Internet ya kumwaga Kenya, tena ya bei nafuu

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,759
48,407
Ushindani mkali umeibuka baina ya makampuni ya mitandao hapa Kenya, binafsi natumia ZUKU ambayo inanipa internet bila kikomo, yaani hamna kuhesabu MB, natazama movies series na kila nikitakacho ikiwemo kazi zangu ambazo hutumia internet sana yote hii kwa shilingi za Kenya 1,500Ksh au Tshs 35,000 kwa mwezi
Internet yenyewe ipo kwenye router ya WIFI, nimewapa wote ruksa kuunga.

Leo Safaricom wamekuja ya offer yao, bei kama hii ya ZUKU, ila mwezi wa kwanza utumie utakavyo hutalipa hata shilingi.
Jameni hii tosha sasa, waanze kupeleka kwa mataifa majirani haswa ambao huhesabiwa internet kwa MBs. Unakuta kila wakati unaangalia angala salio la MBs kabla kufungua video ya Youtube, hapa kwetu familia wanashinda kwenye Youtube, wanapitia pia online classes za videos, makatuni ya kumwaga.

internet_charges.jpg
 
Watu wakutumia bundles..yani hku uko youtube lkn waogopa mbs zako zisiishe...uzamani kwel
 
Wewe ni Mtz au Mkenya, kwani kiswahili chako kimenyooka kama Mtz.

Unasema familia yako wanashinda kwenye youtube, kwa kiswahili cha kenya hapo ungesema; familia yako wanashinda kwa youtube.🤣🤣
 
Ndio maana wakenya mnaangalia sana Pono sababu mko na ulimbukeni wa vitu vidogo,
Halafu We jamaa kazi gani unafanya na Internet wakati wewe ni Dereva wa Fuso?
Wacha dharau. Wewe nawe unaosha choo na unatusumbua hapa.
 
Wewe ni Mtz au Mkenya, kwani kiswahili chako kimenyooka kama Mtz.

Unasema familia yako wanashinda kwenye youtube, kwa kiswahili cha kenya hapo ungesema; familia yako wanashinda kwa youtube.🤣🤣
Kwani umeshafahamu tofauti kati ya kiswahili cha Ke na Tz? Basi tueleze kwa undani tofauti hizo.
 
Kwani umeshafahamu tofauti kati ya kiswahili cha Ke na Tz? Basi tueleze kwa undani tofauti hizo.

Watz;-- " tenga chakula mezani". Wakenya; -" weka chakula kwa meza"

Watz;--"Wapangaji wamegoma kutoka ndani ya nyumba".
Wakenya;---"Wapangaji wamedinda kutoka kwa nyumba".

Hiyo ni mifano michache tu ya sentensi za kiswahili ambazo kwazo kwa kutamka unaweza kumtambua Mtz na Mkenya, pia lafudhi ni tofauti.
 
Hilo halina utofauti wowote Kwanza neno dinda linatumika Sana kisheng Wala sio kila mtu analitumia,pili Kuna aina nyingi za sentensi.labda kile ungesema kinatofautisha ni lafudhi.
Watz;-- " tenga chakula mezani". Wakenya; -" weka chakula kwa meza"

Watz;--"Wapangaji wamegoma kutoka ndani ya nyumba".
Wakenya;---"Wapangaji wamedinda kutoka kwa nyumba".

Hiyo ni mifano michache tu ya sentensi za kiswahili ambazo kwazo kwa kutamka unaweza kumtambua Mtz na Mkenya, pia lafudhi ni tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tenga chakura mezani ni ya akina nani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
labda kile ungesema kinatofautisha ni lafudhi.

Katika hiyo Sentensi yako, Mtz angeandika hivi; "labda useme kinachotofautisha ni lafudhi.

Pamoja na utofauti wa lafudhi lakini pia huwezi kupinga utofauti wa matumizi ya maneno na uundaji wa sentensi kwa watz na Wakenya.
 
Back
Top Bottom