Insights muhimu kuhusu mgomo wa madaktari leo 7/03/2012

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Wakuu wanaJF

Leo ndiyo ile siku ambayo madaktari waliweka wazi kuwa watagoma endapo serekali itashindwa kuwasimamisha kazi mawaziri wa afya. Napost uzi huu ili kujua hali ikoje kwa wale walio karibu na hospitali zetu hususan MUHIMBILI, KCMC, BUGANDO, DODOMA, MBEYA n.k,Je? Kuna madaktari kazini?

Na vipi wananchi wa kawaida wanasemaje kuhusu mvutano huu kati ya serikali na madaktari?
Lakini pia ikumbukwe kuwa waziri mkuu Pinda alipokuwa anaongea na madaktari tar 9/02/2012 pale CPL MNH aliwaahidi wananchi kuwa serikali ina nia ya dhati kutatua mgogoro kwenye sekta ya afya na kwa kuanza akawasimamisha Blandina Nyoni( aliyeteuliwa na kuapishwa na rais) na Deo Mtasiwa( sina uhakika aliteuliwa na nani labda mnisaidie).

Sasa kama pinda alimsimamisha kazi mteule wa rais ambaye ndiye mtendaji mkuu wa wizara na kusema kuwa atamshauri rais awafukuze mawaziri je?

1. kwa nini asiwe na mamlaka ya kuwasimamisha wateuele wengine wa rais ambao wako ofisi moja na katibu mkuu?
2. au hakushuri rais kama alivyo ahidi kufanya? Na kama ni hivyo ina maana aliudanganya umma hivyo anapaswa kujiuzulu mara moja kulinda heshima yake.
3. kama alimshauri rais halafu huyu bwana mkubwa akapuuzia pia anapaswa kuonesha nia yake ya dhati ya kuwatetea wanyonge kwa kujiuzulu maana amedharauliwa kupita kiasi.
4. kama madaktari wataendelea na msimamo wao wa kugoma hadi serikali iwafukuze mawaziri na serikali ikakataa kwa madai kuwa rais hafanyi kazi kwa shinikizo, je? serikali itaweza kuwafukuza madaktari wote na kuajiri wengine au itaendelea kuatimua wanajeshi kutibu raia?
5. Na vipi kwa upande wa madaktari, je? wapo tayari kushikilia msimamo wao hadi mwisho bila kusalitiana endapo wataambiwa warudi kazini mmoja mmoja kwa kusaini makubaliano maalumu?

KITU KINGINE KILICHONISHANGAZA NI KWAMBA YALE MATANGAZO YALIYOKUWA YAMEBANDIKWA KWENYE NGUZO NA KUTA ZA HOSPITALI YA MUHIMBILI TOKA JANA NA ZIKASOMWA NA WATU WENGI WAKIWAMO WAGONJWA WENYEWE LEO HAZIPO! Nani kuziondoa? Ni Njelekela? Ni wagonjwa? Ni usalama wa taifa? au ni upepo ulioambatana na mvua kali? Na kama serikali itaendelea kutumia hizi mbinu za kitoto na za zamani kuzima na kuzuia taarifa kuwafikia wananchi mfano kubandua matangazo yaliyobandikwa na MAT, je tutafika? Na kama hali yenyewe ya utatuzi wa matatizo ni kuondoa matangazo yanayopasha wananchi ukweli wa kwa nini madaktari wanagoma, je? serikali ina nia ya dhati kusuluhisha mgogoro huu au ndiyo inachochea?

WAKUU NAOMBA TUJADILI HAYA MAMBO KWA KINA BILA KUELEMEA UPANDE WOWOTE ILI UKWELI UJULIKANE.
 
Kimsingi cheo cha uwaziri mkuu kwa tanzania ni sawa na mamlaka ya marais wa nchi kama ujerumani, italia nk. yaani ni titular, na ktk utawala wa kikwete hili ndiyo limejidhihirisha wazi kabisa. Kila kiongozi aliyeko ktk ofisi ya umma ni mteule wa rais na uwepo wao madarakani ni kwa lengo la kulinda maslahi ya rais (sio nchi tena kama tulivyozoea baadhi ya awamu zilizopita), huo ndiyo ugumu mkubwa wa utendaji kazi mzuri ktk awamu ya nne ya nchi hii.

Endapo madaktari wataamu kurudi kazini kwa namna yoyote ile bila kutimiziwa masharti yao watakuwa wamejidhalilisha sana na kuipa kichwa serikali hii ya sasa, maana walimu walishashindwa kitambo ingawa madhara yake tunayaona ktk ubora wa elimu.

Utamaduni wa kujiuzuru ulishazikwa zamani sana ndani ya utawala wa awamu ya nne. Kwa uchafu na uozo uliomo kwa watawala wote hautoi ushawishi wa mtu kufanya hivyo kwa kuwa kila anayemuangalia mwenzake haoni tofauti. Mbaya zaidi hata mkuu wa kaya mwenyewe huwa hajui kama mteule wake anakosea au anapatia.
 
madaktari ni lazima na wanapaswa rejea kazin PUNDE.. PERIOD.
 
roho za watu kwanza kingine baadae hivi mfano wewe ni daktar kunachupa za maji 10 wagonjwa wanaohitaji kuwekewa maji ni 12,UTASEMA UNAGOMA WAFE WOTE KISA CHUPA ZAMAJI CHACHE??? AU UTAWANUSURU WALE 10,KAMA SI BANGI NINI?
 
Leo niko hapa kurusha makombora kwa MADAKTARI kwa kla post inayowahusu...
Nasema hvi MADOKTA acheni uff***uni

Data tuko pamoja, na mimi niko online fully charged kuhakikisha mafaktari hawaidhalilishi serikali yetu.
 
Back
Top Bottom