Interrogating CHADEMA and UKAWA decision of accommodating Lowassa (Uchambuzi wa kina kuhusu uamuzi w

It was and still it is a serious mistakes to have a person with undisputed allegations of "Fisadi "

Neither Ukawa nor Lowassa refuted said accusations.
 
Mkuu nimekuuliza swali rahisi nashindwa kuelewa kwa nini unashindwa kulijibu !

Kwa sasa hivi mgombea wa CHADEMA na UKAWA au mgombea wa chama kingine chochote hawezi kubadilishwa....Sasa hivi tuna options mbili tu na inabidi tufanye maamuzi.....it is either UKAWA with Lowassa AU CCM with Magufuli ! Nilichokuuliza unijibu kwa kubase kwenye hizo hoja zako ni option gani inayofaa kati ya hizo mbili ? Mbona mimi nimekwambia option ninayoona inafaa ?

Mjadala utakuwa na maana kama utajenga hoja based on these two options, otherwise ni kama nilivyosema kwenye post yangu ya kwanza itakuwa ni kupoteza muda tu........
Ninahitaji kuwa na uhakika kutoka kwako. Ninachokisoma unaposema kuwa mgombea wa chama chochote hawezi kubadilishwa maana yake ni kwamba kama kosa limeshafanyika haliwezi kusahihishwa kuhusu mgombea. Na kulingana na hoja nilizowasilisha ni kwamba Chadema walikosea kumkaribisha Lowassa kwa sababu nyingi moja kuu ni kuacha sera yake ya kupinga ufisadi. Hivyo, kama Chadema walikosea au CCM walokosea kuchagua mgombea hawawezi kusahihisha, am I right? Nkikuelewa then nitakijibu vizuri zaidi.
 
Jadili hoja usiwe kama yulealiyesema mkasome manifesto kwenye mitandao akaishia kusoma usiku wa saa 3 kwenye ITV.Mbona kujadili mambo kunawashinda sana na matokeo yake ni kuleta majibu kuntu?
Mwambie mkuu, anaacha kuleta hoja analeta matusi.
 
It was and still it is a serious mistakes to have a person with undisputed allegations of "Fisadi "

Neither Ukawa nor Lowassa refuted said accusations.
Ninachukulia post hii kwa tahadhari. Tatizo lako kubwa kulingana na pots na uzi unazoanzisha ni kuwa wewe ni mnazi wa CCM kupita maelezo. Sinahakika kama uko tayari kufanya objective discussions. Hivi, nikitoa hoja kuwa Magafuli ni fisadi, kwa mfano ufisadi wa kuuza nyumba za serikali will you support maelezo haya kama unavyo-support hoja nilizowasilisha kwenye uzi huu?
 
Huwezi kufanya naamuzi yaliyo sahihi (informed decisions) bila takwimu. Takwimu huzipati bila utafiti. Na njia moja ya utafiti ni kurejea yaliyopo (case study). 'The past provides an entry point to a correct and steady future'
Ninapenda hoja za namna hii. Thanx.
 
Katika list of shame walikuwemo vizito wengi mbona hawasemwi? Mbona anasemwa mmoja tu. Nafikiri hamtutendei haki wanyonge. Tuambieni na hao wengine wamesafishwa lini? Na nani? Kama walisingiziwa kwa nini aliyewasingizia hakuchukuliwa na hajachukuliwa hatua hadi leo?
Asante kwa hoja nzuri. Chadema kilikuwa chama pekee, tegemeo la wananchi wengi wanyonge wa nchi hii. Chadema imehimili mikikimikiki ya CCM sababu ya kupendwa kutoka kwenye mioyo ya watu. Hamna anayependa Chadema kuacha misingi yake iliyokifanya kipendwe na umma kwa dhati. Tunataka Chadema irejee misingi yake ndiyo maana tunasikitika inapopotoka namna hii kwa kumkaribisha mtu ambaye alitangazwa na alichukuliwa na Chadema kama alama ya ufisadi ulioasisiwa na CCM.
 
Yes and No.....

Kuna ambao wanaweza kufikiri kwamba CHADEMA walikosea na kuna ambao wataona tofauti.....Hilo lipo na litaendelea kuwepo regardless ya matokeo ya uchaguzi.....Kwa mfano mimi ni kati ya watu waliopinga sana Lowassa kuja CHADEMA na niliamini mwanzoni kwamba walikosea lakini sasa naamini viongozi wangu walikuwa sahihi.....

Ninachokisema hapa ni kwamba, hilo limeshapita ! Kwa maana kwamba uamuzi huo hauwezi kuwa reversed....Na kilichoko mbele yetu ni uchaguzi na inabidi tuamue kati ya UKAWA with Lowassa OR CCM with Magufuli !......Kuendelea kujadili uamuzi ambao hatuna uwezo wa kuubadili ni kupoteza muda. Na ndio maana nasema mjadala utakuwa na maana kama hatimaye utatuongoza kusema option gani ni bora.....

Ninahitaji kuwa na uhakika kutoka kwako. Ninachokisoma unaposema kuwa mgombea wa chama chochote hawezi kubadilishwa maana yake ni kwamba kama kosa limeshafanyika haliwezi kusahihishwa kuhusu mgombea. Na kulingana na hoja nilizowasilisha ni kwamba Chadema walikosea kumkaribisha Lowassa kwa sababu nyingi moja kuu ni kuacha sera yake ya kupinga ufisadi. Hivyo, kama Chadema walikosea au CCM walokosea kuchagua mgombea hawawezi kusahihisha, am I right? Nkikuelewa then nitakijibu vizuri zaidi.
 
Yes and No.....

Kuna ambao wanaweza kufikiri kwamba CHADEMA walikosea na kuna ambao wataona tofauti.....Hilo lipo na litaendelea kuwepo regardless ya matokeo ya uchaguzi.....Kwa mfano mimi ni kati ya watu waliopinga sana Lowassa kuja CHADEMA na niliamini mwanzoni kwamba walikosea lakini sasa naamini viongozi wangu walikuwa sahihi.....

Ninachokisema hapa ni kwamba, hilo limeshapita ! Kwa maana kwamba uamuzi huo hauwezi kuwa reversed....Na kilichoko mbele yetu ni uchaguzi na inabidi tuamue kati ya UKAWA with Lowassa OR CCM with Magufuli !......Kuendelea kujadili uamuzi ambao hatuna uwezo wa kuubadili ni kupoteza muda. Na ndio maana nasema mjadala utakuwa na maana kama hatimaye utatuongoza kusema option gani ni bora.....
Mimi naamini conscious yako ambayo huegemea ukweli ndiyo iliyokufanya uone mwanzoni kuwa Chadema walikosea. Na nina hakika kwenye uzi huu nimegusa sababu zilizokufanya uone Chadema wamekosea. Kuhusu swali lako kutaka maoni kwamba kati ya wagombea waliopo nani anafaa, nakwambia kuwa I rule out wagombea wa vyama vingine ikiwemo chama cha wasaliti ACT. Uwezekano wa kupigiwa kura kwa mgombea wa urais wa Chadema na UKAWA, kutategemea ni kwa kiasi gani Chadema wanarudi kwenye misingi yao ya kupinga ufisadi. Na ikiwezekana watutangazie kuanzia sasa baraza la mawaziri litakuwaje na litajumuisha akina nani na kwa nafasi zipi ili tujue kuwa baraza hilo la mawaziri linaakisi kurudi kwa Chadema kwenye misingi ya kupinga ufisadi. Kinyume na hapo sioni tofauti ya kimsimamo katika suala la ufisadi kati ya CCM na Chadema. Na it is even worse kwa Chadema walioacha kusimamia matumaini ya wananchi ya kutokomeza ufisadi na kukumbatia sera ya kulinda na kutetea ufisadi. Kama nilivyosema awali hali ilivyo sasa kwa kuzingatia hoja yangu ya kwanza kuhusu uwezo alionao Lowasa wa kubadiisha mfumo kama viongozi wa Chadema wanavyomwonyesha, tayari mfumo wa Chadema umebadilika. Lowassa kisha ubadilisha mfumo wa Chadema kutoka ule wa kupinga ufisadi kwenda mfumo ule unaolinda na kutetea ufisadi.
 
nazani mkeo amelala nje kwa hasira ukaja kuwachosha ukawa. hii stori ungepeleka kijiwe cha kahawa tu,
Nadhani ulichoandika ndicho kinachpositahili kupelekwa huko ulikosema. Wewe leta hoja, matusi ya nini?
 
Lengo la uzi huu ni kuchambua kwa makini hoja zinazotolewa kutetea uamuzi wa Chadema na UKAWA wa kumkaribisha na kumjumuisha Lowassa katika ushirikiano wao.

Lowassa atasaidia kubadili mfumo mbovu wa CCM

Hii ndiyo hoja kuu inayotumiwa na CHADEMA na UKAWA kutetea ujio wa Lowassa. Lowassa anaonekana kama kiongozi mwenye uwezo mkubwa wa kusaidia kubadilisha mfumo mbovu ulioasisiwa na CCM. Hoja hii inatolewa na wengi akiwemo Mbowe. Ngoja tukubali kwa sasa hoja hii kuwa ni kweli.

Tukikubali hoja hii, lazima tukubali kuwa Lowassa pia ana uwezo wa kubadili mfumo wa Chadema kadiri anavyopenda, na hapa ndipo shida ilipo. Miaka ya nyuma Chadema walishamweka Lowassa katika list ya ufisadi. Ikiwa Lowassa kweli ni fisadi kama ambavyo Chadema walivyowaaminisha wananchi, inamaana pia anauwezo wa kubadili mfumo wa Chadema na kuweka mfumo wa kutetea, kulinda na kuendeleza ufisadi.

Lowassa anatumiwa tu na Chadema na UKAWA kubadili mfumo mbovu wa CCM
Hoja hii inayotolewa na Chadema na UKAWA (mfano Mh. Msigwa). Wanasema hata kama Lowassa kweli ni fisadi, anatumika tu kusaidia kuondoa mfumo mbovu wa CCM. Kwamba, Lowassa baada ya kuwa rais atafuata taratibu za chama na hivyo atalazimika kuwa mtu mwema. Tatizo la hoja hii ni kwamba Lowassa si mtu wa kutumika tu halafu akubali. Lowassa amekataa kutumiwa na rais aliyepo madarakani aliyemtosa bila kumsaidia kupata urais kama na yeye alivyomsaidia kumwingiza madarakani. Kama alivyokataa kutumiwa na JK ndivyo hivyo hivyo atakavyokataa kutumiwa na Chadema na UKAWA. Hivyo matamanio yaliyomsukuma Lowassa kutaka urais lazima ayatimize na hawezi kukubali atumike tu bila kutimiza malengo yake.

Hakuna mtu aliye juu ya Chama (Chadema)

Hoja hii inatolewa mara nyingi na Mbowe. Kwa juu juu inaonekana kuwa na mashiko. Lakini ikiichunguza kwa makini baada ya ujio wa Lowassa inaonekana kuongelewa kwa hila kwa sababu kuna mwanachama Lowassa anayeonekana kuwa nguvu kubwa kiasi cha kuwa na uwezo wa kubadilisha mfumo. Kwa matendo, Chadema wanamchukulia Lowassa, kumjenga na kuonekana kama mwenye nguvu za kuwa juu ya chama, maana anauwezo hata wa kubadilisha system.

Lowassa aliwekwa kwenye list of shame kupata political points
Hoja hii imetolewa pia na Chadema, mfano Msigwa. Je tuamini kuwa Chadema walimweka Lowassa kwenye list of shame ili tu kupata political points. Hapana, hii ngumu kuamini. Chadema walimtuhumu Lowassa hadharani tena kwa kutoa ushahidi. Sasa leo wanataka kutuaminisha kuwa Lowassa hakustahili kuitwa na Chadema kuwa ni fisadi. Ikiwa Chadema walimsingizia Lowassa kuwa ni fisadi, ni kwa vipi sasa tuwaamini kwa lolote lingine wanalotuambia majukwaani? Kwa nini tusiamini kuwa chochote wanachotuambia baada ya hapo ni kwa ajili ya kupata political points tu na hakuna ukweli wowote?

Lowassa hana hatia ya ufisadi hadi ithibitishwe mahakamani
Hoja hii inatolewa na Chadema na UKAWA kuonyesha usafi wa Lowassa. Kwa mfano mchugaji Msigwa ametumia hoja hii. Swali la kuuliza, je tuamini kuwa mahakama ndiyo kigezo cha ukweli, really? Chadema na UKAWA akiwemo mchungaji Msingwa wanaamini kabisa kuwa mahakama ndiyo kipimo cha ukweli?

Mara ngapi vyama vya upinzani vimelaumu mahakama kutumiwa na serikali. Ripoti mbalimbali zinaonyesha mahakama ni moja ya taasisi zinazoongoza kwa rushwa. Katika mazingira haya ni kwa vipi tuamini kuwa mahakama ndiyo kipimo cha ukweli na haki? Katika nchi zinazoendelea ikiwemo zile zilizopo barani Afrika, serikali ziliyopo madarakani zinatumia taasisi zake kama mahakama kutetea kuwakandamiza wananchi wake.
Kama mahakama ndiyo kipimo cha ukweli kwa nini Lowassa anapata mashaka juu ya kifungo cha Babu Seya hata kusema atatumia utawala bora kumtoa gerezani?

Hii inaonyesha maamuzi ya mahakama kuingiliwa na watawala. Ndiyo maana hoja ya kusema mahakama ndiyo kipimo cha ukweli juu ya tuhuma za Chadema za ufisadi kwa Lowassa haina mashiko. Kwani, wakati wanatoa tuhuma hizo na kuaminisha wananchi kuwa Lowassa ni fisadi mahakama wanazodai ndizo zinazoweza kuthibitisha ukweli wa tuhuma hazikuwepo? Kwa nini Chadema hawakusubiri Mahakama imhukumu Lowassa kuhusu ufisadi wake ndio waseme ni fisadi?

Asiye na dhambi na awe mtu wa kwanza kumsema Lowassa ni fisadi

Hii ni hoja inayopingana sana na kitendo cha Chadema kumweka Lowassa kwenye list of shame. Hivi Chadema na UKAWA mfano mchungaji Msigwa, hawakujua andiko hilo la kwenye Biblia wakati wanamtuhumu Lowassa kuwa ni fisadi? Kwa hakika kati ya vitu vinavyosumbua fikra za watu kwa sasa na kuwasononesha wanamageuzi wa kweli ni mgongano kati ya tuhuma zilizotolewa na Chadema juu ya uhusika wa Lowassa katika kashfa ya Richmond, na uamuzi wa sasa wa Chadema na UKAWA kumsafisha kuwa siyo fisadi.

Mwisho

Chadema wamefanya kosa kubwa la kukana misingi yake. Wamevunja mioyo ya watu wengi hata kama hawasemi na wamemomonyoa trust ambayo wananchi wengi waliwapatia kama mkombozi wao wa kutokomeza ufisadi. Chadema inahitaji kuzaliwa upya, na irudi kwenye misingi yake. Chadema ilisheheni wachapakazi- Msigwa, Mnyika, Tundu Lissu, Lema, Slaa, Mbowe, Mdee n.k. Hawakuhitaji mtu anayezimua harakati sahihi za kuikomboa nchi yetu dhidi ya ufisadi ulioota mizizi. Chadema ilijitosheleza kimikakati na kwa raslimali watu.

Ndugu mtoa mada!nadhani kuja kwa Lowasa ukawa ni sahihi.mpaka sasaiv lengo kubwa la mabadiliko tunayotaka sio tu lowasa kuwa rais bali tunataka mfumo mzima wa serikali kubadilika,Leo hii incase magufuri akiwa rais mfumo uleule wa ccm na mawaziri na manaibu na makatibu wakuu na wakurugenz wote watabaki walewale,hawa ndo tunataka wabadilike na kuja nguvu mpya za kufanya mabadiriko.kwn hawa ndo wezi wakubwa wa rasilimali za nchi hii.kwn sasaivi Tanzania imekuwa kama ya ukoo na watu wanachuma tu as if mali hazina mwenyewe,Baba anakuwa ni waziri na mtoto anakuwa ni katibu au mbunge au mkurugenzi hizi zote ni nyadhifa kubwa za kupiga hela za watanzania,But iwapo atachaguliwa Lowasa naamini mfumo mzima wa kiutendaji serikalini utachange for the the better means mawaziri,manaibu,wakurugenz na wengine wengi watakuwa wapya na wenye mwamko mpya kwa masilahi ya taifa hili.Kwetu sisi wa hali ya chini hatuitaji Rais aweje kwn hatukutaani nae hata siku moja kwenye maisha yetu ya kila siku bali tunakutana na hawa walio chini yake ambao kwa mfumo wa ccm ulivyo sasaivi naweza kusema wote "wameoza"mtu amekaa ktk uwaziri 30yrs hata akili ya kufikilia maendeleo ya nchi hana tena kichwani.Nashangaaa kwnn ccm inaogopa sana ukawa kwa kigezo kuwa watu wanataka madaraka!wao mbona wapo madarakani 50yrs lakini hawataki kuachia viti vyao hivyo?its time Ccm wakae pembeni iingie timu mpya then next election waje upya.
 
Mtoa mada wewe ni shujaa wa hoja. Umedadavua hakuna tena. Asiyeelewa haya basi ataelewa siku ya mwisho wa dunia. Umedadavua kwa kutumia kona ingine kabisa ambayo haijawahi kuguswa. Hakikisha hoja hii inawafikia hata wasioweza kusoma jf. Uko juu.

jamb kaongea ukweli kabisa, ila kwasababu watz wengi wanajudge mambo kishabiki hawataliona hilo.
 
Hizi hoja kwa sasa hazitakiwi kwenye hili jukwaa!

Uliokuwa unaitwa ujinga na upumbavu katika jukwaa hili kwa sasa unaitwa werevu na hekima!

WanaJf wengi wenye hekima na busara kwa sasa wako kimya kutokana na kuhifadhi heshima zitokanazo na fikra na mitazamo yao.

Ninakushukuru kwa hoja zako lakini ninakuhurumia kwa sababu haziwezi kupata hoja mbadala.

CCM ni mbovu lakini CHADEMA/UKAWA itakuwa ni mbovu zaidi ya CCM.
 
Mkuu naomba nitoe pia la ziada katika kipengele cha Chadema kumtumia Lowassa kutoa mfumo mbovu. Si tu kwamba Lowassa ni vigumu kutumika, bali ni kuwa Lowassa na team yake WANAWADHARAU Chadema na kiukweli wanawaona si kitu. Hao akina Mdee wanaojipendekeza kwa Mama Regina na akina Msigwa kwa Lowassa bahati mbaya hawasikii team Lowassa na akina Lowassa wenyewe wanavyowadhihaki na kuwacheka wakiwa wenyewe.
Wakitaka waje wabishe. Na hata hii ya kumshambulia Dr Slaa ni kujipendekeza kwa Lissu ila team Lowassa imechochea na kukoleza mashumbulizi haya ya aibu. Wanamchukia sana Dr Slaa na wanafurahi kutumia watu wake kumtukana.
Kwa mantiki hii siyo Chadema inamtumia Lowassa bali Lowassa inawatumia Chadema na wao kama wajakazi wanamtii Bwana wao mpya.
 
Ndugu mtoa mada!nadhani kuja kwa Lowasa ukawa ni sahihi.mpaka sasaiv lengo kubwa la mabadiliko tunayotaka sio tu lowasa kuwa rais bali tunataka mfumo mzima wa serikali kubadilika,Leo hii incase magufuri akiwa rais mfumo uleule wa ccm na mawaziri na manaibu na makatibu wakuu na wakurugenz wote watabaki walewale,hawa ndo tunataka wabadilike na kuja nguvu mpya za kufanya mabadiriko.kwn hawa ndo wezi wakubwa wa rasilimali za nchi hii.kwn sasaivi Tanzania imekuwa kama ya ukoo na watu wanachuma tu as if mali hazina mwenyewe,Baba anakuwa ni waziri na mtoto anakuwa ni katibu au mbunge au mkurugenzi hizi zote ni nyadhifa kubwa za kupiga hela za watanzania,But iwapo atachaguliwa Lowasa naamini mfumo mzima wa kiutendaji serikalini utachange for the the better means mawaziri,manaibu,wakurugenz na wengine wengi watakuwa wapya na wenye mwamko mpya kwa masilahi ya taifa hili.Kwetu sisi wa hali ya chini hatuitaji Rais aweje kwn hatukutaani nae hata siku moja kwenye maisha yetu ya kila siku bali tunakutana na hawa walio chini yake ambao kwa mfumo wa ccm ulivyo sasaivi naweza kusema wote "wameoza"mtu amekaa ktk uwaziri 30yrs hata akili ya kufikilia maendeleo ya nchi hana tena kichwani.Nashangaaa kwnn ccm inaogopa sana ukawa kwa kigezo kuwa watu wanataka madaraka!wao mbona wapo madarakani 50yrs lakini hawataki kuachia viti vyao hivyo?its time Ccm wakae pembeni iingie timu mpya then next election waje upya.

Huwa ninapata shida sana ninapokutana na hoja ya aina hii juu ya dhana nzima ya mabadiliko. Kwa akili zako zote umewaza na kuwazua kuwa mabadiliko ya watu yanawezekana? Je huyo Lowasa atawatoa wapi Watendaji wasafi baada ya kuwatoa hao unaowasema? Kwa nini tusikuhukumu kuwa pengine hao Makatibu na Wakurugenzi unaowasema unawaona kuwa ni mafisadi kwa kuwa tu sio Wachaga?
 
At least umeonyesha msimamo wako, kwani hicho ndio cha muhimu kwa sasa na mengine yote yaliyopita ni history.......Mtu yeyote mwenye uelewa wa kawaida na anayefuatilia siasa za Tz anajua ni either UKAWA or CCM, hao wengine wote wanasindikiza tu...Ukiwapigia kura hao, kwa kiasi kikubwa utakuwa umeipoteza tu kura yako...

Ninaamini UKAWA with Lowassa ni far far far better ukicompare na CCM na ndio hao nitawachagua na ninaamini wengi watawachagua hao. Hayo masharti unayoweka unajua kabisa hayawezi kutimizwa. Vyama havipangi baraza la mawaziri kabla ya kuchaguliwa. Hawawezi kujua wabunge gani watachaguliwa ili uwaweke kwenye baraza lako kwa sasa na vile vile huwezi jua chama gani kitapata wabunge wengi ili kiweze kutoa waziri mkuu. Katika mazingira hayo utapangaje baraza la mawaziri ?

Huwezi kupata kitu kilicho perfect na ndio maana ya uchaguzi i.e. unachagua kile kinachofaa kati ya options zilizopo. Chukulia kama vifurushi vya muda wa maongezi vile, huwezi ku-modify hivyo vifurushi, inabidi uangalie kile kinachokufaa na ofcourse huwezi kususa kwani wewe ndio una-uhitaji. Vifurushi vilivyopo ni UKAWA with Lowassa and CCM with Magufuli na hakuna chochote unachoweza kufanya zaidi ya kuchagua kati ya hivyo vifurushi viwili......UKAWA walijua kwa kumchukua Lowassa kuna watu watawapoteza na hata Mbowe aliliweka wazi hilo mapema tu lakini ukipima Loss na Faida ile net inakuwa faida tena kubwa tu......Hata mimi ilinichukua kama siku mbili hivi kuadjust na kuelewa, rafiki zangu wawili iliwachukua kama week hivi kuwa onboard, mke wangu ambaye moral values zake ziko juu sana, imemchukua mwezi kwani ni juzi tu amekubali kumpigia kura Lowassa.....

By the way hao wote, bado walikuwa na CHADEMA/UKAWA kwa upande wa Ubunge na Udiwani, kwa hiyo sio kwamba waliiacha CHADEMA moja kwa moja......Na sasa wamerudi tena kwa upande wa Urais, najua na wengine wengi tu baada ya kueleweshwa....kama Mbowe alivyosema tunawaombea Mungu awasaidie waelewe.....wameelewa na wengine wengi wanazidi kuelewa......

Ninaamini tunauwezo wa kuiondoa CCM mwaka huu na wengi wetu tumeamua tufanye hivyo kupitia CHADEMA/UKAWA....

Back
Top Bottom