Insha Maridadi: Watoto Mayai na Maswali ya "Why, Why, Why"!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Na. M. M. Mwanakijiji

Miaka ile ya zama zile, ile miaka ya wakati ule ambao mambo ya aina ile na ile yalikuwa in ya kawaida hatukupenda sana kucheza na wale waliojulikana kama "watoto mayai". Labda msemo huu umepotea kwa wengi lakini kwa ufupi watoto mayai walikuwa ni wale watoto ambao walikuwa wamedeka wakadeka halafu wakapitiliza hadi kudekeka.

Watoto hawa walikuwa ni wale ambao mkicheza mpira - cha ndimu - au hata "tiara bado" wao walikuwa wa kwanza kulia "nimeumia". Yaani, hakuhitaji kupigwa ngwala; tishio la kupigwa ngwala tu mtoto wa watu alianguka chini na kuanza kulia. Ilikuwa ni kero sana kucheza mchezo wowote na watoto 'mayai'.

Wengine wa watoto hawa walikwazika kwa maneno tu; yaani ukimfokea kidogo tu uso unamuanguka, anajihisi kuumia moyoni, na anajiuliza kwanini yeye anaonewa hivyo. Mtoto mayai hakuhitaji kufokewa, kukemewa wala kukataliwa. Kila anachotaka ilibidi apewe na asipopewa atanuna hadi mvua inanyesha! Siyo tu walidekezwa na wazazi na familia zao hata jamii za karibu zilijikuta zinalazimika kuwadekeza kwani wakiangusha kileo unaweza kufikiria ameangukiwa na contena la vyuma!

Naogopa sana kuwa inawezekana utawala wa mfumo wa kifisadi uliozaliwa, kukomaa na kukua katika uongozi wa Chama cha Mapinduzi ulitujengea taifa la watu waliodeka wakadekeka. Mfumo huu wa kifisadi ulijenga taifa la watu waliodekezwa ambao hawakujua kukataliwa, kufokewa, kuulizwa na wala kubanwa. Watu walizoea maneno ya upole, ya kubembelezwa na kuchekewa wakati wanakemewa. Watu hao ukiwakunjia ndita tu walianza kuangusha vilio!

Katika mazingira yale, watu hawakuwahi kufikiria kuishi kwa mapato halali, wala kudhania wanaweza kufanya kazi halali na kuweza kujipatia kipato halali. Leo hii wapo watu wanapata shida sana kila ikitokea kupanda na kushuka kwa thamani ya fedha, wanapata shida kila mvua ikichelewa kunyesha kidogo, wanapata shida kila wakiona mawingu kwani wanadhania ni gharika inakuja na kila jua likiwaka wanahofia ukame! Ndugu zetu hawa wakiona upepo umeongeza kasi kidogo wanahofia ujio wa kimbunga na dimbwi likianza kujaa maji wanaanza kulia "mafuriko" na wengine watasema ni "gharika".

Ndugu zangu, tumefika mahali hadi inabidi kujiuliza kama ni kweli watu wanapokosoa wanakosoa kwa sababu za ukweli kabisa au ni kwa sababu ya kutoka mazoea ya aina moja na sasa ni mazoea mengine? Hivi ni kweli kabisa watu wanaamini ili uchumi uende vizuri basi shilingi isibadilike hata chembe, bei ya vitu isipande na kusikuwepo kabisa mfumo wa bei? Kwamba, shilingi ikishuka dhidi ya dola, bei za vitu zikipanda na ukiwepo mfumuko kidogo wa bei basi ni kiama? Kwamba, sasa uchumi una hali mbaya, taifa linaenda kuangamaia?

Hivi ndugu zetu hawa kama ikitokea wakapata madaraka wanataka kutuambia kuwa katika miaka yao yote watakayokuwa madarakani, bei za vitu hazitabadilika, thamani ya shilingi itapanda tu hadi iwe karibu ya dola moja kwa shilingi moja? Kwamba, wakati wa utawala wao wenzetu hawa, mvua zitanyesha, mavuno yatakuwepo , na kila mtu atakula na kusaza? Kwamba, wao wakishika madaraka mapato yatakuwa ya uhakika wakati wote, na kila tatizo la kijamii na la kiuchumi linaloikabili Tanzania litatatuliwa ndani ya miaka miwili tu ya utawala wao?

Ndugu zangu, haina maana mtoto mayai hatakiwi kulalamika. Ni kweli wakati mwingine wanaumia kweli lakini kwa tunaojua watoto mayai tunajua kabisa, watoto mayai wakiumiwa kweli au wakikutwa na baya la kweli hawalii kama wanaojisingizia, watalia na utajua kweli hawa wameumia.

Tatizo ni kuwa kumeanza kuwepo na dalili ya kuwepo kati yetu watu ambao wako kama yule mtoto aliyelia "mbweha, mbweha" wakati hakukuwepo na mbweha. Alilia hivyo kwa sababu alikuwa ameboreka kukaa kuchunga peke yake. Mwisho wa siku alipolia "mbweha" wakati mbweha kweli alitokea watu walisitia kukimbia kumsaidia kwani walijua anafanya utani wake tena!

Tusitengeneza taifa la watoto mayai, ambao hawataki kutoka jasho, hawataki kukemewa, hawataki kukataliwa, na hawataki kuambiwa. Na wale walioko madarakani na wao wasiwe kama watoto hao hao. Taifa zima la wananchi na viongozi wake wakiwa watu waliodeka na wanaodeka litakuwa ni taifa lililogumu sana kulijenga upya.

REJEA MADA HII YA 2012:
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Mwaka huu usipopewa hata Ukuu wa wilaya na Magufuli basi nitashangaa sana. Maana wale washindani wako wengine wote umewaacha mbali sana, hasa hasa...
1/Jerry Muro.
2/Fred Mpendazoe.
3/Rais wa bao wa ITV Kipimajoto.
4/Askari mstaafu wa ITV kipimajoto.
5/Sam Mahela.
6/Pascal Mayalla.
 
Watoto mayai wameshindwa kupambana bongo nakukimbilia kwa wazungu!
Watoto mayai wanafundisha na kulipwa laki 3 na kuchangia mwenge!
Watoto mayai hata nyongeza zao za kisheria za mishahara hawadai!!
Watoto mayai wanamlaani Trump anayetaka kuwarejesha kwenye vumbi na ugali wa uwele/ulezi!
Watoto mayai mbona tupo kibao?
 
Watoto mayai wanajijua kuwa wao ni watoto mayai?
Na. M. M. Mwanakijiji

Miaka ile ya zama zile, ile miaka ya wakati ule ambao mambo ya aina ile na ile yalikuwa in ya kawaida hatukupenda sana kucheza na wale waliojulikana kama "watoto mayai". Labda msemo huu umepotea kwa wengi lakini kwa ufupi watoto mayai walikuwa ni wale watoto ambao walikuwa wamedeka wakadeka halafu wakapitiliza hadi kudekeka.

Watoto hawa walikuwa ni wale ambao mkicheza mpira - cha ndimu - au hata "tiara bado" wao walikuwa wa kwanza kulia "nimeumia". Yaani, hakuhitaji kupigwa ngwala; tishio la kupigwa ngwala tu mtoto wa watu alianguka chini na kuanza kulia. Ilikuwa ni kero sana kucheza mchezo wowote na watoto 'mayai'.

Wengine wa watoto hawa walikwazika kwa maneno tu; yaani ukimfokea kidogo tu uso unamuanguka, anajihisi kuumia moyoni, na anajiuliza kwanini yeye anaonewa hivyo. Mtoto mayai hakuhitaji kufokewa, kukemewa wala kukataliwa. Kila anachotaka ilibidi apewe na asipopewa atanuna hadi mvua inanyesha! Siyo tu walidekezwa na wazazi na familia zao hata jamii za karibu zilijikuta zinalazimika kuwadekeza kwani wakiangusha kileo unaweza kufikiria ameangukiwa na contena la vyuma!

Naogopa sana kuwa inawezekana utawala wa mfumo wa kifisadi uliozaliwa, kukomaa na kukua katika uongozi wa Chama cha Mapinduzi ulitujengea taifa la watu waliodeka wakadekeka. Mfumo huu wa kifisadi ulijenga taifa la watu waliodekezwa ambao hawakujua kukataliwa, kufokewa, kuulizwa na wala kubanwa. Watu walizoea maneno ya upole, ya kubembelezwa na kuchekewa wakati wanakemewa. Watu hao ukiwakunjia ndita tu walianza kuangusha vilio!

Katika mazingira yale, watu hawakuwahi kufikiria kuishi kwa mapato halali, wala kudhania wanaweza kufanya kazi halali na kuweza kujipatia kipato halali. Leo hii wapo watu wanapata shida sana kila ikitokea kupanda na kushuka kwa thamani ya fedha, wanapata shida kila mvua ikichelewa kunyesha kidogo, wanapata shida kila wakiona mawingu kwani wanadhania ni gharika inakuja na kila jua likiwaka wanahofia ukame! Ndugu zetu hawa wakiona upepo umeongeza kasi kidogo wanahofia ujio wa kimbunga na dimbwi likianza kujaa maji wanaanza kulia "mafuriko" na wengine watasema ni "gharika".

Ndugu zangu, tumefika mahali hadi inabidi kujiuliza kama ni kweli watu wanapokosoa wanakosoa kwa sababu za ukweli kabisa au ni kwa sababu ya kutoka mazoea ya aina moja na sasa ni mazoea mengine? Hivi ni kweli kabisa watu wanaamini ili uchumi uende vizuri basi shilingi isibadilike hata chembe, bei ya vitu isipande na kusikuwepo kabisa mfumo wa bei? Kwamba, shilingi ikishuka dhidi ya dola, bei za vitu zikipanda na ukiwepo mfumuko kidogo wa bei basi ni kiama? Kwamba, sasa uchumi una hali mbaya, taifa linaenda kuangamaia?

Hivi ndugu zetu hawa kama ikitokea wakapata madaraka wanataka kutuambia kuwa katika miaka yao yote watakayokuwa madarakani, bei za vitu hazitabadilika, thamani ya shilingi itapanda tu hadi iwe karibu ya dola moja kwa shilingi moja? Kwamba, wakati wa utawala wao wenzetu hawa, mvua zitanyesha, mavuno yatakuwepo , na kila mtu atakula na kusaza? Kwamba, wao wakishika madaraka mapato yatakuwa ya uhakika wakati wote, na kila tatizo la kijamii na la kiuchumi linaloikabili Tanzania litatatuliwa ndani ya miaka miwili tu ya utawala wao?

Ndugu zangu, haina maana mtoto mayai hatakiwi kulalamika. Ni kweli wakati mwingine wanaumia kweli lakini kwa tunaojua watoto mayai tunajua kabisa, watoto mayai wakiumiwa kweli au wakikutwa na baya la kweli hawalii kama wanaojisingizia, watalia na utajua kweli hawa wameumia.

Tatizo ni kuwa kumeanza kuwepo na dalili ya kuwepo kati yetu watu ambao wako kama yule mtoto aliyelia "mbweha, mbweha" wakati hakukuwepo na mbweha. Alilia hivyo kwa sababu alikuwa ameboreka kukaa kuchunga peke yake. Mwisho wa siku alipolia "mbweha" wakati mbweha kweli alitokea watu walisitia kukimbia kumsaidia kwani walijua anafanya utani wake tena!

Tusitengeneza taifa la watoto mayai, ambao hawataki kutoka jasho, hawataki kukemewa, hawataki kukataliwa, na hawataki kuambiwa. Na wale walioko madarakani na wao wasiwe kama watoto hao hao. Taifa zima la wananchi na viongozi wake wakiwa watu waliodeka na wanaodeka litakuwa ni taifa lililogumu sana kulijenga upya.

REJEA MADA HII YA 2012:
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Hii kweli insha tena ni zile waswahili wanaita insha za wasifu wala siyo za hoja, insha za kupamba na kutetea jambo bila kuonesha upande wa pili very biased.

No wonder insha za Jerry Muro zinapata mvuto na kuvutia wachangiaji kuliko hizi zako. Hii ni dalili kuwa huko Lumumba umegeuka liability pia.
 
Hawakawii kukuteka na kukutesa au hata kuanza kukuwinda na mitutu yao ya SMGs kisa umewakosoa!!!
Hahaha! Nguvu ya dola ndiyo kimbilio la kwanza hao ndiyo watoto mayai orijino wanalindwa zaidi ya watoto wa geti kali hawatakiwi kunyooshewa kidole wala kuguswa yaani wanataka watudanganye kuwa uchumi, umepanda wapike data sisi tu celebrate.
Kama uchumi kushuka na thamani ya fedha kushuka ni kawaida kwanini wapike data au waongee uongo? Huu siyo utoto mayai kutaka uonekane mwema tu? Na ndiyo maana haya mambo yanaongelewa kwa sababu ni inaonekana yanafichwa sana hivyo yana impact yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom