Elections 2010 Injinia Humphrey Tuni wa Chadema amwendesha Agrrey Mwanri wa CCM puta jimbo la Siha

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Leo nipo jimbo la Siha na hali siyo nzuri hata kidogo kwa mgombea wa CCM ambaye ni naibu Waziri serikali za mitaa: Mheshimiwa Aggrey Mwanri hivi sasa anapumulia kwa mashine na yaelekea ataanguka vibaya sana kutokana na wananchi kumchoka. Tuhuma za kujinyakulia mashamba yeye na swahiba zake ni kero kubwa huku. Uendeshaji wa halmashauri usiozingatia maadili nao kuna msuta Mheshimiwa huyu ambaye ni kipenzi cha JK.

Wapigakura ambao wengi wao ni vijana hawana ajira na wanakerwa na tabia ya Mbunge wao kutoa kandarasi kwa wageni na wao kubaki kuishia kuwa watamazaji tu.

Pia kuna ile hali ya wapigakura kujiuliza hivi ni wewe tu hakuna mwana Siha mwingine anayeweza kuliongoza jimbo? Ni maswali ambayo Mheshimiwa Mwanri mpaka sasa hana majibu hata kidogo

Mgombea wa Chadema aitwaye Injinia Humphrey Tuni yaelekea ndiyo chaguo la wengi huku. NEC wasiporuhusu wapigakura kuwepo mita 200 kutoka katika vituo vya kupiga kura na matokeo yakachakuchuliwa vurugu zitaweza kutokea.
 
Chadema Goooo, hakuna kurudi nyuma. Tunahitaji wachapakazi siyo hawa watani zetu wanafanya umimi na urafiki kila sehemi bila kusoma wakati. we are in 21 century lakini viongozi wengi wa ccm hawana creativity zaidi ya kuendelea kukaribisha wageni wajinemeeshe.
 
Hapo mimi ninkubaliana nawe hata ukienda kule kibong'oto ambapo amejenga hekalu lake asilo ishi ameweza kununu ardhi ya majirani zake kwa hela kiduchu na kupanua wigo wa himaya yake. Aggrey ni mbinafsi na mpiga kelele za kijanjajanja tu." Kunu kwehu" siha sasa muda wenu wa kuamka umefika.
 
Akabwe zaidi hadi mambo yaharibike!! Tumewachoka!!! aargu!!
 
Watu wa Siha pigeni kampeni ya mtu kwa mtu dk za mwisho hizi mpaka kieleweke hawa warafi tumewachoka
 
watu wa vijiji vya serengeti wanahitaji picha za slaa wadau mlioko hujo shughulikieni suala hilo
 
Wakuu zangu,

Mwanri ni mmoja wa viongozi ambao mimi nawapitisha. Uwakilishi wake kama Mbunge kusema kweli siufahamu lakini kama kiongozi na waziri bila shaka huyu ni mmoja wa viongozi ambao mimi nawapitisha. Swala la viongozi kuhodhi mali hadi sasa hivi sii kosa ikiwa zimepatikana kihalali na ndio maana tunaichagua Chadema ambao watabadilisha mfumo mzima wa kiutawala. Usimchague Mwanri ktk kinyang'anyiro cha Ubunge lakini pia tusimweke ktk kundi la Mafisadi..'cause he is not!
 
mwanri ameshindwa kutumia fursa zilizomo ndani ya wilaya na jimbo lake kuwakomboa vijana,ukichukulia hata miongoni mwa milango ya kupandia mlima kilimanjaro ipo jimboni mwake na vijana bado masikini sana kama wa pale sanya juu
 
Wakuu zangu,

Mwanri ni mmoja wa viongozi ambao mimi nawapitisha. Uwakilishi wake kama Mbunge kusema kweli siufahamu lakini kama kiongozi na waziri bila shaka huyu ni mmoja wa viongozi ambao mimi nawapitisha. Swala la viongozi kuhodhi mali hadi sasa hivi sii kosa ikiwa zimepatikana kihalali na ndio maana tunaichagua Chadema ambao watabadilisha mfumo mzima wa kiutawala. Usimchague Mwanri ktk kinyang'anyiro cha Ubunge lakini pia tusimweke ktk kundi la Mafisadi..'cause he is not!

Wewe mwenyewe unakili kuwa mambo ya ubunge wake na kwao huyajui; sasa unapata wapi ujasiri wa kumtetea kuwa sio fisadi mtu ambae amenunua ardhi ya watu anaowawakilisha kwa bei ya kuwadhulumu!! Mali alizojilimbikizia hasa ardhi kule Siha havifanani na mapato yake ya kazini toka aajiliwe!! Yuhu ni mwizi kama walivyo wengine katika chama cha mafisadui!!
 
Huyo Tuni hasije akawa yule jamaa aliyeoa mtoto mkubwa wa kaka yake na Aggrey Mwanri. Maake huo ukoo una bifu kinoma baada ya Kaka yake Aggrey Mwanri (Ndaskoi Mwanri) kufariki. Yeye na ndugu yake wa Tanzania Breweries (Moshi) waliamua kuchukuwa nyumba za marehemu wakati watoto wa marehemu wakiwepo. Hizi familia haziongei, wanaonana tu kipindi kama kuna msiba, that is it.
 
Umechanganya mambo. Mada yenyewe umeielewa! Maana naona umekaa na kuinama. Au tuseme una maana Eng Tuni anapigania ubunge kumkomoa Mwanri kwa mambo aliyomfanyia marehemu kaka yake? au tufikiri vipi, maana hapa tunazungumzia utaifa na ubunge kati ya wagombea wawili hasa, yaani CCM na CHADEMA. Hakuna haja ya wananchi kumchagua mtu anayetaka kumwangusha mwenzie kwa sababu za kifamilia. Tunataka watu walio tayari kusukuma gurudumu la maendeleo. Unataka kusema nini?
 
Mwanzisha mada naomba uwe mkweli sio kuja huku kijiweni na kutoa picha ambaye itawamislead watu wengi wasiojua hali halisi ya jimbo na baadaye matokeo yakitoka watu wakaanza kushangaa. Tujaribu kuripoti ukweli wa mambo ulivyo.

Jimbo la siha limepata maendeleo makubwa mno miaka 10 iliyopita, ikiwemo barabara za lami, maji ambayo ilikuwa hadithi miaka yote toka uhuru, umeme wa uhakika unaopatikana karibu jimboni kote. Shule za msingi na sekondari zimeongezeka almost 10*, na zahanati na hospitali nazo zimeongezeka na kuimarishwa. Sisi tunaokaa huku Sanya juu kilimani nyumba zetu zina maji yanayotoka kwa uhakika kuliko hata Dar na umeme wa uhakika nao tunao.

Kikubwa kuliko vyote kilichofanyika ambacho wanaSiha wote wanakijua ni jimbo hili kupewa WILAYA mwaka 2005, kitendo ambacho kimeleta maendeleo makubwa mno kwenye hili jimbo(wilaya) last 5 yrs.

Jimbo linachangamoto zake kama ajira, umaskini wa watu hasa vijijini n.k. lakini hizi zote ni changamoto ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi.

Sasa mafanikio na matatizo yaliyopo, bado wananchi wananafasi ya kuchagua nani awaongoze.

Swali ni Je Mbunge Mwanri ambaye uchapakazi wake na ushirikiano na wananchi unafahamika au mpinzani wake??
Kwa ninavyolijua mimi jimbo na watu wake na mafanikio yaliyopo itakuwa miracle kwa uchaguzi kuwa close let alone Mwanri kushindwa.
 
WELL SAID... Kura kwa Mwanri ila kwenye Urais Kura kwa Dr.Slaa
 
Shida ipo kwa wakazi wa Siha kwani wana amini wakifanya mabadiliko watasuswa kama ilivyotokea 1995 walipo mchagua makidara NCCR-Mageuzi wakati huo likiwa jimbo moja Hai
hayayote yalifanyika kwa makusudi na serikali ya CCM Kwa kuinyima Halmshauri ya Hai miradi ya maendeleo. Kweli siha inahalmashauri yake ila bado haijatulia.
 
Uliyosema ni ukweli mtupu, lakini pamoja na hayo wananchi nao wanajua mbunge wao anavyopush serikali ili miradi siha itekelezwe na hayo yote alifanya wakati ni mbunge tu na hayuko serikalini.

Siha kupata wilaya ilikuwa ni kazi ya ziada ya mbunge na kwa kweli sisi wananchi tulijua ni ndoto na ahadi hewa ya mbunge wakati huo wanzoni mwa miaka ya 2000's. Siha ilikuwa haina kigezo kikubwa mno cha namba ya wananchi ili kukidhi kigezo namba moja cha kupata wilaya.

Ebu tumuulize mleta hii topic:::

Huyu kijana Tuni ataweza kufanya yapi kwa jimbo la Siha ambayo Mwanri hataweza?? Yaani Tuni ataleta maendeleo gani kwa wananchi ambayo ama Mwanri ameshindwa kuyaleta au atashindwa kushugulikia miaka ijayo??

Kununua viwanja ni makubaliano ya muuzaji na mnunuzi, sasa hata sioni tatizo liko wapi ikiwa mtu anauza kiwanja chake na mnunuzi akatokea kuwa mbunge, kuna kosa lolote??

Kuhusu wakandarasi nadhani hiyo ni kazi ya halmashauri ambayo madiwani wako karibu zaidi, of course mbunge naye anatakiwa apush ili wakandarasi ikiwezekana wawe local. Kuhusu ajira hiyo ni changamoto kubwa sana, lakini swali hapa ni Huyu Tuni wa Chadema ataweza vipi kutoa ajira kwa sisi vijana wa huku Sanya Juu??
 
Back
Top Bottom