Intelijensia ya Chadema inazidi kukidhoofisha chama

Ninachojiuliza kwa hawa CHADEMA kila taarifa ya kiintelijensia ina msemaji wake? mara SLAA , mara Mnyika , mara Marando na wakati mwingine Mbowe Mwenyewe. Hizi si ni dalili za uongo na upotoshaji mkubwa?

Hii inatokana na uzito wa jambo husika,ujumbe si umefika lakini?

Au unataka useme umbo la Ndugu marandu limechangia taarifa kutopokelewa vizuri?
Stuka!
 
Ninachojiuliza kwa hawa CHADEMA kila taarifa ya kiintelijensia ina msemaji wake? mara SLAA , mara Mnyika , mara Marando na wakati mwingine Mbowe Mwenyewe. Hizi si ni dalili za uongo na upotoshaji mkubwa?
kama kiwete,nape na mkama vile.eti?
 
Watanzania wa sasa SI WAJINGA wa kuamini kila neno la mwanasiasa.
ni kweli kabisa unavyosema hatumwamini kabisa huyo mropokaji wenu mwenye domo linalotoa maneno machafu kama CHEMBA la mavi anayetumia mitambo ya mtoto wa vascodagama kutuma mesej za kusingizia anataka auwawe, MARANDO AMEBAINI NA KUTUELEZA WATANZANIA UHUNI MNAOFANYA KM MMESINGIZIWA NENDENI MAHAKAMANI mnasuasua nini?
 
Kuna madaktari wengi ilikuwaje Dr. Ulimboka mkataka kumuua....kwanini kombe mlimuua?

Hizo ndio siasa mpya za Chadema wamebakia kuwa watu wa kudandia matukio na kuyatolea matamko ya ajabu ili waendelee kusikika kwa wananchi kwamba bado wapo kwenye harakati za kisiasa.
 
Wanachofanya Chadema kinanikumbusha maneno ya Gobbles aliyekuwa Waziri wa Propaganda wa utawala wa Adolph Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia 1939-1945 alisema jambo lolote ukitaka lienee na likubalike upesi litangaze na ulikariri mara kwa mara...lakini viongozi wa Chadema wanashindwa kujua kuwa watanzania wa sasa si wajinga wa kuamini kila neno la mwanasiasa.

Hapo ndipo uchambuzi wako na ulinganisho unakuwa na mapungufu ebu soma haya ya kwako "Chadema wanashindwa kujua kuwa watanzania wa sasa si wajinga wa kuamini kila neno la mwanasiasa". Halafu jilinganishe na ukweli huu "CCM wanashindwa kujua kuwa watanzania wa sasa si wajinga wa kuamini kila neno la mwanasiasa wa chama hicho" Ndiyo maana kuna sintofahamu ya hali halisi, na kila lililokanushwa na wanasiasa wa CCM limetokea kuwa kweli. Mifano EPA, ufisadi, kujibinasia mashirika, wizi serikalini (CAG), mauaji ya kisiasa (taarifa hazijatolewa), migomo, utekaji nyara. Chama cha CCM kuchukiwa kwa sababu ni janga.

Ni kawaida kujifaragua ukiwa madarakani, lakini huwezi kuondoa ukweli kuwa serikali kupwaya ni kitu dhahiri mbele ya jamii. Ndiyo maana ya kutumia mabavu hadi kuingia kwenye mipango ya kutaka kuwauwa viongozi wanaoonekana ni tishio. Hapa hoja ni "uchunguzi"; kwa nini ungojee uchunguzi wa jambo badala ya kulibaini mapema au utuhumiwe? Jibu Serikali legelege inaongozwa na viongozi DHAIFU kwa mfumo uliofumuka, na wapiga debe tegemezi (ritz akiwemo).
 
Tumia nafasi hiyo kushangilia kimya kimya pindi unapoona mpinzani wako kaingia chaka kwakuwa intelijensia yao haikuhusu. Wala huna sababu ya kushangilia kwa kupiga kelele hadi adui mwenyewe akakusikia na mwishowe "akajirekebisha" kwa mujibu wako mwenyewe. Intelijensia ya CDM waachie waachie wenyewe na Inteligensia ya TISS (UWT) waachie wenyewe. Unless ujitambulishe wewe kuwa ndiye msemaji wa CDM na UWT.
 
Ninachojiuliza kwa hawa CHADEMA kila taarifa ya kiintelijensia ina msemaji wake? mara SLAA , mara Mnyika , mara Marando na wakati mwingine Mbowe Mwenyewe. Hizi si ni dalili za uongo na upotoshaji mkubwa?

kwa mtiririko ule ule ulioutumia niambie hao uliowataja walitoa matamko yapi juu ya mambo ya intelijensia
 
Wanachofanya Chadema kinanikumbusha maneno ya Gobbles aliyekuwa Waziri wa Propaganda wa utawala wa Adolph Hitler wakati wa vita kuu ya pili ya dunia 1939-1945 alisema jambo lolote ukitaka lienee na likubalike upesi litangaze na ulikariri mara kwa mara...lakini viongozi wa Chadema wanashindwa kujua kuwa watanzania wa sasa si wajinga wa kuamini kila neno la mwanasiasa.

hapo kwenye red, mkuu ritz naona unamuota sana mhe Godbless Lema. waziri wa propaganda wa Hitler alikuwa anaitwa Joseph Goebells na si godbless lema.
 
Shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa huwa zinafanyika katika hali ya usiri mkubwa kiasi kwamba hata mtumishi hajui mtumishi mwenzake anachunguza nini je, intelijensia ya Chadema imejuaje?
 
ritz,kitu kilichooza huwa kimeharibika,hakifai hasa kwa matumizi ya binadamu.lakini ktk tofauti za viumbe,baadhi ya viumbe hupendelea uozo,wapo viumbe wanaonufaika na kundemeka kwa uozo.Kitu kimeoza lkn funza wanakitumia na kunawiri.Wewe,ccm na serikali mkiambia mnakula uozo hamoni kwa kuwa mnenepeana.
 
Mkubwa ukishangaa hili mengine yanakuja....hii ni breaking news au old is gold, ulikuwa wapi au ndio umeshituliwa kuwa kimenuka sasa unajikosha?
 
Shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa huwa zinafanyika katika hali ya usiri mkubwa kiasi kwamba hata mtumishi hajui mtumishi mwenzake anachunguza nini je, intelijensia ya Chadema imejuaje?

Ndivyo inavyotakiwa kwa taasisi za Serikali zinazozingatia na kufanya kazi kwa uadilifu lakini kwa sasa hilo halipo ndani ya Serikali ya Tanzania
 
Watu wenye akili timamu walisawashitukia long time. Ni tabia ya wanaharakati pindi watafutapo msaada toka nchi za kigeni
 
ukikaa kimya itakusaidia zaidi, moto unaokuja mtashindwa pakujifichia, ndiyo mtajua watu tumeisha wachoka sana, utajuta kuwa kibaraka wa magamba hapo tutakuja kuidai nchi yetu. ongeeni upuuzi wenu, kwa mimi siasa si utani wa jadi ni vita kabisa maana mmejilimbikizia mali ya nchi hi ili kula na watoto wenu wala laana hii hamta ikwepa. mtalia na kusaga meno. wala siyo mbali
 
Shughuli za Idara ya Usalama wa Taifa huwa zinafanyika katika hali ya usiri mkubwa kiasi kwamba hata mtumishi hajui mtumishi mwenzake anachunguza nini je, intelijensia ya Chadema imejuaje?

KAKA
Nilikuwa sitaki kuchangia uzi huu lakini yanipasa kusema
unadhani usalama wa taifa wote wanapenda watu wao kupata tabu? unadhani usalama wa taifa hawana mioyo ya kusikia maumivu na simanzi?
usalama wa taifa ni binadamu mwenye hisia na moyo wa huruma.
 
Back
Top Bottom