Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro atuma salamu za Pasaka kwa Watanzania wote

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497



Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro anawashukuru Wananchi kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwa Jeshi la Polisi jambo ambalo limesaidia kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa hapa nchini.

Kiujumla hali ya usalama hapa nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia Silaha yamepungua kwa kiasi kikubwa na jitihada za kukabiliana na makosa ya usalama barabarani zinaendelea ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo na majeruhi kwa raia.

Tunapoelekea kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi katika mikoa yote linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa sikukuu hii inasherekewa kwa amani na utulivu na hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyofanyika na pale vitakapojitokeza vitadhibitiwa kwa haraka.

Ulinzi utaimarishwa kwenye maeneo yote yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo katika hali ya utulivu.

Wazazi wanatakiwa kuwaangalia watoto wao na kutowaacha kutembea peke yao bila ya kuwa na uangalizi wa karibu, pia wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo ikiwemo kutoruhusu disko toto na kujaza watu kupita kiasi.

Vilevile Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara kuwa makini na kuzingatia Sheria za Usalama barabarani hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kubeba mishikaki, kwenda mwendo kasi, kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.

Nawatakia Pasaka njema.

Chanzo: Mpekuzi
 
02-soldier-saluting-fsl.jpg
 
My Take
Labda mseme mnatanda kwa hofu ya waraka. Mimi sijawahi kuona hao wezi wa kuibia waumini katika kiwango cha kuhitaji polisi
Sio kila kitu unapinga
Usalama kwa maisha na mali za waumini ni jambo muhimu
Si wezi tu,je magaidi wakiamua kutetemesha nchi utasemaje?
 
Sio kila kitu unapinga
Usalama kwa maisha na mali za waumini ni jambo muhimu
Si wezi tu,je magaidi wakiamua kutetemesha nchi utasemaje?
Ni lini makanisa yaliwahi kuingiliwa na vibaka,wakati wa ibada? Punguzeni woga
 
Back
Top Bottom