Intelijensia ya CHADEMA imekufa baada ya ujio wa Lowassa

Chadema ya sasa imejaa usanii na ulaghai tu - mtu yeyote mwenye akili timamu kamwe hawezi kuwaamini!
Chama bila inteligensia yenye manufaa kwa chama haiwezi kuaminiwa na watu wenye uelewa mpana na dhamana ya kitaifa.
 
CHADEMA ya wakati wa Dkt. Slaa ilikuwa inanusa mambo mbali mbali yanayofanyika ndani na nje ya CHADEMA na kuyafanyia kazi kwa haraka kabla hayaja athiri chama.

CHADEMA ya wakati wa Dkt. Slaa sio CHADEMA hii ya leo ambayo inashindwa hata kupata intelegensia ya kinachoendelea ndani ya chama na kwa viongozi wake achilia mbali kinachoendelea nje ya chama.

CHADEMA ya wakati wa Dkt. Slaa iliweza hata kuaminiwa na baadhi ya wafanyakazi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kama Usalama wa Taifa ambao waliipa mrejesho wa kile ambacho kinaendelea serikalini huku wengine wakiipa mpaka makaratasi ya siri za serikali kwa sababu waliamini yatakisaidia chama na taifa kutokana na Uzalendo wa Mtendaji Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa.

CHADEMA ya sasa haiaminiwi tena na watu makini ambao ni wazalendo ukilinganisha na CHADEMA ya Dkt. Slaa.

Inteligensia ya sasa ya CHADEMA ilishindwa hata kunusa na kugundua kuwa Mwenyekiti wao wa BAVICHA Taifa anafanya mawasiliano na CCM mpaka pale waliposhangaa kumuona Ikulu katika kikao cha CCM-NEC.

Viongozi mbali mbali wanaojitoa ndani ya CHADEMA wanaibuka kwenye majukwaa ya CCM bila inteligensia kujua kinachoendelea.

Inteligensia haikufahamu kama Lowassa anajaribu kufanya mawasiliano na viongozi waandamizi wa serikali na CCM ili aweze kupata nafasi ya kukutana na Rais Magufuli. Walishangaa kumuona Lowassa akiongea na vyombo vya habari Ikulu baada ya kukutana na Rais Magufuli.

Kufa kwa intelegensia ya CHADEMA kumesababishwa kwa kiwango kikubwa na ujio wa Edward Lowassa na genge lake ambapo mojawapo ya tabia na sifa yake kubwa ni kujijenga binafsi huku ukiua nguzo za taasisi.

Lowassa amefanikiwa kuua nguzo za CHADEMA kwa kuweka watu wake katika nafasi ambazo niza kimkakati (strategic) na kuhakikisha wale ambao sio watu wake wanakosa nguvu za kimaamuzi. Kwa sasa Lowassa anaijua vizuri CHADEMA wakati CHADEMA haimfahamu Lowassa ahilia mbali kujua anachokifanya.

Mbinu yake ya kujijenga huku akiua nguzo za taasisi ilikiathiri sana Chama Cha Mapinduzi wakati akiwa mwanachama wa CCM. Lowassa alikuwa ni taasisi ndani ya taasisi ya CCM. Kwa maana nyingine, Lowassa alikuwa ni chama ndani ya CCM kiasi kuwa baadhi ya viongozi muhimu na wanachama wa CCM walikuwa wanaripoti kwa Lowassa badala ya kwenye vikao vya CCM.

Kilichoinusuru CCM kumezwa na Lowassa ni kwa sababu CCM ni chama dola.

Kama aliweza kuathiri nguzo za taasisi ndani ya CCM, kwa CHADEMA ambayo haina hata dola atahakikisha hata Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa anawajibika(answerable)kwake. Haishangazi kusikia wale ambao walimshambulia baada ya kukutana na Rais Magufuli wamepata karipio kali kutoka Kamati Kuu ya chama ambayo nina uhakika iko kwenye kiganja chake.

Ieleweke pia Katiba ya CHADEMA haitoi nafasi kuwa na kiongozi mkuu au maarufu zaidi ya mmoja. Umaarufu wa Lowassa ndani ya CHADEMA ni kifo kwa Kiongozi Mkuu wa CHADEMA. Kwa sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ambaye kikatiba ni kiongozi Mkuu anakuwa ndiye mpokeaji wa Lowassa katika mikutano na vikao vya chama badala ya Lowassa kumpokea Mwenyekiti.

Huyu ndiye Lowassa ambaye ni taasisi ndani ya taasisi, CHADEMA wao wanamuita eti ni ‘’tembo wa kisiasa’’.
Wewe endelea kubusu viatu vya mabosi wako hapo lumumba
 
CHADEMA ni chama Kikuu cha upinzani lakini ukichukua picha ya Katibu Mkuu na kuitembeza mitaani ukiwauliza wananchi kama wanamtambua, ninakuhakikishia ni wananchi wachache sana watakaomfahamu.
Tumieni akili muda mwingine.Dr.slaa alishawahi kuwa mbunge,Dr.slaa alikuwa anafanya mikutano ya hadhara nchi nzima kwasababu iliruhusiwa.Mashinji yupo kipindi ambacho mikutano ya hadhara wakati ambao sio wa kampeni imezuiliwa,sasa mnadhani watu wakamuone kwa mkewe?au mwadhani kila MTU ana smartphone? Acha akili za mapokeo.
 
KAMA HAINA NGUVU ILIWEZAJE KUPATA USHAHIDI WA FLASH JINSI MADIWANI WANAVYONUNULIWA? NAJUA WATU WA LUMUMBA BADO ROHO ZINAWAUMA SANA KUMUONA LOWASA BADO YUPO UPINZANI
Mimi napenda sana Lowassa aendelee kuwepo CHADEMA.

Ninasikitika sana ninaposikia baadhi ya ndugu zake wanamshinikiza astaafu siasa au arudi CCM.

Lowassa kuendelea kuwepo CHADEMA ni ushindi wa kishindo kwa CCM.
 
CHADEMA ya wakati wa Dkt. Slaa ilikuwa inanusa mambo mbali mbali yanayofanyika ndani na nje ya CHADEMA na kuyafanyia kazi kwa haraka kabla hayaja athiri chama.

CHADEMA ya wakati wa Dkt. Slaa sio CHADEMA hii ya leo ambayo inashindwa hata kupata intelegensia ya kinachoendelea ndani ya chama na kwa viongozi wake achilia mbali kinachoendelea nje ya chama.

CHADEMA ya wakati wa Dkt. Slaa iliweza hata kuaminiwa na baadhi ya wafanyakazi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama kama Usalama wa Taifa ambao waliipa mrejesho wa kile ambacho kinaendelea serikalini huku wengine wakiipa mpaka makaratasi ya siri za serikali kwa sababu waliamini yatakisaidia chama na taifa kutokana na Uzalendo wa Mtendaji Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa.

CHADEMA ya sasa haiaminiwi tena na watu makini ambao ni wazalendo ukilinganisha na CHADEMA ya Dkt. Slaa.

Inteligensia ya sasa ya CHADEMA ilishindwa hata kunusa na kugundua kuwa Mwenyekiti wao wa BAVICHA Taifa anafanya mawasiliano na CCM mpaka pale waliposhangaa kumuona Ikulu katika kikao cha CCM-NEC.

Viongozi mbali mbali wanaojitoa ndani ya CHADEMA wanaibuka kwenye majukwaa ya CCM bila inteligensia kujua kinachoendelea.

Inteligensia haikufahamu kama Lowassa anajaribu kufanya mawasiliano na viongozi waandamizi wa serikali na CCM ili aweze kupata nafasi ya kukutana na Rais Magufuli. Walishangaa kumuona Lowassa akiongea na vyombo vya habari Ikulu baada ya kukutana na Rais Magufuli.

Kufa kwa intelegensia ya CHADEMA kumesababishwa kwa kiwango kikubwa na ujio wa Edward Lowassa na genge lake ambapo mojawapo ya tabia na sifa yake kubwa ni kujijenga binafsi huku ukiua nguzo za taasisi.

Lowassa amefanikiwa kuua nguzo za CHADEMA kwa kuweka watu wake katika nafasi ambazo niza kimkakati (strategic) na kuhakikisha wale ambao sio watu wake wanakosa nguvu za kimaamuzi. Kwa sasa Lowassa anaijua vizuri CHADEMA wakati CHADEMA haimfahamu Lowassa ahilia mbali kujua anachokifanya.

Mbinu yake ya kujijenga huku akiua nguzo za taasisi ilikiathiri sana Chama Cha Mapinduzi wakati akiwa mwanachama wa CCM. Lowassa alikuwa ni taasisi ndani ya taasisi ya CCM. Kwa maana nyingine, Lowassa alikuwa ni chama ndani ya CCM kiasi kuwa baadhi ya viongozi muhimu na wanachama wa CCM walikuwa wanaripoti kwa Lowassa badala ya kwenye vikao vya CCM.

Kilichoinusuru CCM kumezwa na Lowassa ni kwa sababu CCM ni chama dola.

Kama aliweza kuathiri nguzo za taasisi ndani ya CCM, kwa CHADEMA ambayo haina hata dola atahakikisha hata Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa anawajibika(answerable)kwake. Haishangazi kusikia wale ambao walimshambulia baada ya kukutana na Rais Magufuli wamepata karipio kali kutoka Kamati Kuu ya chama ambayo nina uhakika iko kwenye kiganja chake.

Ieleweke pia Katiba ya CHADEMA haitoi nafasi kuwa na kiongozi mkuu au maarufu zaidi ya mmoja. Umaarufu wa Lowassa ndani ya CHADEMA ni kifo kwa Kiongozi Mkuu wa CHADEMA. Kwa sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ambaye kikatiba ni kiongozi Mkuu anakuwa ndiye mpokeaji wa Lowassa katika mikutano na vikao vya chama badala ya Lowassa kumpokea Mwenyekiti.

Huyu ndiye Lowassa ambaye ni taasisi ndani ya taasisi, CHADEMA wao wanamuita eti ni ‘’tembo wa kisiasa’’.
Umeongea ya maana lakini kwa hiyo chad3ma sacos ni sawa division 0 bado wanaimba tundu lusu
 
Wewe waache, intelijensia yao ikipona mpoozo wake watakuwa kama wametoka usingizini, hata hivyo it will be too late!
Yangu ni macho.

CHADEMA walimbomoa Lowassa, kwa sasa wanamjenga huku taasisi ya CHADEMA ikipukutika polepole.

Hii ni faida kwa CCM.

Naomba aendelee kuwepo CHADEMA ili andiko langu litimie.
 
Nani alikuambia suala la bombardier kushikiliwa na mahakama ni siri? Au unadhani mashauri yanayofanyika mahakamani ni siri.

Acha uvivu wa kujisomea, ingia kwenye tovuti ya mahakama ili isome mashauri yote yanayoendelea katika mahakama.

Huyo Lissu wako hakutunguliwa kwa sababu ya kusema ndege ya Tanzania inashikiliwa Canada bali ametunguliwa kwa sababu anazozijua yeye.
Si unaona mambo hayo?
Sad walahi
 
Intelijensia ya nchi imekasimiwa kanda ya maziwa makuu kiasi mkuu wa nchi haiamini anashindwa kusafiri nje ya nchi. Lakini ni sawa kwa sababu intelijesia ya nchi imehamia Lumumba na kusimamiwa na Bashite na wataalamu wa kagame.
Mkuu;
Ni bora kuwa mjinga lakini ukajua kama ni mjinga kuliko kuwa mjinga lakini hujui kama ni mjinga!
 
Kwani ni lini labda hao CHADEMA waliwahi kuwa na ' Intelijensia ' imara?
Mkuu;
Nadhani katika andiko langu sikuandika kuwa CHADEMA walikuwa na inteligensia imara.

Nimesema waliwahi kuwa na inteligensia ambayo iliweza kunusa mambo mengi na kuyafanyia kazi. Kunusa mabo mengi haina maana kuwa ni inwteligensia imara.

Kwa sasa hata kunusa hawawezi.
 
Acha porojo.... Ccm haijawahi kuwa chadema, wala chadema haitakuwa ccm.

Unaongea porojo nyiingi,kwa kuwa huijui chadema, na kwa kuwa umeshaingiza kwa post yako, basi tulia...

Ila uelewe maana ya nilichokuambia, ccm haijawahi kuwa chadema, na chadema haitakuwa ccm
Ni wapi nimesema CHADEMA imewahi kuwa CCM na CCM ni chadema?

Kumbuka kuwa katiba ya CHADEMA kwa kiwango kikubwa ni copy & paste ya Katiba ya CCM.
 
Back
Top Bottom