Intelijensia haiko salama, Je, nchi itakuwa salama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Intelijensia haiko salama, Je, nchi itakuwa salama?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Miwatamu, Oct 13, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Ndugu wana jamvi, kwa kila mtu anayependa amani, uhuru na mshikamano ambao umekuwepo kwa kipindi chote tangu tupate uhuru, hakika ataanza kujiuliza mara mbilimbili ni wapi tumeteleza nawapi tuendako kwa sasa!!

  Watu wengi wamekuwa wakiinyoshea serikali kidole kwa lengo jema tu, la kutaka kuitawala nchi hii kwa mjibu wa sheria na kanuni zilizowekwa. Lakini kinyume na hapo mfumo wa utawala umebadilika na kuwa wa aina moja! Nasema hivyo kwa kuwa sasa hivi kuanzia nyumbani kwako, ofisini, kwenye vijiwe na kwingineko, ili mtu uonekane wa maana lazima uwe unaunga mkono mfumo uliopo hata kama ni mbovu.

  Waona mbali wamekuwa wakikosoa kuwa mfumo wa kufanya taasisi ya ulinzi kuwa ni sehemu ya chama tawala, ipo siku italeta sintofahamu katika jamii au Taifa kwa ujumla. Sasa kitu hicho tumeanza kukiona! Kitendo cha Kamanda wa Mkoa wa Mwanza kuuawa ni kielelezo tosha kuwa sasa hali si shwari. Polisi wameshindwa kulinda nchi na wananchi wake, sasa njia mbadala itafikia hatua kila kundi linajitengenezea interijensia yake ya kujilinda! Na hapo ndipo taabu itakapokuwa imeanzia.

  My take: ili kukomesha haya yasiendelee, tunaomba serikali isimamie haki pale panapostahili ili kila mtu aamini kuwa kitengo cha usalama kipo kwa ajili ya watu wote na nchi yao. Vinginevyo makubwa zaidi ya hili la Mwanza na Mbagala tutaendelea kuyaona sana.

  Je, wewe unasemaje kwa hili?
   
 2. Z

  Zimamoto JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 464
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Tatizo ni kwamba viongozi wamesahau wajibu wao wa msingi. Wajibu wa viongozi ni kusimamia rasilimali za nchi, ikiwa ni pamoja na rasilimali watu kwa manufaa ya wananchi wote. Kinyume chake viongozi wanatumia rasilimali hizo kujitajirisha wao na familia zao, na suala kubwa likiwa ni jinsi ya kuendelea kutawala tena kwa gharama yoyote. Kwa mfumo huo tutegemee mambo mbengi.
   
 3. N

  Nyadunga Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Je hakuna uhusiano na suala la kamanda wa uhamiaji aliyenusurika kuuwawa? kuna tetesi walikuwa wanagombania demu
   
 4. Root

  Root JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,184
  Likes Received: 12,898
  Trophy Points: 280
  Divide and rule


  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 5. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Intelijinsia ameuwawa na kitu kizito,we huna habari??
   
 6. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hatuna usalama wa taifa, ila tuna usalama wa viongozi mafisadi wasiojali maslahi ya raia na nchi yao. Tunausalama wa chama kilicho madarakani ili kulinda maovu ya viongozi na wezi wa rasilimali. Tuna usalama wa wezi mafisadi na watovu wa maadili kulinda uonevu, maouvu na rushwa zisipelekwe mahakamani na watuhumiwa kupewa hukumu.
   
 7. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Jamani mbona hamuelewi? Hawa sio Chedema bana, kama wangekuwa Chadema wangepata taarifa za kiintelijensia!
   
 8. m

  mnyinda JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wiki hii imekuwa mbaya kwa jeshi la polisi na majambazi huko moshi baada majambazi kuliwa na jeshi la polisi huko kilimanjaro na wao kumuuwa RPC katka jiji la mwanza...
   
 9. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  udhaifu wa Mr. Dhaifu aka Vasco Da Gama II anajaribu kutugawa Watanzania ili amalize kipindi chake
   
 10. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Kila kukicha linazuka jipya linaloashiria anguko kuu la serikali ya ccm chini ya jk.

  Mifano ni mingi kuanzia kuuawa kwa raia wasio na hatia kunakofanywa na vyombo vya dola sehemu mbalimbali nchini; lugha chafu za kashfa na uchochezi zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kama redio na magazeti; kukataa kuwajibika kwa upande wa serikali pale ambapo makosa yanajulikana wazi ni yao; rushwa iliyokithiri ndani ya serikali na ccm; vurugu za wazi zinazofanywa na baadhi ya waumini wa dini au madhehebu fulani kwa waumini wa dini au madhehebu mengine n.k.

  Kwa kifupi Tanzania ni kama meli inayoelea kwenye bahari yenye mawimbi makali bila nahodha. Meli yetu haina dira na mafuta yanaelekea kuisha. Kila mtu sasa anafikiria namna ya kujitupa majini ajiokoe mwenyewe.

  Watanzania tusikubali kuachia janga hili maana tutaumia wote. Wakati umefika tutafute nahodha mwingine mwenye uwezo wa kutufikisha pale tunapotaka kwenda.

  Pamoja tutaweza. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
   
 11. e

  emmanuel babu New Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mambo yanatisha .
   
 12. M

  Makupa JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni muda muafaka sasa kumkamata Dr Sllaa kwa ajili ya mahajiano zaidi kwani ndie mtu anaetangazia umma kuwa Tanzania haitatawalika .
   
 13. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  mGOMBA101: hilo nalo neno.
   
 14. e

  emgitty06 Senior Member

  #14
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haita tawalika kwasababu ya ujunga na udhaifu wa viongozi waliopo madarakani na si kwasababu yake yeye binafsi.
   
 15. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Hiii kali sasa! tangu fashion ya vitu vizito vianze imekuwa taabu kwelikweli.
   
 16. l

  lufungulo k JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 1,267
  Likes Received: 451
  Trophy Points: 180
  Nakushukuru saana mtoa hoja, maana umeonesha kuguswa na yale mabaya yanayolisibu taifa kwa sasa. huku ukijaribu kuwashirikisha watanzania wenzako, nini ushauri wao kwa taifa lao. binafsi namkubali saana mkoloni kwenye suala la utawala jinsi wanavyopanga ulinzi wao binafsi na raia wanao watawala pamoja na mali zao. viongozi wetu wamekuwa na safari nyingi nje ya nchi na ndani ya nchi lakini wamekuwa wakiona maendeleo ya wenzetu wao hawachukui chochote kwa ajili ya taifa zaidi ya kufurahia safari hizo na kuponda raha kwa zile fedha za masurufu walizolipwa. tofauti saana na kijana aliyefanikiwa kwenda ughaibuni kwa jityihada zake mwenyewe hurudi nyumbani akiwa amejifunza mambo mengi kwa ajiri ya taifa lake na familia yake na kile alichofanikiwa kukichuma basi familia yake na jamii inayomzunguka itanufaika .jiulize mkoloni ktk mji wa DSM enzi hizo aliweka vituo vya polisi Central, msimbazi,magomeni,oyesterbay, chang'ombe kilwa road na buguruni jiulize umbali ulioko kati ya kituo kimoja na kingine wakati huo wa mji wa DSM hivi sasa wakati wa jiji la DSM lililopanuka tunavyo vituo vya polisi vya kutosha jibu kwa watawala wetu ni jepesi , hali ikiruhusu tutajenga maana iko ktk mikakati yetu. kweli suala la ulinzi nalo nila propaganda? miji yote mikubwa duniani patrol ya askari ni ya muhimu mno, magari ya doria, mbwa wa doria na farasi wa doria haviepukiki .vingozi wetu ni waongo wenye kupenda kutawala na muda wao ukifika wa kustaafu wanabuni mbinu za kuonyesha bila wao khali itakuwa mbaya kwa idara wanazoziongoza na taifa kwa jumla sasa jiulize amefanya nini kuhakikisha akiondoka sekta ameiboresha na kila mtu atakayeingia ataweza kuitendea haki nafasi hiyo.tukubali tusikubali wanasiasa wapunguze matumizi na fedha hizo zielekezwe kwenye vyombo vya ulinzi ,ujenzi was vituo vya kisasa vya polisi nje ya mji, vitendea kazi vya kisasa magari ya kisasa ya doria na mafuta ya kutosha pamoja na motisha kwa watendaji.
   
 17. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  TISS wafu tu
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...