International Friendly Match: Simba SC Vs Bandari FC, burudani ya pekee Uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Katika kuendelea kujiweka sawa na patashika ya Vodacom Premier League VPL, Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 watakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Bandari FC kutoka nchini Kenya.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika tisini, utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa 10:00 jioni, huku Kocha wa Simba SC, Patrick Aussems akisema kikosi chake kimejiandaa vilivyo kucheza na timu nzuri.

"Tumejiandaa na mchezo tukijua tunaenda kucheza na timu nzuri. Utakuwa mchezo nzuri kwa wachezaji kuendelea kuwa fiti na kwetu kama timu kujipima", amesema Kocha Aussems.

•••Wanasimba na wadau wa kandanda karibuni kushuhudia burudani ya pekee yenye viwango vya CAF pamoja na ushindi Uwanja wa Taifa..NguvuMoja
IMG_20191012_120117_512.jpeg
IMG_20191012_120135_678.jpeg
 
Kwanini asingempa nafasi Rashid juma kwenye match Kama hii kuanza kwenye first eleven dogo anajua Sana maana msimu Huu tokea uanze hajacheza hata mechi moja lasivo huyu dogo kipaji chake kitapotea.
 
Baada ya kuwa nje kutokana na majeraha, Bull Striker Wilker Henrique Da Silva, wa Simba SC kutoka Brazil, anaongoza mashambulizi kwa kuanza dhidi Bandari FC
 
Huyo bwana mdogo Salum Shaban anapiga mpira mkubwa sana hasa akicheza midfield ya juu.
Naona tuna Mkude mwingine anaibuka sijajua Abdul Selemani kapotelea wapi
Katika kuendelea kujiweka sawa na patashika ya Vodacom Premier League VPL, Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, leo Jumamosi Oktoba 12, 2019 watakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Bandari FC kutoka nchini Kenya.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika tisini, utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa 10:00 jioni, huku Kocha wa Simba SC, Patrick Aussems akisema kikosi chake kimejiandaa vilivyo kucheza na timu nzuri.

"Tumejiandaa na mchezo tukijua tunaenda kucheza na timu nzuri. Utakuwa mchezo nzuri kwa wachezaji kuendelea kuwa fiti na kwetu kama timu kujipima", amesema Kocha Aussems.

•••Wanasimba na wadau wa kandanda karibuni kushuhudia burudani ya pekee yenye viwango vya CAF pamoja na ushindi Uwanja wa Taifa..NguvuMojaView attachment 1230560View attachment 1230561
 
Simba ipo uwanjani kupasha misuli moto, tayari kuwakabili Bandari FC
FB_IMG_1570884556874.jpeg
 
Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa Taifa...!

Naaaaaaaaaaaaaaam kipute kimeanza

Simba SC 0-0 Bandari FC
 
Huyo bwana mdogo Salum Shaban anapiga mpira mkubwa sana hasa akicheza midfield ya juu.
Naona tuna Mkude mwingine anaibuka sijajua Abdul Selemani kapotelea wapi
abduli aliumia vibaya kwenye Under 20 ligi so jina lake halijajumuisha kwenye kikosi cha msimu huu
 
08' Simba wanapata kona..Inapigwaaa konaaaa..Lakini inaokolewa

Simba SC 0-0 Bandari FC
 
17' bado milango ni migumu kwenye mchezo huu wa kirafiki..! Bandari wamepata kona 2 ambazo hazikuzaa matunda

Simba wamelifikia lango la Bandari FC mara nyingi.
 
27' Ajibu anamimina krosi safi kwake Shiboub anatuliza...Wilker anapigaaaaaaa goal kick

Simba SC 0-0 Bandari FC
 
32' mpira umesimama baada ya mchezaji wa Bandari FC kupata rabsha..!

Ni free kick, kuelekea Simba..Inapigwaaa njeee..goal kick
 
40' Bandari FC wanafanya jaribio kali..Lakini golikipa Beno anapangua..!
 
45+2' kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa Taifa

Naaaaaaaaaaaaaaam mpira ni mapumziko timu zote zikitoka bila kufungana..!

Simba SC 0-0 Bandari FC
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom