakini ni miradi yenye tija,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.


SAMIA: SAFARI ZINA FAIDA, LAZIMA TUTOKE TUKATAFUTE
Rais Samia amezungumzia kuhusu safari zake za nje ya nchi kwa kusema kuwa anatoka kwa kuwa safari zina faida nyingi kwa nchi ikiwemo kufungua biashara.

“Wanataka tujifungie hapa afu walie ukata mifuko ipo mitupu, sina miujiza ya kujaza mifuko yao, lazima tutoke tukatafute.

Wafanye tathmini za safari zenyewe, kila ninapoenda ninakuwa na wafanyabiashara, mfano nilikuta vikwazo 64 Kenya na vyote tulitatua baada ya kuzungumza,” Rais Samia akizungumza na Azam TV.

Ameongeza kuwa safari zake za Marekani amesaini mikataba ambayo kama itatekelezwa Tanzania itaingiza Tsh. trilioni 11.

RAIS SAMIA: NITAWATAJA WALIOCHANGIA BILIONI 7 ZA ROYAL TOUR
Rais Samia Suluhu amesema kupitia vipande vya kuitangaza Filamu ya Royal Tour ambavyo vimekuwa vikirushwa kwa miezi mitatu sasa zimeleta faida kubwa ambayo ni zaidi ya kiasi kilichotumika kuandaa filamu hiyo.

Tsh. Bilioni 7 zilitumika kuandaa filamu huku Serikali ikisema zilitokana na michango ya wadau mbalimbali

“Ni fedha nyingi lakini faida zake zikianza kuingia wataona, kuhusu waliochangia juzi Arusha niliwashukuru kwa ujumla lakini nitawataja tu,” - Rais Samia akizungumza na Azam TV.


RAIS SAMIA: TUTAFUTA KODI YA MAFUTA YA KULA
Baada ya mafuta ya kula kupanda bei Rais Samia Suluhu ameelezea kilichotokea na njia inayofuata ni kuondoa kodi ya mafuta ghafi yanayotoka nje.

“Mwaka 2020 mabadiliko ya tabia nchi hatukufanya kilimo vizuri, bajeti ya 2019/20 tulipandisha kodi ya mafuta yanayoitwa crude ambayo hayakuwa na kodi.

“Mafuta yakawa hayaingizwi, nazi na chikichi hazikutosheleza soko, hivyo bajeti inayokuja tunaenda kupitia mfumo wote wa kodi, tutaondoa kodi ya mafuta ya kula ili walete crude oil tuichakate tupate mafuta tuyasambaze ndani,” Rais Samia akizungumza na Azam TV.


RAIS SAMIA: BEI YA MAFUTA TANZANIA NI NZURI KULIKO ILIVYO MAREKANI
Kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta miezi ya hivi karibuni, Rais Samia Suluhu amesema pamoja na hali hiyo bado bei ya mafuta kwa Tanzania ni nzuri ukilinganisha na yanavyouzwa Marekani.

“Kwa Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki, Tanzania tupo pazuri, hata kwa Afrika Mashariki sisi hali ya maisha ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.

"Kwetu bei za mafuta ni nzuri zaidi kuliko mafuta yanavyouzwa Marekani, lakini watu hawataki kutafuta ukweli, wanapiga kelele za kienyeji. Tanzania hatuagizi chakula, kipo cha kutosha,” - Rais Samia alipozungumza na Azam TV, leo Mei 4, 2022.
 
Mama anaupiga mwingi...

Mungu ampe maisha marefu...

Mitano tena kwa mama... atake asitake. Kama Sukuma gang inawauma sisi hatujali tunasonga mbele
ngoja nimalizie kiporo changu kwanza
IMG_20220503_145345_608.jpg
 
Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje?
Tuachane na hilo la pili kwamba itaendeleaje.. Maana hata yeye hapa anatia shaka..! Sasa tuje kwenye tafsiri ya 'fedha zetu Lakini tulikopeshwa'... Kikiwa chako ni chako huwezi ukakopeshwa na yoyote yule bali unaweza kukopesha.. PERIOD!
Peas iliyojenga miradi mikubwa ilikuwa ni ya MIKOPO MIKUBWA YA SIRI isiyojulikana masharti yake
 
Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje?
Tuachane na hilo la pili kwamba itaendeleaje.. Maana hata yeye hapa anatia shaka..! Sasa tuje kwenye tafsiri ya 'fedha zetu Lakini tulikopeshwa'... Kikiwa chako ni chako huwezi ukakopeshwa na yoyote yule bali unaweza kukopesha.. PERIOD!
Peas iliyojenga miradi mikubwa ilikuwa ni ya MIKOPO MIKUBWA YA SIRI isiyojulikana masharti yake
Mkuu ebu tupe tathimini walozi wanamuongeleaje Mama maana nyie Ni watu muhimu !!@
 
amezungumzia miradi mikubwa ambayo ilikuwa ikitekelezwa wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli kwa kueleza kuwa alikuwa akiijua lakini changamoto ni kwa kuwa ilikuwa ikiendeshwa kwa fedha za mikopo.
Kwani yeye kuna mradi ametekeleza nchii bila mikopo?

Tusisahau juzi tu ametoka kujenga madarasa ya Covid kwa mkopo wa beki ya Dunia.
 
Kwa tafsiri ni kuwa tumeijenga kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa, tatizo ni itaendeleaje?
Tuachane na hilo la pili kwamba itaendeleaje.. Maana hata yeye hapa anatia shaka..! Sasa tuje kwenye tafsiri ya 'fedha zetu Lakini tulikopeshwa'... Kikiwa chako ni chako huwezi ukakopeshwa na yoyote yule bali unaweza kukopesha.. PERIOD!
Peas iliyojenga miradi mikubwa ilikuwa ni ya MIKOPO MIKUBWA YA SIRI isiyojulikana masharti yake
Wewe ni mkopo gani hii kati ya Trilioni 78 tunazodaiwa unajua masharti yake ama uliambiwa mashrti yake ni haya na haya na haya?
 
Back
Top Bottom