Injinia Stella Manyanya alifunda jiji la Dar kiaina!

Manyanya alijafanya mpambanaji wa ufisadi, na hali na yeye fisadi vilevile!

vipi katika hili la upambanaji wake katika uchafu?huoni kama ni mfano wa kuigwa na nyie huko mliko muache kupenda uchafu kuliko usafi na kuanzisha vita ya makusudi dhidi ya uchafu?kila siku ufisadi ufisadi wakati miji yetu pia ina uchafu!
 
Huyu mama amesaidia vipi katika profession yake kwani huyu mama alikuwa kwenye shilika la Megawatt kabla hajaikimbia profession yake, ningempa credit kama angeenda kusaidia mafundi umeme kufanya connection kwenye nyumba zao, kufagia kila mtu anaweza kufanya hivyo na angeweza hata kuajili watu wangefanya kazi hiyo, sasa fuatilia ni kiasi gani cha fedha kimetumika kwenye tukio la huyo Engineer kufagia.

Haiwezekani watu wote wakafanya kazi za umeme,kuna sekta nyingine pia zinahitaji watu...tuichukue hii kama challenge na tuifanye miji yetu mikubwa ing'are kama sumbawanga,inawezekana tukiacha politics na kuamua kufanya kazi sasa
 
Kwanini afagie mbele ya makamera kama ni mtu wa kazi?
Wanaofagia wapo mabarabarani bana, hawahitaji camera ya mtu wala nini!..Jua lao mvua yao!
Acheni unafiki usio na ishu!..
 
Kama hawajui wafagia barabara mwambieni atazame hawa hapa!
Si vizuri kuigiza kazi za watu na makamera ya video ...thats hypocricy!

kufagia barabara.jpg
 
Kwanini afagie mbele ya makamera kama ni mtu wa kazi?
Wanaofagia wapo mabarabarani bana, hawahitaji camera ya mtu wala nini!..Jua lao mvua yao!
Acheni unafiki usio na ishu!..

Yeye anchofanya ni kuamsha ari kwa kila mtu kwenye eneo lake ajenge tabia ya kufanya usafi,yeye kama kioo cha jamii akionekana anafanya ni rahisi watu anawaowaongoza kumuiga so publicity ilikua ni muhimu sana hapo ili ujumbe ufike mbali,kumbuka yeye hawezi kwenda kila kata kuonyesha mfano huo wakati tecnolojia ya kuifikia kila kaya ipo...hao viongozi wenu wa dar hata kuthubutu hawajawahi licha ya jiji zima kutoa harufu ya uvundo kutokana na uchafu
 
Anatafuta umaarufu wa kisiasa ili Jk akaone one, Juzi kati kakihojiwa Sumbawanga tv live kalinibore sana kalivoanza kupiga proganda za kisiasa, kanaulizwa kanaonaje kuhusu mchakato wa katiba, badala ya kujibu hoja kakajaa upepo na kuwagekia CDM oh mara wahuni, wanamambo ya kitoto!!!, hafu kanajifanya kajuaji sana, kimsingi manyanya ni mnafiki sana hakafai aisee! Kuhusu tukio zima unalokomaa nalo nasema kwangu mimi is an issue kwangu kwa nimjuavyo Manyanya majibu yangu yale yale ni kanafiki sana
kwanini?mbona hamuongelei hilo tukio zima mnaenda personal kwa mama?
 
Anatafuta umaarufu wa kisiasa ili Jk akaone one, Juzi kati kakihojiwa Sumbawanga tv live kalinibore sana kalivoanza kupiga proganda za kisiasa, kanaulizwa kanaonaje kuhusu mchakato wa katiba, badala ya kujibu hoja kakajaa upepo na kuwagekia CDM oh mara wahuni, wanamambo ya kitoto!!!, hafu kanajifanya kajuaji sana, kimsingi manyanya ni mnafiki sana hakafai aisee! Kuhusu tukio zima unalokomaa nalo nasema kwangu mimi is an issue kwangu kwa nimjuavyo Manyanya majibu yangu yale yale ni kanafiki sana

ahaaaa!ndio mana kumbe tulikua hatuelewani kumbe wenzangu mko kwenye politics za ccm na cdm! hapo itakuona ngumu kweli kuona lolote zuri,hata ningekua mimi,hapo nimewaelewa wandugu,basi yaishe bana!ndio maana nchi zinazotawaliwa na madikteta bila opposition zinasonga mbele!
 
Kama hawajui wafagia barabara mwambieni atazame hawa hapa!
Si vizuri kuigiza kazi za watu na makamera ya video ...thats hypocricy!

View attachment 45256

Yani watu wa dar mnashindwa na watu wa sumbawanga kwa vitendea kazi vya usafi jiji lenu na watu wenu wa usafi wamechoka namna hiyo,nendeni mkajifunze sumbawanga kusafisha jiji lenu chafu
 
Kardash!
Kwanza nani alikuambia Stella ni Engineer? Alimaliza pale Dsm Technical college 1990 Kama sijakosea na ule mtihani wa Advanced Diploma walifeli wengi tu na kwa ukabila aliajiriwa Tanesco. Huo uinjinia aliupata kutoka Engineers Registration Board kwa kufanya mtihani wake fake atuonyeshe statement of results za chuo alichosoma apart from huo upuuzi wa ERB anawajua wenzake wote walijipatia uinjinia haramu. Pili kufagia Barabara ni kuonyesha cheap politics huo upuuzi walishafanya wengi hapa Tanzania na Afrika lakini yote yanaishia ukungoni. Kwa Serikali makini ni kuweka mfumo thabiti na ufuatwe. Manispaa ya Moshi ni safi lakini Mkuu wa mkoa hajashika fagio. Usafi ni attitude of the mind lazima wananchi waelimike na kukubali kubadilika na mamlaka zilizopo ziweke kanuni na sheria ndogo ndogo na kuzisimamia pronto! Kiwango cha elimu ya jamii husika ndiyo yardstick. Kama umasikini na elimu ni duni then uchafu kwenye hizo sehemu ndiyo taswira inayokubalika Kama ilvyo kwa jiji la uchafu Dar es salaam. TANU ilwahi kuja na sera ya kilimo cha kufa na kupona matokeo yake wapumbavu wakaanza kulima mahindi kwenye bustani za nyumba Kule Oysterbay huku wakivunja city by laws zilizowekwa na wakoloni as a result mbu wakazaliana kibao na hadi awamu hii ya nne ya CCM bado malaria ni tatizo kubwa. For a quick fix JK wanagawa chandarua na hati punguzo. This is just another crazy gang narudia bora ukoloni urudi rasmi huu wa uwekezaji is very stupid bora jumla!:A S 465:
 
Hii ya mbu na chandarua nakubaliana na wewe hata mimi huwa sielewi kwanini viongozi wetu wameaminishwa na wamerakani kwamba dawa ya mbu ni kujificha kwenye vyandaru,hii sio kweli.

Lakini anachofanya stella tukiacha huo uinjinia wake ambao unadai una utata yuko sahihi,hapo kama kiongozi anaonyesha njia na kutoa hiyo elimu ya usafi kwa njia ya vitendo,hii naona kaiiga kwa kagame ambae amefanikiwa sana,hakuna ubaya kuiga jambo zuri,leo rwanda nimesoma huko mwanzo kila mtu anajua umuhimu wa kutunza mazingira,na stiil bado kuna siku maalum ya usafi kila wiki jmosi watu wanavaa tshirt na jeans na kwenda makazini kushiriki shughuli za usafi wa mazingira,kwa hili stella asipingwe aungwe mkono ili awaambukize na viongozi wengine katika mikoaa yao then tuone tutafanikiwa vipi,tukimkatisha tamaa uchafu kwenye miji yetu hasa dar itakua ni never ending story mazee! kipindu pindu na magonjwa mengine yanayotoka na uchafu hayachagui huyu ni ccm,nccr,cuf ama cdm!
 
vipi katika hili la upambanaji wake katika uchafu?huoni kama ni mfano wa kuigwa na nyie huko mliko muache kupenda uchafu kuliko usafi na kuanzisha vita ya makusudi dhidi ya uchafu?kila siku ufisadi ufisadi wakati miji yetu pia ina uchafu!
asafishe uchafu wa ndani.
 
Hizi siasa zetu zilivyo, hata professional unaipiga chini halafu unabanjuka kwa kwenda mbele
 
Kwanini afagie mbele ya makamera kama ni mtu wa kazi?
Wanaofagia wapo mabarabarani bana, hawahitaji camera ya mtu wala nini!..Jua lao mvua yao!
Acheni unafiki usio na ishu!..

Hata mavazi yake tu hayaoneshi kama alijiandaa kufanya kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom