kwa hali hii watanzania wenzagu tegemeeni hali mbaya zaidi huko tunakoelekea /MASKINI NCHI YETU TANZANIA/UPDATE
Habari nilizozipokea sasa hivi kwa njia ya SMS kutoka kwa doctor mmoja pale Mhimbili zinasema hivi,nanukuu,"Hii ya sasa ni bab kubwa responce ni 100% MPAKA EMERGENCY,intern ndio wamemaliza kikao chao cha kupeana moyo na specialist ndio wanaanza Russian culture nw..together we can make it" mwisho wa kunukuu sms niliyoipokea.
My take hivi serikali ina shindana na madaktari kwa ajili ya maslahi ya kisiasa? au inatakiwa kulinda afya za wananchi wake?
Maana kama mawaziri wamelalamikiwa na ni kweli wameshindwa kuwajibika kwa nini waendelee kuwepo hapo?na je inawezekanaje kupokea malalamiko ambayo kimsingi wao ndio wanalalamikiwa na kisha wakayafanyia kazi?