Intelijensia Ilivyoweza Okoa TAIFA lisiteketezwe katika Vita ya Siku 6 (Six Day War)

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
waarabu wakiwa wamesalimu amri.jpg


INTELEJENSIA ILIVYOWEZA WAOKOA WAISRAEL KATIKA VITA YA SIKU SITA (SIX DAYS WAR)


Hii ni Vita ambayo mpaka leo imekuwa mwiba mchungu kwa mataifa mengi ya kiarabu. Na kiuhalisia ni vita ambayo hawapendi kabisa kusikia ikizungumzwa au kusimuliwa.

Miaka hiyo na mpaka Mwaka 1967 Misri ikiwa taifa kubwa sana katika Ulimwengu wa Kiarabu kiuchumi na Kijeshi ,na pia ni taifa lililokuwa na watu wengi wanaokadiliwa kuwa Mil 31. Misri walikusanya majeshi yao katika Mipaka ya Israel kwa nia ya Kuwafutilia mbali kabisa Waisrael katika eneo hilo. Wakawa wameweka pia kikwazo ili waisrael wasivuke upande wa bandari ya kusini kitendo ambacho kilitafsiriwa kuwa ni uanzilishi wa vita au kitendo cha kivita(an act of war) mataifa ya Kiarabu kutokana na Mgogoro wao na Israeli walikuwa wametangaza kulifuta kabisa Taifa la Israel katika ramani. Hawakujua. Hawakujua.

NINI KILIKUWA CHANZO CHA VITA YA SIKU 6?

Hii kwa mataifa ya kiarabu hawakuwa wakiiona kama ni vita mpya walidai ni mwendelezo wa vita toka mwaka 1948 na kuendelea wakipinga kuanzishwa kwa taifa la Israel. Na baadaye pia viongozi wa Israel walikubaliana na hilo wakisema ni mwendelezo wa vita ya mwaka 1948 wakiita vita ya uhuru au INTIFADA YA PILI.

Chanzo kikubwa cha kuchochea vita na msuguano kati ya israel na matifa ya kiarabu/majirani zake ni ni uongozi wa nchi za kiarabu kukataa kutambua uwepo wa Taifa la israel na makazi yao katika nchi hiyo wanayoiita nchi ya ahadi. Na hapa waisrael nao wamekuwa wakijitahidi kuweza kuendana na changamoto za kiusalama ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kila mara kutoka kwa wapalestina na matifa mengine ya kiarabu yaliyo jirani nao.

Ukirudi nyuma mwaka 1929 wakati waarabu waliamua kuwa wanawashambulia jamii za kiisrael na kuwaua wakazi wa jamii hizo na hii ikapelekea kuwa waisrael waone kuwa jamii yao ipo katika mazingira hatari.na mwaka 1948 ikawa ni dhahiri kuwa waarabu wanataka kulifutilia mbali taifa hili la Israel.lengo lilikuwa ni kulifuta kabisa katika ramani.

Hivyo mwaka 1967 kukawa na tishio kubwa sana la kutoweshwa kwa taifa la Israel. Majeshi ya Misri, Syria na Jordan yalijiandaa kwa vita kuipiga Israel. Viongozi wa nchi za kiarabu walishatoa matamko na mitaa yote ilikuwa imejawa na kauli za kuwaogofya waisrael hawa ambao tukumbuke pia walikuwa na kumbukumbu mbaya waliyofanyiwa huko Ujerumani na Adolf Hitler. Luteni Yossi peled ambaye alikuwa ni mmoja ya waliookoka katika lile tukio la waisrael kuchomwa moto huko Ujerumani alisema” tayari tumeshaanza kufikiria katika hali ya kuwa tunatakiwa kuangamizwa” Waziri wa Ulinzi wa Israel moshe Dayan akitambua changamoto ambayo wangekumbana nayo ikiwa watashambuliwa na waarabu alisema” Mungu atusaidie katika hili ikiwa tutaanza kushambuliwa” Yitzkhak Rabin huyu alikuwa amepewa mapumziko kutokana na kupatwa na mshtuko wa kiakili na hivyo kupelekea kupewa mapumziko.
Yitzhak-Rabin-Quotes-5.jpg


Hospital za Israel zikajiandaa kuwahudumia majeruhi maana walikuwa wakifikiria silaha za kisasa ambazo Misri na Syria walikuwa nazo wakiwa wamezipata toka Urusi na kufikiria pia silaha za Kikemikali ambazo Misri ilifahamika kuzitumia wakati wa vita vyake dhidi ya Yemen.

Hali ya wasi wasi ilizidi nchini Israel na waziri mkuu wa wakti huo Levy Eshkol alisisitiza kuwa ameona mataifa mengine pia ya kiarabu yakisogeza wanajeshi wao mipakani. Na akasema kuwa ingepaswa kufanyike majadiliano ya kidiplomasia ama sivyo Israel itajiandaa kijeshi. Na hii ndiyo ilikuwa mwanzo wa vita vya siku tatu kabla Israel haijachukua Ukanda wa Gaza na Upande wa Magharib.

KUANZA KWA VITA

Kuendelea kwa hali ya waswas katika mpaka wa Israel na Syria ilikuwa ni moja ya sababu ambazo zilianzisha ghafla vita hivi. Syria waliongeza kushambulia maeneo ya makazi ya wayahudi kupitia mipakani. Israel ikazitungua Ndege sita za Syria aina ya MiG fighters. Hii ilitokea baada ya Syria kusema kuwa israel ilikuwa inaingiza majeshi yake mpakani. Misri ikawa imejipanga na kuwataka wanajeshi wa UN waondoke Israel haraka sana katika ule ukanda wa makubaliano ya kutokuwa na vita ya mwaka 1956. Ilipofika May 19 wanajeshi wa UN walianza kuondoka na siku 3 baadaye Misri ikafunga mfereji wa Tiran ambao ulikuwa unatumika na meli za Israel.

Tarehe 30 Mei. Jordan wakaingia mkataba na Misri na Syria wa Kiulinzi na mataifa mengine ya Kiarabu ikiwepo Iraq,Kuwait na Algeria nao wakatuma wanajeshi wao kuungana na mataifa mengine ya kiarabu kuwapiga waisrael. Hakika zilikuwa ni siku zenye kujaa hofu kubwa sana kwa wakazi wa Israel. Nao wakalia sana wakimwomba Mungu wao akumbuke ahadi alizokuwa amewapa miaka mingi iliyopita.

Kwa kuangalia kuwa sasa wapo mashakani na kuwa kuna vita tayari vinaanza waisrael wakaona Muunganiko mkubwa ambao hakuwa umewah kutokea kwa miaka hiyo wa nchi za Kiarabu dhidi yao.ukikumbuka bado walikuwa ni taifa changa na dogo ukilinganisha na Mataifa hayo ambayo bado hata moja moja yalikuwa na nguvu kubwa. Sasa hawa wote wameungana.

Misri walikuwa tayari wamejipanga tayari pamoja na washirika wao. Kwa vifaa vya kisasa kabisa vya kivita kukiwa an madege makubwa makubwa kutoa USSR na silaha kali sana za maangamizi kwa Taifa la Israel.

Tarehe 4 June Jeshi la Israel pasipo woga kabisa katika hali ya kuushtua ulimwengu likawa limeidhinisha kuwa tayari kupambana na Mataifa ya Kiarabu. Na hivyo wakiwa na information zote muhimu kupitia shirika lao la kijasus walikuwa Wanajua kila kinachoendelea katika nchi hizo za kiarabu na ni wapi Silaha hizo zimepangwa tayari kwa ajili ya mashambulizi.

Kipindi chote hicho mataifa haya ya kiarabu hayakuwa yakidhani kuwa Israel nayo ilikuwa imejiandaa kukabiliana nayo kwa namna yao. Hivyo waisrael wakafanya mashambulzi ya kushtukiza kuziangamiza silaha za mataifa hayo kabla hazijafyatuliwa au ndege kuanza kufanya mashambulizi nchini Israel. Ni Shambulio bora kabisa lililowahi kutokea katika ulimwengu huu wa kivita mbalo mpaka leo limekuwa ni moja ya mambo ambayo yanawaweka wenzetu katika daraja la juu sana katika mambo ya Intelejensia na usalama wa TAIFA LAO.

Mataifa ya Kiarabu yalikuwa na Silaha zenye nguvu sana na za kisasa. Israel wakapanga mashambulizi ambayo yalipiga kwa wakati mmoja Vituo vya kijenshi vya Jordan, Syria na Iraq na ndani ya siku moja Tayari ISRAEL WALIKUWA WANALITAWALA ANGA la nchi hizo zilizokuwa zimejiandaa kupambana nao.View attachment 443505

June 5 Israel ikahamishia kipigo chake ardhini wakipiga Ukanda wa gaza na kilele cha mlima Sinai ambako kulikuwa na Majeshi ya mataifa adui. Kwa kasi ya Mwanga Israel ilikuwa imepasua anga lote la Misri na maeneo ya Sinai. Wamisri walijaribu kujitutumua lakini walikuwa wamezidiwa na mipango na umakini ambao wa Israel walikuwa wamejipanga.Mpaka tarehe 8 June Wamisri walikuwa wamepigwa vibaya sana na Israel ikawa inashikiria Ukanda wa Gaza, Sinai na mfereji wa Suez.

View attachment 443505

Wanajeshi wana mataifa ya kiarabu waki surrender

Wakati huo huo Upande wa Mashariki Jordan wakaanza kumimina risasi kwenye makazi ya wayahudi na hivyo kuwafanya Israel wajibu mapigo. Na Israel ikashika Ukanda wa Magharibi mpaka tarehe 7 ikawa imekamata Mji wa Kale wa Yerusalem kwa upande wa Magharib. Na chief chaplain wa Jeshi la Ulinzi la Israel akapuliza tarumbeta ya kuashiria kuwa sasa wameiunga Yerusalem ya Magharib na kuwa kitu kimoja.

Upande wa kaskazini Israel ikapiga Ngome ya Syria katika vilele vya Milima ya Golan kwa siku mbili kabla ya kupeleka Vifaru na wanajeshi wa miguu June 9. Baada ya mapambano makali ya siku moja Syria wakaanza kurudi nyuma kukimbia milima ya Golan.

Waarabu Waomba Kusitishwa Vita

Kilio cha nchi za kiarabu kikafika umoja wa Mataifa ambao ikabidi waingilie katika na tarehe 11 UN wakaomba kusitishwe mapambano yaliyokuwa yakiongozwa na Israel dhid ya mataifa ya kiarabu.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa likaitisha kikao na kuwaomba Israel wayaachie yale maeneo ambayo walikuwa wameyashikiria. Israel ikakataa wakayateka na kuyakalia maeneo ya Yerusalem ya mashariki na kuweka majeshi yao rasmi katika maeneo waliyo yakamata. Na Waisrael wakaweka masharti kuwa Gaza,Ukanda wa Magharibi na Milima ya Golan itarudishwa kwa kubadilishana na waarabu ikiwa watatambua haki za Waisrael na kuheshimu Taifa la Israel.

Viongozi wan chi za kiarabu wakiwa wamefadhaishwa sana na kushindwa vita ile wakakutana mwezi Ogasti kujadiliana na nini mustakabali wa Mashariki ya Kati. Nao wakaamua kuwa hakutakuwa na amani, hakutakiwa na mazungumzo na kuwa hawatalitambua taifa la Israel na kujipanga kupigania haki za taifa la palestina katika maeneo yaliyotwaliwa.

Misri tofauti na wenzie ikawa imechoka sana na kufadhaishwa sana kwa kile kipigo kiasi kwamba haikuwa na hamu tena na vita. Ikakaa kujadiliana na Israel na kufikia hatua ya kuwekeana mkataba wa amani. Na mwaka 1982 israel ikawarudishia Misri ghuba ya Sinai baada ya Misri kukubali kuitambua Israel. Baadaye Misri na Jordan wakaamua kuachana na madai yao ya ukanda wa kazi na West Bank kwa wapalestina ambao mwaka 1990 walianzisha mazungumzo ya “kubadilishana amani kwa ardhi” land for peace. Ukanda wa Mashariki ukarudishwa Jordan. Na mwaka 2005 Israel wakaamua kuachia ukanda wa gaza na mpaka sasa makubaliano yao yanafanya kazi

Nini matokeo ya vita vile?

Kinyume na mategemeo ya nchi za kiarabu kuwaondoa Israel, Israel ikawa sasa wamewapewa nafasi na sababu ya kujitanua zaidi kwa kujiongezea maeneo mengi zaidi na mpaka leo tunaona baada ya Vita vile Israel ilitanuka zaidi kuliko kabla ya Vita.

Mataifa ya kiarabu yalifadhaika sana na kile kitendo cha wao kwa ujumla kupigwa na Taifa dogo na ambalo pia lilikuwa changa ni vita ambayo mpaka leo inawaumiza watu wengi sana wenye mlengo tofauti na Israel.

Israel waliishangaza dunia kwa kiasi ambacho mpaka leo imekuwa ni mfano mkubwa sana kwenye masuala ya uzalendo na intelejensia duniani. Walizidi kuimarika na kujiona kuwa wao ni kitu kimoja na kuwa wnapaswa kushikamana pamojana tofauti zao za Kiimani. Katika Israel kuna Wayahudi, Wakristo na Waarabu. Lakini hawa wote linapokuja suala la taifa lao hushikamana sana na kuwa kitu kimoja.

images.jpg
index.jpg



GuDume ,Gide MK et al
 
Kuna mzee mmoja aliniambia kuwa... Kulikuwa na moja ya viongozi wakubwa kwenye jeshi la misri na wapambe wake ambaye ndio alikuwa ndiye anatakiwa kutoa ruhusa ya mwisho ili ndege za Misri ziweze kuruka na kushambulia... Lakini kumbe bila wao kujuwa yule mkuu wa majeshi hayo alikuwa na asili ya Israel)myahudi) na hivyo akatumia mwanya huo kutoa taarifa kwenye jeshi la Israel kwa siri na kufanya mawasiliano namna gani wagewapiga wamisri ili hali mpango wa wamisri ilikuwa ni kulifuta taifa la Israel ndani ya mda wa chini ya nusu SAA liwe halipo kabisa. Kwa hiyo mwanajeshi huyo mwenye asili ya kiyahudi kila walipokuwa wanamuuliza(jeshi la misri) kwamba turuke yeye alikuwa anawaeleza subiri kidogo hadi mda ufike.na kumbe kwa upande wa pili alikuwa akiwasiliana na jeshi la Israel,na jeshi la israeli lilitumia mwanya huo kujipanga kimashambulizi.
Na mambo yalipokuwa tayari kwa Israel, bila jeshi la Misri kujuwa wakajikuta wameshambuliwa na mwisho yule mwanajeshi wa misri(myahudi) alijiua kwa kujipiga risasi..
Note; sijawahi kuthibitisha taarifa hizi lakini ni mzee mmoja wa zamani kidogo ndio aliyeniambia kwa hio usinihukumu sana.
 
Asante "chizi maarifa" habari tamu sana, sasa Israel waliwezaje kugundua sehemu silaha zilipofichwa?

Nipe habari hiyo.
 
waarabu habari yao iliisha kwe vita ile kwa hawa warabu wa cku hzi walivyokua wanafiki hawawez kabisa kuanzsha vita maana watapigwa mpk wachanganyikiwe....maana watakaa mchana wapange vita lakin usiku wengine wanapanda ndege wanaenda telaviv kusema
 
Kuna uzi humu intelligence unahusu shushushu wa Israel alikua akitoa taarifa kuhusu silaha za Syria akijifanya kama mfanyabiashara wa Argentina nimeusahau uzi jina Lake
Eli Cohen nadhani
Asante "chizi maarifa" habari tamu sana, sasa Israel waliwezaje kugundua sehemu silaha zilipofichwa?

Nipe habari hiyo.
Google MTU anaitwa Eli Cohen km cjakosea,Uzi upo humu
 
Miaka yote Israel ilikuwa na upelelezi mzuri sana kwa mataifa yote.kipindi hicho egypt na marafik zake wanajiandaa na israel walikuwa kazin kukusanya data ya mipango na silaha zitakazotumika kuTumika.

Wakaamua kuzifanyia ndege zao mazoez ziwe na uwezo wa kupiga mara sita zaid tofaut na ilivyokuwa mara ya kwanza zilikuwa zinaweza piga mara moja na kurudi.ndege za mataifa ya kiarabu zilikuwa na uwezo wa kwenda kwa adui kupiga na kurud mara moja kabla ya kuandaliwa kwenda kupiga tena. Israel wakawa wakifanya mazoez zaid. Usa na europe nations zilikadiria kuwa kama ile vita ingepiganwa kwa namna ambavyo waarab walikuwa wamejiandaa ni ndani ya siku 1-2 kusingekuwa na taifa la israel.

Israel wakajipanga kwa namna yao na kuona wangeweza wapiga jamaa kwa siku 2-3 na kuwanyong'onyesha kabisa.

Walipataje info? Walikuwa na intelejensia kubwa na hata kupata mazungumzo ya vikao vya mataifa hayo ya kiarab kupitia mfalme wa morroco king hassan II yeye aliweza hata kuwapatia records za mazungumzo. Israel wakanyamaza kimya wakijiandaa kimya kimya bila mataifa hayo kujua sababu vikao vyao vilikuwa vya siri sana. Kipindi chote hicho israel inakusanya data kupitia waisrael ambao wapo nchi hizo za maadui kwenye nafas za juu. Pia waliweza kunasa mazungumzo ya simu ya wakuu hao waliwasiliana na makamanda kuwa wawe tayar kwa ajil ya kuwamaliza waisrael.

Udukuzi ulianza miaka.mingi sana na israel wamekuwa siku zote wakitaka kuwa hatua mbele zaidi ya maadui zao.
Asante "chizi maarifa" habari tamu sana, sasa Israel waliwezaje kugundua sehemu silaha zilipofichwa?

Nipe habari hiyo.
 
Back
Top Bottom