Injini ya Treni na Meli, ni ipi yenye nguvu zaidi kuliko nyingine?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
2,939
517
Kuna taarifa kuwa injini ya treni ndio yenye nguvu kuliko injini zote za vyombo vya moto kama magari, ndege, meli, boti. vifaru.

Je, kuna ukweli wowote katika hili?
 
Yeah binafsi sidhani kama kuna nyingine yenye nguvu kama hayo madude, kuna yale yaliyokuwa na namba 88 halafu cjui ngapi ngapi huko zinaendelea, weeeeeeeh ni balaa
 
yeah binafsi sidhani kama kuna nyingine yenye nguvu kama hayo madude, kuna yale yaliyokuwa na namba 88 halafu cjui ngapi ngapi huko zinaendelea, weeeeeeeh ni balaa

yawezekana ikawa kweli maana utaona inavuta behewa kama 40 halafu lipo spidi sana
 
yawezekana ikawa kweli maana utaona inavuta behewa kama 40 halafu lipo spidi sana

Baba'ngu mkubwa alikuwa anasukuma hayo madubwana, aliwahi kusema kwamba kwa kawaida kabisa yanakuwa na uwezo wa kuburuza mzigo wa mabehewa 75, lakini kwa hapa kwetu inakuwa ngumu kutokana na miundombinu ya ujenzi wa reli inakuwa ni vigumu hata kwakati wa kupanga mabehewa na wakati mwingine kupishana kwny stations kama ikibidi
 
mkuu wewe unasemaje hapa

Naamini hata meli ni hatari. Kuna meli ikija inatapika magari na kontena kadhaa. Pamoja majini uzito hupungua lakini naamini meli kubwa za kubeba magari na kontena itazidi engine ya train.

Lakini pia mashine kubwa za viwanda kama cha cement, power plants, gas plants na nuclear plant! Kuna maviwanda ya metallurgy na foubdry vya kuyeyusha chuma nazo engine zake ni very powerful
 
yawezekana ikawa kweli maana utaona inavuta behewa kama 40 halafu lipo spidi sana

Kontena 40 ni chache sana. Hiyo ni karibu 1/38 ya kontena zinazobebwa na meli moja.

Lakini ndege aina ya AIRBUS, ANTONOV NA BOEING 767 zinapopaa zinatumia nguvu ya tani 700, yaani ile power itumikayo kuilift ndege ni ya tani 700 sawa na karibu Semi trailer 25 kwa mpigo zenye tani 20(almost) kila moja.
 
Mwenzako anasema behewa 40,wewe unaleta habari za contena40!!!.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom