Intel Alert: Wamiliki wa nyumba walizwa na utapeli mpya; Wauza nyumba zao bila kujua

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Nimekutana na habari kuwa upo utapeli wa aina yake ambao umeshawaliza watu wachache. Unahusiana na kundi linalokuja kwa lengo la kuja kupangisha nyumba na kufanya mambo lukuki hasa kwa watu wenye nyumba mpya. Mtu mmoja amesimulia hivi:

Mmh ndugu zangu ni kwel hawa matapeli mimi mwenzenu nimeuvaa mkenge Morogoro na niliona ni wahitaji wa nyumba kweli na modus operandi waliyoitumia ni hiyo ya kuhonga TRA ILI MALIPO YAWAHI Wanatumia namba 0758409096 na 0682768889 ni vyema watu wa usalama waingilie kati asante kwa kunifumbua macho na masikio kwani nilikuwa naendelea kufanya nao mawasiliano

Na mwingine akadokeza

jamani yamenikuta ni juzi walikuja kwenye eneo langu chanika ila sikufikia hatua ya kutoa hela walikuwa bado wapo kwenye mawasiliano na wakaniambia niende posta wamenitumia mkataba wa vitu wanayohitaji jamni tuweni mamcho mimi nashangaa kwa nini simu zimeshasajiliwa na hawakamatwi?nadhani kuna siri kubwa nadni ya mtandao huu..lakini siku moja watakamatwa tu.
Yaani ni jana tu ndio nimecheck mtandao nione ahiyo project ndio nakutana na watu wametoa comments zao kuwa wameshatapeliwa. Tuwemakini kwa kweli.

na mwingine akasimulia

mimi niko amerika, najenga nyumba yangu hapo dar, fundi anayejenga nyumba amenipigia simu kuwa watu hao wa TANZANIA JAPAN ORPHON PROJECT WA SIMU NUMBER 0783-927-196 MR SABAI wana hitaji nyumba ya kupanga kwa miaka 2 kwa dola 800 jumla watatoa dola 19,200.00 kwa ajili wafanyakazi wao, wakasema watajenga fence ya umeme kuzunguka nyumba, kuchimba kisima cha maji, watamalizia kuweka umeme kama offer . Lakini baada ya kupata habari hiyo nikapiga simu kwenye ubalozi wa japan hapa USA wakasema hakuna shirika la namna hiyo na wakanitajia majina kama hayo uliyoolezesha kuwa ndiyo wamiliki wa shirika hilo haramu.OK WANAIBAJE? watakupeleka kwa wakili wao ambaye pia ni taperi mwenzao, unasaini mikataba mingi usiyoilewa na kwa vile mawazo yako yote yako kwenye lundo la pesa ya miaka miwili unasaini tu, lakini akili yao ni kukusainisha mkataba kwamba unawauzia nyumba kwao kwa bei hiyo ya kupanga kwa miaka miwili, sasa kwa vile wewe hujui baada ya miaka miwili ya mkataba wa kupanga kuisha ukiwambia ku-renewal mkataba watakucheka kwamba wewe uliwauzia nyumba, na ni kweli umesaini tena kwa wakali!!! kuweni macho sana.

Kama tulivyoifumua DECI lets stop do it again.. !!!
 
Asante kwa taarifa mkuu...wananchi tuwe makini na utapeli huu...TCRA amkeni kumekucha.
 
Utapeli huu una muda mrefu nadhani ulififia kidogo na sasa umeibuka, kuna staff mwenzangu alikuta barua ya offer ya kupanga nyumba yake kwa bahati nzuri alinishirikisha na nikamtahadharisha akataka asiamini akidhani namuwekea kauzibe, lakini baadaye aliendelea kuwasiliana nao kwa tahadhari kubwa, mwishowe walimtaka awatumie ths. 200,000 ili wamfanyie mpango TRA mwanza apate msamaha wa kodi hapo ndipo alipokuja kujua nia yao ilikuwa nini. jina la Kampuni iliyotumika ni hilo hilo na moja ya majina yao ni Odhiambo na Ole sabai.
Pia kuna utapeli wa kutaka kujenga minara ya simu huja mtu akiwa na gari ya moja ya makampuni ya simu za mikononi na kukueleza kuwa kuna mpango wa kujenga mnara eneo hilo na huonyesha nyumba zinazoweza kuhusika yako ni mojawapo, humuhadaa mwanye eneo kuwa wanalipa vizuri na ili mnara ujengwe eneo lake anatakiwa atoe kiasi cha pesa ili wamfanyie mpango huo na akitoa ndio zinakuwa zimeyeyuka.
 
Ni kweli mwanakijiji the same name company walikuja mwanza maeneo ya jina langu wakataka kupanga kwa kutaka kumalizia kibanda changu na usafiri wangu ambao wamekuwa wakiiona nikitumia na wanajua siko ndani ya tanzania wakasema wanaomba wamalizie kwa 750$ per month kwa two years....mama aliye kuwa onsite akawasiliana na mie kuwa watu wanataka gari na nyumba yako..ili wapange...nikastuka early stang nikawaambia wasubili nipate likizo....hawakuwa wavumilivu..by the time nafika wakawa washangudilika...so hata mwanza wapo.
 
Mmmm kweli tuweni macho jamaa hawa wako makini sana na wanfanya kazi kwa mahesu ya hali ya juu sana.Tuache taama ya kupenda psa za haraka haraka.
 
Asante kwa taarifa mkuu...wananchi tuwe makini na utapeli huu...TCRA amkeni kumekucha.
<br />
<br />
sheria za ardhi zinajulikana hiyo style wanaoitumia kwa mtu mwenye ufahamu huwezi kumtapeli..utawezaje kusainishwa sales agreement bila kujua .
 
Niliona kitu hii nadhani mwezi machi mwaka jana huko mikocheni. Na hawa walikuja moja kwa moja kwa bwana mmoja jirani yetu ambapo tulikuwa tumepanga jirani yake. Mzee yule alikuwa very excited na offer za hao matapeli. Lakini bahati nzuri alishtuliwa na mzee mwingine ambaye alikwisha uona utapeli wa aina hiyo. Matapeli hao walidai wanatokea mwanza ambako ndio shirika lao liliko na kuwa wanatafuta nyumba kwa purpose kama hizo zilioainishwa katika post za hapo juu. Kinachowatega watu kirahisi ni ile promise kua wao wataiwekea nyumba vifaa vya kisasa mfano AC na kua vifaa hivyo vitabaki kua mali ya mwenye nyumba pindi mkataba utakapoisha. Pia bei wanayotoa kama malipo ya upangishaji zinatempt kwelikweli. Lakini kwa akili rahisi tu jiulize kama wana uwezo huo na wanatoka ktk shirika kubwa namna hilo kwanini wanatafuta nyumba mitaani na wasitangaze katika magazeti? Jamani tuweni makini
 
mkuu asante kwa taarifa.. nadhani nikutokana njaa na haraka zetu ndio zinatuponza na kitu chengine mi naona hizi hela za mazabe ndio zinaongoza
 
Jamani tuwe makin sana ujue kila siku kinacho tu ghalimu ni tamaa tu hakuna kingine tuache tamaa
 
Na siye watanzania sometimes tunakuwa wazembe, nyumba yangu sasa iweje unisainishe mikataba yako? Mimi ndiyo natakiwa kuwa na mkataba wa kukusainisha wewe. Hata kama ni World bank, Obama au hata Gaddafi unapanga nyumba yangu, mkataba ntakupa mimi wewe ndiyo uusaini!!!!!!!!!!! Lakini pia hii ni tatizo la ukosefu wa real estates kumonitor na kusimamia haya mambo ya nyumba.
 
Hao kina Ole Sabai na NGO yao ya Tz Japan Orphanage Project walitaka kupanga nyumba yangu mwaka 2008 kwa style hiyo ya kitapeli, sikuwa tayari kupangisha kwa bei waliyotaka ya Dola 600 kwa mwezi. Walinisumbua sana na nakumbuka walimwachia Mlinzi wa nyumba yangu barua yao na rasimu ya mkataba wa hovyo, bahati mbaya niko mbali na nyumbani....hivyo nimeshindwa kuweka hiyo nakala ya mkataba wao.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Utapeli huu una muda mrefu nadhani ulififia kidogo na sasa umeibuka, kuna staff mwenzangu alikuta barua ya offer ya kupanga nyumba yake kwa bahati nzuri alinishirikisha na nikamtahadharisha akataka asiamini akidhani namuwekea kauzibe, lakini baadaye aliendelea kuwasiliana nao kwa tahadhari kubwa, mwishowe walimtaka awatumie ths. 200,000 ili wamfanyie mpango TRA mwanza apate msamaha wa kodi hapo ndipo alipokuja kujua nia yao ilikuwa nini. jina la Kampuni iliyotumika ni hilo hilo na moja ya majina yao ni Odhiambo na Ole sabai.
Pia kuna utapeli wa kutaka kujenga minara ya simu huja mtu akiwa na gari ya moja ya makampuni ya simu za mikononi na kukueleza kuwa kuna mpango wa kujenga mnara eneo hilo na huonyesha nyumba zinazoweza kuhusika yako ni mojawapo, humuhadaa mwanye eneo kuwa wanalipa vizuri na ili mnara ujengwe eneo lake anatakiwa atoe kiasi cha pesa ili wamfanyie mpango huo na akitoa ndio zinakuwa zimeyeyuka.
Hilo jina Sabai lime-click kwenye kichwa changu. Huyu bwana alikuwa mfanyakazi wa Wizara ya Ardhi kwenye miaka ya 1970-80 hivi. Baadae aliachishwa kazi lakini aliendelea kujitambulisha mitaani kama Afisa Ardhi akiwapimia watu viwanja, kuwawekea beacon fake na kuwapa Offer za uongo. Alikuwa akishirikiana na wenzake ambao walikuwa bado wako kwenye ajira wizarani. Mimi ni mhanga wake katika eneo la Mabibo, Makuburi. Watu wengi tuliaminishwa kuwa tuna offer za kweli lakini tulipofuatilia tukakuta zote ni fake.
 
Sasa je mtu aliyiengia mkenge ina maana ndio kaliwa moja kwa moja? Kwani sheria na mahakam zipo kuteteta hata upindishwani na uptoshwaji wa sheria?????

Zaidi ya watu kuwa makini wenye ndugu na jamaa waliongizwa mkenge wajitokeze wasaidiwe.

Ingawa sio mwanasheria naamini mkataba sio katiba hata kama umeshakwisha na kupita bado mahakama na sheria zinatakiwa kuwepo wa ajili ya kutoa haki.
Haki ambayo iliibiwa inaweza kurudiishwa


Na siye watanzania sometimes tunakuwa wazembe, nyumba yangu sasa iweje unisainishe mikataba yako? Mimi ndiyo natakiwa kuwa na mkataba wa kukusainisha wewe. Hata kama ni World bank, Obama au hata Gaddafi unapanga nyumba yangu, mkataba ntakupa mimi wewe ndiyo uusaini!!!!!!!!!!! Lakini pia hii ni tatizo la ukosefu wa real estates kumonitor na kusimamia haya mambo ya nyumba.


Sio mara zote lazima mwenye nyumba ndio aandike mkataba mkuu .Mkataba uliondaa wewe wewe unaweza usiwe na scope na vigezo vyote yote amabayo wanahitaji mashirika kama world bank au watu marufu. Mara nyingi mashirika makubwa yaipanga kwa kwa mtu individual wao ndio wanaandika mkataba bada ya majadiliano na mwenye mali then mtu unachotakiwa kufanya ni kutafuta mwanasheria aupitie na kukushauri kuw aatia viklombwezo vyao wavilivyoongeza hakuna kunachopindisha mkataba wako wa kupangisha.

Theoreticlly umesema ni sahii lakini practically mashirika mengi yaliypanga kwa watu ndio yanaadaa miatakaba .Hapo tean wapangishaji wengine hawatafuti hata wanasheria. Ni TRUST tu. So matapeli wametumia ule mwanya wa trust.



 
<br />
<br />
sheria za ardhi zinajulikana hiyo style wanaoitumia kwa mtu mwenye ufahamu huwezi kumtapeli..utawezaje kusainishwa sales agreement bila kujua .

Si wote wanajua mkuu ndio maana ni wajibu wetu kukumbushana.
 
Na wabongo tulivyo wepesi wa kusaini tu bila kusoma kwa umakini!
Angalau tunakumbushana mambo kama haya kwani hata ndege mjanja naye hunasa katika tundu bovu.
 
Sasa je mtu aliyiengia mkenge ina maana ndio kaliwa moja kwa moja? Kwani sheria na mahakam zipo kuteteta hata upindishwani na uptoshwaji wa sheria????? Zaidi ya watu kuwa makini wenye ndugu na jamaa waliongizwa mkenge wajitokeze wasaidiwe. Ingawa sio mwanasheria naamini mkataba sio katiba hata kama umeshakwisha na kupita bado mahakama na sheria zinatakiwa kuwepo wa ajili ya kutoa haki. Haki ambayo iliibiwa inaweza kurudiishwa


Let the buyer and seller be aware. Hizo ni baadhi ya sheria zinazo apply kwenye haya mambo. Unapoingia kwenye mkataba make sure you clearly understand what you are signing for. Kama hukulazimishwa, kama kulikuwa hakuna undue influence, kama hukuwa minor, kama mkataba is not against the law or public policy, huwezi kuvunja mkataba on the ground kuwa uliingizwa mkenge.

Sio mara zote lazima mwenye nyumba ndio aandike mkataba mkuu. Mkataba uliondaa wewe wewe unaweza usiwe na scope na vigezo vyote yote amabayo wanahitaji mashirika kama world bank au watu marufu. Mara nyingi mashirika makubwa yaipanga kwa kwa mtu individual wao ndio wanaandika mkataba bada ya majadiliano na mwenye mali then mtu unachotakiwa kufanya ni kutafuta mwanasheria aupitie na kukushauri kuw aatia viklombwezo vyao wavilivyoongeza hakuna kunachopindisha mkataba wako wa kupangisha. Theoreticlly umesema ni sahii lakini practically mashirika mengi yaliypanga kwa watu ndio yanaadaa miatakaba .Hapo tean wapangishaji wengine hawatafuti hata wanasheria. Ni TRUST tu. So matapeli wametumia ule mwanya wa trust.
Hivi anayedraft mkataba ni muuzaji au mnunuaji? Nakubali mkataba uliondaa wewe unaweza usiwe na scope na vigezo vyote yote amabayo wanahitaji mashirika kama world bank au watu marufu. Lakini sio wewe, ni mwanasheria wako, ndie anayetakiwa ku draft huo mkataba on your behallf. Ukidraft mwenyewe hutajua ni vipengele gani uweke na vipi uache unless na wewe ni mwanasheria, tena wa sheria za ardhi. Hata mashirika kama world bank au watu maarufu mikataba yao inakuwa drafted na kupitiwa na wanasheria.

Hao watu waliongizwa mkenge kama wangekuwa wamewatumia wanasheria walio specialise kwenye property law au wataalamu wa ku draft na kusoma mikataba wala wasingeingizwa mkenge. Tena kama mkataba wameudraft wenyewe lazima niupeleke kwa mwanasheria au specialist wa real estate acheki kama uko kama nilivyokubaliana na upande wa pili. Tatizo wabongo tunajifanya tunajua kila kitu.
 
Back
Top Bottom