Instagram Kuwezesha Kupost Picha au Video 10 kwenye Post Moja

muvika online

JF-Expert Member
Nov 27, 2016
374
283
Instagram-Post.jpg

Baada ya Instagram kufanya majaribio ya uwezo mpya wa kupost picha au video zaidi ya moja kwenye post moja, sasa uwezo huo umekuja live kwenye programu zote za instagram. Mtumiaji ataweza kupost picha au video 10 kwa mara moja kwenye post moja ya mtandao huo wa Instagram.



Ili kupost picha nyingi kwa wakati mmoja uta bofya kitufe kipya kilichop upande wa kulia juu ya picha wakati unataka kupost kisha hapo utapata uwezo wa kuanza kupost picha 10 kwenye post moja. Kumbuka kuwa kwa sasa instagram imeweka uwezo wa kuweka maneno (caption) kwenye picha moja tu hivyo usitegemee kila picha itakuwa na maneno yake bali picha zote zitatumia (caption) moja.

Sehemu hiyo mpya tayari imeshanza kutoka kwa watu wote wenye programu za Instagram za iOS na Android hivyo pale unapona toleo jipya la programu hiyo ni vyema ukaupdate ili kuweza kupata sehemu hiyo mpya
 
Back
Top Bottom