Insights muhimu kuhusu mgomo wa madaktari leo 7/03/2012

Mgomo wa madaktari unahusishwa na udini

|
9:11 AM
|
Pendael laizer
|

Mgomo wa madaktari uliomalizika hapo juma na unaoendeleo hata leo wahusishwa na udini kuwa eti Dr haji mponda anashinikizwa kujiuzulu maana ni muislam na wanasema hawa wanaharakati hawafai maana wanaibua mambo katika sekta ambazo waislam wamezishkilia na wanadai kuwa watakuja hata kumshinikiza rais Jk kujiuzulu manake nchi haita tawalika na wanasema pia waislam wanaonewa sana hata katika elimu manake waziri wa elimu ni mkiristo. Wamesema wanaandaa maandamano makubwa kupinga mgomo wa madaktari na kuwapinga hawa wanaharakati maana watakuja sababisha nchi isitawalike. Source radio imani asubui hii

Madaktari wapo kwenye mgomo hakuna atayekutibu utindio wa ubongo
 
Hili game ni pevu.
Wagonjwa MNH wamepungua sana, Clinic za nje zinasuasua, Baadhi ya madaktari wako njia panda. Wengi hawapo maeneo ya kazi. Nadhani mgomo ni dhahiri.
Serikali ifanye maamuzi haraka maana hali hii haiwezi kuvumulika tena kuna hatari ya serikali kujutia hali hii, na wahenga wanasema majuto ni mjukuu.:hat::hat:
 
Wakuu wanaJF

Leo ndiyo ile siku ambayo madaktari waliweka wazi kuwa watagoma endapo serekali itashindwa kuwasimamisha kazi mawaziri wa afya. Napost uzi huu ili kujua hali ikoje kwa wale walio karibu na hospitali zetu hususan MUHIMBILI, KCMC, BUGANDO, DODOMA, MBEYA n.k,Je? Kuna madaktari kazini?

Na vipi wananchi wa kawaida wanasemaje kuhusu mvutano huu kati ya serikali na madaktari?
Lakini pia ikumbukwe kuwa waziri mkuu Pinda alipokuwa anaongea na madaktari tar 9/02/2012 pale CPL MNH aliwaahidi wananchi kuwa serikali ina nia ya dhati kutatua mgogoro kwenye sekta ya afya na kwa kuanza akawasimamisha Blandina Nyoni( aliyeteuliwa na kuapishwa na rais) na Deo Mtasiwa( sina uhakika aliteuliwa na nani labda mnisaidie).

Sasa kama pinda alimsimamisha kazi mteule wa rais ambaye ndiye mtendaji mkuu wa wizara na kusema kuwa atamshauri rais awafukuze mawaziri je?

1. kwa nini asiwe na mamlaka ya kuwasimamisha wateuele wengine wa rais ambao wako ofisi moja na katibu mkuu?
2. au hakushuri rais kama alivyo ahidi kufanya? Na kama ni hivyo ina maana aliudanganya umma hivyo anapaswa kujiuzulu mara moja kulinda heshima yake.
3. kama alimshauri rais halafu huyu bwana mkubwa akapuuzia pia anapaswa kuonesha nia yake ya dhati ya kuwatetea wanyonge kwa kujiuzulu maana amedharauliwa kupita kiasi.
4. kama madaktari wataendelea na msimamo wao wa kugoma hadi serikali iwafukuze mawaziri na serikali ikakataa kwa madai kuwa rais hafanyi kazi kwa shinikizo, je? serikali itaweza kuwafukuza madaktari wote na kuajiri wengine au itaendelea kuatimua wanajeshi kutibu raia?
5. Na vipi kwa upande wa madaktari, je? wapo tayari kushikilia msimamo wao hadi mwisho bila kusalitiana endapo wataambiwa warudi kazini mmoja mmoja kwa kusaini makubaliano maalumu?

KITU KINGINE KILICHONISHANGAZA NI KWAMBA YALE MATANGAZO YALIYOKUWA YAMEBANDIKWA KWENYE NGUZO NA KUTA ZA HOSPITALI YA MUHIMBILI TOKA JANA NA ZIKASOMWA NA WATU WENGI WAKIWAMO WAGONJWA WENYEWE LEO HAZIPO! Nani kuziondoa? Ni Njelekela? Ni wagonjwa? Ni usalama wa taifa? au ni upepo ulioambatana na mvua kali? Na kama serikali itaendelea kutumia hizi mbinu za kitoto na za zamani kuzima na kuzuia taarifa kuwafikia wananchi mfano kubandua matangazo yaliyobandikwa na MAT, je tutafika? Na kama hali yenyewe ya utatuzi wa matatizo ni kuondoa matangazo yanayopasha wananchi ukweli wa kwa nini madaktari wanagoma, je? serikali ina nia ya dhati kusuluhisha mgogoro huu au ndiyo inachochea?

WAKUU NAOMBA TUJADILI HAYA MAMBO KWA KINA BILA KUELEMEA UPANDE WOWOTE ILI UKWELI UJULIKANE.

Kwa huu mgomo wa safari hii madaktari wamechemka, ule wa kwanza niliwa support, ila huu wa sasa wamechemka ile mbaya, rudini kwenye meza ya mazungumzo

tuko wengi tunao[pinga huu ufi.......r...u....ni ndio maana amesema sisi...pia ni busara kutumia neno sisi badala ya mimi.

Ni "wewe" sio sisi bwana mbona mimi naunga mkono mgomo usitulazimishe matakwa yako.
 
Kwa huu mgomo wa safari hii madaktari wamechemka, ule wa kwanza niliwa support, ila huu wa sasa wamechemka ile mbaya, rudini kwenye meza ya mazungumzo

wakae meza moja na nani?.......huyu pinda huyu muongo kama nini
 
Kwa huu mgomo wa safari hii madaktari wamechemka, ule wa kwanza niliwa support, ila huu wa sasa wamechemka ile mbaya, rudini kwenye meza ya mazungumzo

Mgomo huu Serikali ndiyo imechemka kabisa. Ule wa kwanza sikuuafiki maana walikuwa hawajawekeana makubaliano, ila huu nauunga mkono 100%. Serikali hii inaendeshwa kiuongo uongo sana na propaganda lukuki. Inaonekana Watanzania wengi tumeshazoea kupewa ahadi za uongo ndiyo maana sasa tunaona Madaktari wanakosea. Kwanini Serikali (Mh. Pinda) aseme uongo kila mara????? Tumechoka usanii huu.
 
Nimetoka muhimbili asubuh,madaktari walikuwepo

Unaongelea madaktari au wafanyakazi wa Muhimbili? Maana wengi wanaamini kila mfanyakazi wa Muhimbili ni Daktari.

Amini usiamini huu mgomo upo sana. Subiri utaona. Ndio kwanza umeanza leo mpaka Serikali itambue tumedhamiria.....
 
[

Mgomo wa madaktari uliomalizika hapo juma na unaoendeleo hata leo wahusishwa na udini kuwa eti Dr haji mponda anashinikizwa kujiuzulu maana ni muislam na wanasema hawa wanaharakati hawafai maana wanaibua mambo katika sekta ambazo waislam wamezishkilia na wanadai kuwa watakuja hata kumshinikiza rais Jk kujiuzulu manake nchi haita tawalika na wanasema pia waislam wanaonewa sana hata katika elimu manake waziri wa elimu ni mkiristo. Wamesema wanaandaa maandamano makubwa kupinga mgomo wa madaktari na kuwapinga hawa wanaharakati maana watakuja sababisha nchi isitawalike. Source radio imani asubui hii

Hiyo Radio ina laana toka kwa mwenyezi Mungu.

(1) Aliyekwambia kuwa Madakitari wote ni Wakristo NANI.

(2) Alikwambia kuwa Wanaharakati wote ni Wakristo NANI.

MTALAANIKA WOTE PAMOJA NA HIYO RADIO MNAOZUSHA KUHUSU UDINI KATIKA SUALA HILI LA MGOMO WA MADR.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
mimi naishi na jamii na ninasaidia watu wenye matatizo na shida mbalimbali

wewe weka hapa kiasi unachochangia ndipo nami ntaweka.

mwisho haya uliyoniuliza ni nje ya mada tunayoijadili sijui umeamka saa ngapi au bado unaamka amka kwa hiyo usingizi haujaisha vizuri
mimi sichangii sana mkuu japo nilitamani sana na ningependa kufanya hivyo, lakini madakitari wnanafanya hivyo kiasi mtu anavyoshindwa kutambua mchango wao ndio inanichukulia mimi kukuandikia hata hayo nisiyostahili kukuandikia!

Madaktari wapo kwenye mgomo hakuna atayekutibu utindio wa ubongo
Na Lucy NKYA, BLANDINA NYONI na DEO MTASIWA ni waislam? Na Madaktari wote waislam wapo kazini? Leo mmelikoroga na lazima mlinywe!! MMezoea propaganda za kidini na hili halitawagawa madaktari!!! Timizeni matakwa ya madaktari yaishe!!
 
Kwa huu mgomo wa safari hii madaktari wamechemka, ule wa kwanza niliwa support, ila huu wa sasa wamechemka ile mbaya, rudini kwenye meza ya mazungumzo

WAMECHEMKAJE mkuu?Kumbuka huyu huyu pinda ndiye aliwapiga mkwara kuwa atawatimua kazi kama wataendelea kugoma na hakufanya hivyo. Badala yake alikuja kuwalilia na kuwabembeleza warudi kazini! Hivi mnakumbuka kila kitu alikuwa anakkita cha kwake pale CPL? Mfano:MADAKTARI WANGU, WAGONJWA WANGU, HOSPITALI ZANHU,MAWAZIRI WANGU n.k!!!!!!!!!!!!!!! MNAKUMBUKA HAYA wanaJF mnaoleta taarifa za upotoshaji kuwa madaktari wako wrong? Nauliza tena,MNAKUMBUKA VILE AMBAVYO PINDA ALIWALILIA MADAKTARI?Na akaahidi kuwa atatekeleza makubaliano yele mara moja lakini sharti kwanza warudi kazini?

SASA imekuwaje jana anaenda kwenye MEDIA kuongea maneno ambayo yaashiria kuwa hana mpango wa kutimiza yale aliyoahidi? Lakini pia unaposema kuwa madaktari wamekosea na warudi kwenye meza ya mazungumzo,hivi unafikiri ni rahisi kiasi hicho?Yaani umemkamata mwizi halafu unampeleka polisi akashtakiwe and then kule mahakamani huyo mwizi anageuka kuwa hakimu, je? kuna fair play hapo? unafikiri utatendewa haki?
By the way nyie akina MAMA POROJO,INAUMA n. ambao mko kinyume na ukweli huu, ARE YOU OUT OF YOUR MIND? ARE YOU INSANE? ARE YOU DREAMING IN A SUNNY DAY? YOU MUST BE JOKING my friends!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hata Mponda na Nkya wakiondolewa, mgomo uendelee hadi Pinda nae ajiuzulu...
 
Mgomo wa madaktari unahusishwa na udini

|9:11 AM|Pendael laizer|

Mgomo wa madaktari uliomalizika hapo juma na unaoendeleo hata leo wahusishwa na udini kuwa eti Dr haji mponda anashinikizwa kujiuzulu maana ni muislam na wanasema hawa wanaharakati hawafai maana wanaibua mambo katika sekta ambazo waislam wamezishkilia na wanadai kuwa watakuja hata kumshinikiza rais Jk kujiuzulu manake nchi haita tawalika na wanasema pia waislam wanaonewa sana hata katika elimu manake waziri wa elimu ni mkiristo. Wamesema wanaandaa maandamano makubwa kupinga mgomo wa madaktari na kuwapinga hawa wanaharakati maana watakuja sababisha nchi isitawalike. Source radio imani asubui hii

Teh teh teh!Ukisikia divide and rule ndiyo hii sasa!Wameshalipeleka kwenye udini tena?
 
Nyie watu wa usalama wa Taifa acheni ushenzi wenu wa kuoa taarifa potofu!!

Watu wa usalama wa taifa wapi hao mkuu?hao ni kula kulala form four failures wapo wapo tu nyumbani,wewe angalia comment zao tu utawajua ni kula kulala
 
UPDATE

Habari nilizozipokea sasa hivi kwa njia ya SMS kutoka kwa doctor mmoja pale Mhimbili zinasema hivi,nanukuu,"Hii ya sasa ni bab kubwa responce ni 100% MPAKA EMERGENCY,intern ndio wamemaliza kikao chao cha kupeana moyo na specialist ndio wanaanza Russian culture nw..together we can make it" mwisho wa kunukuu sms niliyoipokea.
My take hivi serikali ina shindana na madaktari kwa ajili ya maslahi ya kisiasa? au inatakiwa kulinda afya za wananchi wake?
Maana kama mawaziri wamelalamikiwa na ni kweli wameshindwa kuwajibika kwa nini waendelee kuwepo hapo?na je inawezekanaje kupokea malalamiko ambayo kimsingi wao ndio wanalalamikiwa na kisha wakayafanyia kazi?
 
Hiyo Radio ina laana toka kwa mwenyezi Mungu.

(1) Aliyekwambia kuwa Madakitari wote ni Wakristo NANI.

(2) Alikwambia kuwa Wanaharakati wote ni Wakristo NANI.

MTALAANIKA WOTE PAMOJA NA HIYO RADIO MNAOZUSHA KUHUSU UDINI KATIKA SUALA HILI LA MGOMO WA MADR.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Hiyo radio ina matatizo na ni ya uchochezi,hv waziri wa elimu ni nani?
 
Back
Top Bottom