Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,150
- 7,328
Kwenye mjadala huu 'serious' tutajadili kwa kina juu ya vipengele vifuatavyo kuhusu hali ya ajira kwa vijana nchini;-
1.Hali ikoje kwa sasa?
2.Matokeo ya tatizo hili la ukosefu wa ajira ni nini kwa wakati huu?
3.Tatizo hili linasababishwa na nini?
4. Hali hii ikiendelea hivyo hatari yake ni nini?
5. Nini kinachofanyika kwa sasa na kwa nini tatizo bado ni kubwa?
6. Ushauri sasa; ni nini tunaweza kufanya na ili iwe nini? na mwisho ni,
7. Faida zitakazopatikana ikiwa ushauri tunaotoa utaonekana unafaa na kupokelewa vizuri.
1.Hali ikoje kwa sasa?
2.Matokeo ya tatizo hili la ukosefu wa ajira ni nini kwa wakati huu?
3.Tatizo hili linasababishwa na nini?
4. Hali hii ikiendelea hivyo hatari yake ni nini?
5. Nini kinachofanyika kwa sasa na kwa nini tatizo bado ni kubwa?
6. Ushauri sasa; ni nini tunaweza kufanya na ili iwe nini? na mwisho ni,
7. Faida zitakazopatikana ikiwa ushauri tunaotoa utaonekana unafaa na kupokelewa vizuri.
Hali ya ajira kwa sasa hapa nchini kwetu ikoje kwa picha ya jumla?
Idadi ya vijana ambao angalau wanafika level ya chuo imeongezeka sana kwa miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, pengine zaidi ya 90% hawapati ajira kwenye sekta rasmi. Kwa mfano kuna vijana wengi tu ambao wamemaliza vyuo toka mwaka 2010 na hadi leo wanatafuta ajira na hawajapata.
Hili linafahamika vyema ndio maana tumekuwa tunasikia kauli ya ‘ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiri kulipuka’. Kwa ujumla watu wanakubalina kuwa sio tu kwamba tatizo lipo ila ni serious na lazima kifanyike kitu.
Matokeo ya tatizo hili la ukosefu wa ajira kwa sasa ni nini?
Vijana hawa wanakuwa hawawezi kuzalisha, hawawezi kujitegemea, hawachangii kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi wanakuwa ni watu waliokata tamaaa, wanaoishi wa kuombaomba, kujipendekeza, na inasemekana pia wanapoteza nguvu za kiume (jocking!). Aidha, katika hatua fulani utu na ubinadamu wao unakuwa compromised jambo ambalo linasikitisha sana.
Tatizo hili linasababishwa na nini kwa muhtasari?
Elimu zinazotolewa kwenye mifumo yote rasmi nchini zinamuandaa kijana kuajiriwa huku zikiua uwezo wake wa ubunifu. Kwa bahati mbaya ajira rasmi nazo hazipo kwa sababu kasi ya ukuaji wa sekta binafsi kwa kuzalisha wawekezaji wa ndani na kuvutia wawekezaji wa nje ni ndogo sana kuliko rate ya vijana wanaohitimu kila mwaka.
Hali ikiendelea kama ilivyo hatari yake ni nini mbele ya safari?
Pamoja na athati tajwa hapo juu, kama hatua za haraka zisipochukuliwa, tunaandaa kizazi ambacho sio tu kwamba hakitaweza kutoa mchango kwenye uchumi wa nchi bali pia hakitaweza kujikimu. Kizazi ambacho kitakuwa kimejikatia tamaa ambapo nchi inapokuwa na watu wengi waliokata tamaa na wasio na cha kupoteza ,ni hatari kubwa sana kiusalama.
Nini kinachofanyika kwa sasa na kwa nini tatizo bado ni kubwa?
1. Kutoa mikopo ya elimu ya juu; Serikali imejitahidi kweli kutoa mikopo ya elimu ya juu ili vijana wasome kweli kweli. Kwa bahati mbaya, wakimaliza ajira rasmi hamna, wanakuwa washapoteza ubunifu binafsi na mtaji hawana. Kwa hiyo hawezi kulipa mikopo.
2. Aidha, mikopo hiyo inaongezeka kwa 6% kila mwaka, kwa hiyo aliyekopa 10 M kwa mfano, baada ya miaka 15 ya kushindwa kulipa, anaweza kudaiwa karibu 30M (ambazo hataweza kulipa vile vile maana hana kazi maalum).
3. Mkazo kwenye VETA Ambapo vijana husoma ufundi. Hata hivyo kwa kuwa elimu hii nayo ina mtaala, hatimaye vijana hujikuta wakisomea mitihani na hivyo kuua uwezo wao binafsi wa ubunifu kwa kiasi fulani, hivyo hujikuta wakisubiria kuajiriwa vile vile, ajira ambazo kimsingi hazipo. Aidha, hata wale wanaobaki na ubunifu, hujikuta hawana mtaji kwa hiyo hawawezi kujiajiri na hivyo kurejea kwenye mzunguko wa tatizo.
4. Kuhimiza uwekezaji wa nje na ndani ambapo pamoja na serikali kujitahidi sana kwenye eneo hili, uwekezaji wa ndani unakuwa mgumu kwa sababu watu wengi hawana mitaji (miongoni mwa mambo mengine) na wawekezaji wa nje hawaji kwa kasi kubwa inayowezesha kutoa ajira za kutosha.
5. Kuhimiza kufanya kazi kwa kujitolea; Kuna fikra kuwa watu hawapati ajira kwa sababu hawana uzoefu kitu ambacho sio sahihi. Kutokana na fikra hiyo, vijana huhimizwa kujitolea sehemu mbalimbali, hatimaye baada ya kujitolea hujikuta hakuna la ziada kwa kuwa nafasi za kazi ni chache kuliko waliojitolea.Hatimaye huwajibika tena kuingia mtaani wakiwa hawana hili wala lile.
Kwa mantiki hiyo tunaomba kushauri sasa, kwa lengo la kuchochea mjadala na kupata mawazo mapana.
Ushauri sasa; ni nini tunaweza kufanya na ili iwe nini?
1. Elimu ya msingi iwe mpaka kidato cha nne. Lengo hapo ni kijana aweze kujua mambo ya msingi ya jumla. Katika kipindi hicho, vijana wawekewe mazingira ya kuvitambua vipaji vyao.
2. Baada ya kumaliza kidato cha nne, kuwe na mirengo mitatu;-
(a) Vijana wanaoendelea na kidato cha tano hadi vyuo. Mrengo huu usipewe kipaumbele sana maana kwanza ajira zake ni chache na pili unaandaa mameneja ambao hawatakiwi kuwa wengi. Hapa wapewe kipaumbele wale walioko ki-academics sanaaaa. Mrengo huu uchukue kama (20%) tu ya vijana wote.
(b) Mrengo wa VETA; Huu uchukue angalau (30) ya vijana kwa ajili ya kuandaa technicians, ambao nao kwa kiasi kikubwa pia watategemea kuajiriwa. Na,
(c) Mrengo wa kujiajiri ambapo kila kijana atachagua kazi anayoitaka kulingana na kipaji chake. Mrengo huu utachukua (50%) ya vijana wote waliobaki. Eneo hili ndilo linapaswa kupewa kipaumbele cha juu sana maana ndio litakalozalisha wawekezaji wa ndani ambao ndio watakaoajiri kundi (a&b hapo juu) Kwa hiyo hapa ndio tutakuwa tunatengeneza matajiri wenyewe sasa.
Hapa jukumu la serikali itakuwa ni
(i) Kutengeneza mfumo wa coaching & mentorship ambapo kila kijana atasaidiwa na coach au mentor kujipangia malengo na kuyatekeleza kwa ubunifu binafsi na pale anapokwama kupata ujuzi flani anapewa connections ya kuipata ujuzi husika (ikumbukwe sasa hivi solutions nyingi zinapatikana kwenye internet tu)
(ii) Kuwapatia mikopo vijana hawa ambayo itatumika kama mitaji ya kuanzia. Mikopo hii itapatika kutoka kwenye fungu litakalookolewa kwa wale wa elimu ya juu ambao watakuwa wamepungua. Inaweza kuongezewa kidogo kutoka kwenye vyanzo vingine kama itakavyoonekaa inafaaa.
Faida zitakazopatikana ikiwa ushauri tunaotoa utaonekana unafaa na kupokelewa vizuri.
1. Hao vijana 50% ambao watakuwa ni wawekezaji wandani watakuwa sio tu kwamba wamepata ajira bali ni matajiri chipukizi.Kwa mara ya kwanza kama taifa tutakuwa tumeanza kuzalisha matajiri wetu wenyewe kwenye batches.
2. Hii 50% ya vijana ambayo ni wawekezaji wa ndani itaajiri 30% ya technicians kutoka VETA na 20% ya mameneja ambao wameenda hadi vyuo vikuu (kama ilivyoelezwa kwenye (a&b hapo awali). Matokeo yake tatizo la ukosefu wa ajira litakuwa limeshatatuliwa kwa karibu 100%.
3. Mfumo huu utawezesha makundi yote kuweza kulipa mkopo tofauti na sasa ambapo karibu wote hawawezi kulipa maana hawana ajira.
4. Karibu vijana wote watakuwa wanaweza kuzalisha kwa ajili ya kujikumu na kujenga familia na kuishi maisha yenye heshima.
5. Karibu vijana wote watakuwa wanachangia kwenye ukuaji wa pato la taifa na kuchangamsha uchumi wa nchi kwa kiwango cha juu sana.
6. Uhalifu utashuka hadi karibu 0%