Internet cafe business | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Internet cafe business

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by stringerbell, Apr 19, 2010.

 1. stringerbell

  stringerbell Member

  #1
  Apr 19, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakuu nataka kuanzisha internet cafe hapo bongo mimi nipo state nataka kujua kawaida how much do you charge per hour this days ?na internet provider fee yao ni kiasi gani kwa mwezi.thanks
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Apr 19, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Sehemu nyingi ni shilingi 1000 kwa saa moja ila hii ni kwa nje ya jiji , kati kati ya mji ni alfu 1500 kwa saa moja kwingine ni 1000 kwa Nusu saa inategemea na maeneo kwa sasa biashara ya net inalipa kwa kiasi kikubwa unatakiwa utafute location nzuri tu , uwe na wafanyakazi wazuri na pia komputa nzuri matatizo ya connection ya internet sio ishu siku hizi ni wewe tu
   
 3. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kama alivyotangulia kusema mwenzangu, gharama kwa nusu saa ni kuanzia 500 - 1000. Ingawa sehemu nyingin nilizoziona mimi ni 1000 kwa nusu saa.

  Saa moja huwa 1500 - 2000. Ila 2000 ni nadra sana.

  Kuhusu gharama za internet providers, bei hazitofautiani sana. Internet cafe nyingi maeneo ya kwetu wanatumia TTCL, ila WIA na Zantel nao ni wazuri pia.

  Kwa WIA na Zantel sifahamu gharama zao, ila TTCL fuata hiyo link hapo chini:

  TTCL Bandwidth Prices
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Mh kwa saa siku hizi ni kutoka Tsh 1500 hadi 2000 kwa saa na pia ukitumia laptop wengi wanakucharge mara mbili ya bei ya kutumia compu zao,

  Kwa uzoefu wangu ukitaka biashara iende vizuri kwanza tafuta wahudumu wanojua kazi na wawe wastaarabu,kingine uifanye intaneti yako iwe na huduma za ziada kama vile printing ,photocopy na ki stationary kwa mbali pia angalia eneo lililo na mkusanyiko wa watu wengi,mimi naona kama plae Mlimani City panafaa ila tatizo ni rent zao ambazo zitakufanya ucharge zaidi,

  Lakini wahenga walisema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza ,ukiwa na huduma nzuri utapata wateja wengi,kingine pia uruhusu na uweke eneo la watumiaji wa laptop iwe wire less au hata wakiwa wanatumia cable,hapa bongo watu wengi siku hizi wanatumia laptop zao,na cha zaidi provider awe net yenye speed yaani kuwa na uwezo wa kudownload na ku upload files mbalimbali.

  Kwa mfano pale Makumbusho kuna internate cafe karibu na Steers inafurika watu kwani ukiiingia hapo unapata huduma zote ,unaweza kutumia laptop yako ,unaweza kudownload files, sehemu zingine hawarusu kudownload mafaili.
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Apr 19, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hata hivyo WIA Wamekuwa sio wazuri sana wa Huduma kwa wateja pamoja na TTCL kuna mtu alipata tatizo walikaa karibu siku 3 kutatua tatizo lake kwa wale wa SASATEL nao watu wao wa IT hawana uelewa mpana wa Bidhaa zao wanazouza za internet kiasi kwamba wengi wanashinda hata kuinstall modem za internet kwa wateja
   
 6. n

  ndekia1 Member

  #6
  Apr 19, 2010
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa Hour ni Tsh1500/=
   
 7. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Me nadhani kwa kuanza, ungeanzisha wireless hotspot. Watu wengi wana laptop hapa bongo. Kwa pale mlimani city kuanzisha internet cafe, unabidi ujiandae na renting fee ambayo ni ya kufa mtu.

  Ila, unaweza ukapata sehemu karibu na mlimani city, then ukatafuta wireless device ambayo ni powerful inayoweza ku beam hadi pale mlimani city. Wireless network yako isiwe na security, ili kila mtu aweze ku connect.

  Ila after connection, they get a message on how to pay to get a service. This is easy to do na kuna software zinasupport. Alafu, wewe unatengeneza voucher cards zenye activation code zinazoweza kumpa mtu muda wa saa 1 2, 3 kutokana na mahitaji. Ongea na watu wa pale restaurants wakuuzie hizo vouchers kwa commission flani.

  Kama upo US, kupata powerful wireless devide its easy. I know how to assemble equipments that ca beam up to 10 - 15 km distance. So ukiwa pale karibu na mlimani city, unaweza uka beam mpaka ubungo bila wasi wasi. It will roughly cost around 300 - 400 bucks.
   
 8. stringerbell

  stringerbell Member

  #8
  Apr 19, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa kiasi gani renting fee pale mlimani ?kwakweli bei nzuri tuu kwa saa mimi nitachaji kwa saa 1000 na natarajia kuweka 20 pc.kuna jambo tu ambalo nimekuwa disapointed nasikia internet provider bado wanatumia sattelite connection na vile vile bei yake ni kubwa mno kwa unlimited .ukitizama huku nje sasa hivi internet provider wanatumia fibre optic connection which is very fast .na bei kwa mwezi ni kama $40 per month the speed you get is 50mb and is unlimited.nilijaribu kuuliza bei kwa kampuni inayoitwa zanzilink kwakweli bei yao kwa unlimited imenikatisha tamaa .530 dollar per month.hatari tupu
   
 9. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 765
  Likes Received: 550
  Trophy Points: 180
  Mkuu,

  Hisabati inayoweza kuumiza kichwa ni kwamba watoa huduma wengi kama TTCL wanatoza viwango kwa kiasi cha data (Megabytes per month, etc.) wakati wewe mwenye mgahawa unategemewa utoze wateja wako kwa masaa.

  Kwa hiyo kinadharia, kama mtandao una kasi kubwa sana wateja watatu wanaweza ku download movie tatu ndani ya masaa matatu, gigabyte 12 hizo, halafu wakakupa shilingi ngapi, 500/= X watu 3 X masaa 3, shilingi 4500!

  Unajua gigabyte 12 Tanzania zinauzwa kiasi gani na hawa kina TTCL, niamini, sio 4500/=.

  Unafanyaje? Unafunga software ya kupunguza makali ya kasi ya mtandao kwa wateja wako, kichekesho. Mteja anakaa nusu saa anasubiri barua pepe moja ifunguke. Kama ni mteja mwenye ufahamu, kama hawa watumia "hotspot" ataona kwa nini asende kununua vocha ya Zantel akatumie nyumbani kwa mda wake?

   
 10. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #10
  Apr 19, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu wako watu wengi wanaofanya biashara za internet na zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa wanalipa bei hizo hizo kubwa sema kuna mambo ya kitaalamu unatakiwa kuangalia sana na kufuatilia kwa karibu haswa kwenye komputa zako bila mteja wako kuhangaika anapotaka vitu vingi unajua kwa mfano wengi hawana huduma za hapo kwa hapo kama miziki and so on unakuta mwingine amekuja kwa mfano kuangalia au kutafuta miziki ya kisasa kwanini usidownload usiwe nayo kwenye server mtu akitaka apewe na sio kudonwload ? hiyo ni moja kuna mengi na mengi sana ya kufanya kuvutia wateja

  Kuna internet cafe moja mitaa ya mwenge inafunguliwa masaa 24 hata kama mtandao umekatika watu wamejaa uliza wanajalia nini jamaa ameshajua wanataka nini
   
 11. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 765
  Likes Received: 550
  Trophy Points: 180

  Duu, Yona Maro karejea.

  Wasioaga hawarudi, wanaoaga wanarudi...!
   
 12. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Twambie basi wanajalia nini na hiyo cafe hapo mwenge inaitwaje nasi tukapate darasa ndugu
   
 13. stringerbell

  stringerbell Member

  #13
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu
  kwa kununua data ni maumivu ya kichwa ,bora uchukua unlimited ambayo itakuwezesha wateja kuwapa fursa ya kudowload anything they want music,movie,games .na vile vile kuangalia programs mbali mbali online ,hata matumizi ya skype vile vile .kwakweli hawa maprovider wanawakamua watu vibaya sana .mimi hapa home nina unlimited na dowload speed ni 24meg .na ninalipa only $15 per month.kwakweli bongo maisha magumu watu masikini then this peoples come up with pathetic price it is ridiculous.
   
 14. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  kwa biashara ya internet cafe peke yake, pale mlimani city haiwezi kulipa. Labda uwe na watu wengi saana. Unlimited ipo slow sana hapa bongo, na hii ni sababu ya kibiashara zaidi.

  Kwa bongo, Zantel and TTCL tayari wame connect na fiber, so internet zao zina speed ya kuridhisha. Kwa TZ, itachukua muda kuacha kabisa fiber, kwa sababu makampuni mengi (almost yote) yalikuwa tayari na mikataba na setelite providers so we have to wait until such contracts expire.
   
 15. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu wewe uko majuu.njoo na wazo kubwa zaidi la kibiashara.haya mambo ya internate cafe waachie wabongo wa hapa hapa ambao.kwanini kila mtu aige biashara, kwani nini usifikirie wazo jipya mkuu. Una maarifa mengi basi yatumie sio kuiga tu.yaani kila mtu auze maandazi kisa kamuona fulani anawateja kiasi.mi sipendi biashara za kuiga iga kwa hazina faida zaidi ni kukudumaza tu.Please njoo na wazo jipya.asante
   
 16. 1

  1975 Senior Member

  #16
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bei ni tofauti kwa kila internate cafe wengine wanacharge shilingi 1000 kwa saa,wengine 1500 kwa saa na zipo pia chache shilingi 2000 kwa saa.Bei hizo zinatofautiana na sehemu ilipo office,uwepo wa wateja na kama unavyojua wateja wanaangalia vitu kama speed (Mbps,kbps),ufikaji wa eneo,upatikanaji wa huduma nyingine kama Printer,Fax,Telephone na kadhalika.Nakushauri ufanye reseach ya kutosha kwa kuangalia mambo yaliotajwa hapo juu,kumbuka vilevile kwa sasa bongo watu wengi wanalaptop na pia utakanaji internet modem ,simu zinazosuport internet(CDMA,GPRS,DWCDMA,WIMAX,) imekuwa rahisi mno.
   
 17. stringerbell

  stringerbell Member

  #17
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo biashara ya internet cafe mimi nataka kuwapa watu employment ,ni kwa ajili ya bro wangu .huku niliko tayari nina kazi zangu kwahiyo siwezi kuziacha kwa ajili kuja bongo kuendesha internet cafe .once evething is running smooth then I will leave it to them .
   
 18. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #18
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hah hah hah, Yona una ubia nini na hawa jamaa? jamaa speed yao ya internet ni slow sana ila wanawavutia wateja wao kwa kuwaeke Porn movies na music kwenye chumba maalumu ambacho kila computer imetenganishwa na pazia. Iko hapa Mwenge bara bara ya Africasana inatizamana na msikiti mmoja hivi.Hivi wewe I.T spesholist unawashawishi watu kwenda kwenye cafe kama ile ambayo imejaa ma-virus? isitoshe Huwezi kuchukua movie/music kwenye computer zao wame disable USB port zote.
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Usisahau kutuwekea huduma muhimu kama soda ,,maji ...na iwe classic
   
 20. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Well said mkuu. Big up!
   
Loading...