Inglishi media "aka" saint nanihii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inglishi media "aka" saint nanihii

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Gamaha, Mar 24, 2010.

 1. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa watoto wote wa vigogo wa serikali na kampuni binafsi watoto wao wote wanasoma shule za english media AU saint nanihii, kwa kuwa hata wale wananchi wa dalaja la kati wanajitahidi kujinyima hata kile kidogo wanachopata ili mtoto wake akasome huko saint furani,

  Na hata wale wenzangu na mimi makabwela wanatamani saaaaaaaaaaaana watoto wao wakasome saint naniii ili angalau mtoto aweze kusema morning dady, momy, nakadhalika.

  Kwa ujumla siku hizi mtoto wa kitanzania akisoma english media anaonekana ni mtoto wa kileo, mtoto wa dalaja la juu, Je serikali inasita nini kubadilisha lugha ya kufundishia mashuleni ili kiwe kizungu na sisi watoto wetu watuite dady, uncle na mengineyo ya kizungu... situkuzi kizungu lkn kama kizungu ndio kinaonekana kuwa lugha ya kufundishia katika shule nyiiingi zinazochipukia sasa na ambazo ndio wenye pesa wote wanapeleka watoto wao huko.

  Kwa nini serikali haitufikilii sisi makabwela jamani, hii ya kuanza kutumia kizungu form one unakutana na wenzio walisha kitumia toka chekechea huko saint nanihii inaweka ka inferiolity furani hivi, na hata ukimaliza chuo kwenye interview zetu za kizungu mtu wa saint nanihii atakupita kwa sababu sisi wa tulioanza kusoma kizungu form one utabakia unatafuta neno gani utumie kujibu swali hata kama unalijua na unaishia kutupwa nje sababu tu ya kigugumizi cha kizungu.

  NATAMANI KWELI HATA WALE WA MANZESE PRIMARY SCHOOL WAFUNDISHWE MASOMO YOTE KWA KIZUNGU NA WAONGEE MASHULENI KIZUNGU ILI ANGALAU NGOMA IWE DROO. SITAKI KUSIKIA ETI BUDGET HAITOSHI YA KUBADILISHA MITAALA NA KUFUNDISHA WAALIMU MBONA PESA ZA UCHAGUZI MNAPATA, MBONA EPA MLIIBA.
   
 2. M

  Mwedi Member

  #2
  Mar 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Naunga mkono hoja,serikali iangalie uwezekano wa kubadilisha mitaala,mana hata hao wnaoidhinisha mitaala ya kiswahili ukweli huu wanaufahamu vyema,na ushahidi wa hilo ni kitendo chao(WOTE) Hao watunga sera/MITAALA watoto wao wote hawasomi shule za kiswahili Medium.
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Ngoma wajameni ni sisi walimu je kiinglish na sie twakiweza au ndio itakua square root is square root of the the the squre root iz you know square root yaani ndio nitazunguka hapoo mpaka kipindi kiishe. Lakini ni wazo zuri ati naunga mkono na mguu hoja
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mwedi...huenda una hoja nzuri lakini kuna mahali lugha yako yaweza kupotosha maana. Ukisema unatamani shule zote zifundishe masomo kwa kizungu kwa maoni yangu sio sahihi. Nadhani sahihi unatamani shule zifundishe masomo kwa lugha ya kingereza maana si kila mzungu anajua kingereza.....otherwise ni mtazamo mzuri.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Gamaha,

  Naunga mkono hoja yako kwa asilimia zote,Nadhani Tanzania inatakiwa /inahitaji kubadili mitahala ili lugha ya kufundishia masomo yote iwe ya kiingereza.Najua kubadili si jambo rahisi kulifanya kwa haraka lakini tunaweza tukaanza kwa baadhi ya mikoa [pilot project] na baadae tukaifanya kwa nchi nzima.

  Zipo sababu za msingi kabisa ambazo Tanzania haina njia ya mkato bali kukubaliana na hali halisi.Soko la ajira litakuwa moja kwa nchi wanachama wa EAC ifikapo mwezi July 2010,nchi za Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi zimewekeza na zinaendelea kuwekeza kwenye lugha ya kiingereza hivyo kuwafanya wananchi wake wawe katika nafasi nzuri katika soko la ajira.

   
 6. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,170
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Buhahahahahaha.,
  Lile tangazo la square root linanichekesha.

  Yaani ticha kipindi kinaanza mpaka kinaisha anaelezea square root na haeleweki. Mpaka madenti wakastuka ticha anawaibia!

  Hawa ndo walimu wetu.
   
 7. m

  mmlaponi Member

  #7
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapo umechemka sijakubaliana na hilo wazo!
  maana hilo wazo litazika kabisa lugha yetu ya taifa.
  mimi mwenyewe nimeshuhudia hao watoto wa saint naniihi wanavyochemsha katika lugha yetu ya taifa hivyo haina haja ya kubadili mitaala waache hao watoto wa vigogo wapotee hivyohivyo!
  don't worry wengi tumepitia shule zetu hizi hizi na bado tuko fiti kwenye hii lugha ya waingereza!
   
 8. Abraham

  Abraham Senior Member

  #8
  Mar 24, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hoja naiunga mkono 100% na nashauri watunga mitaala wasiogope kwani mwanzo mgumu. Hata kama walimu wanaogopa lakini tunaweza tukaanza kwa kuwapeleka english course then waanze kufundisha kwa kiingereza. taratibu baada ya muda tutajikwamua tutajikuta ile kuvunja vunja inaisha as Practice makes perfect. Mwalimu akiwa anaongea na kufundisha kiingereza throughout with time naye atazoea na atakuwa mzuri tuu , tusiwe na shaka!
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Na mie wasiwasi wangu ndo huo, walimu je wana uwezo? Nimekua nawafunza(training) walimu wa taasisi moja ya serikali kwa miaka 3 sasa, baada ya mafunzo wanaandaa presentation na tunawatathmini. Kwa kweli watoto wetu huko shuleni wanadanganywa sana, na inasikitisha sana. Mwalimu anatohoa maneno anabadilisha maana nzima iliyokusudiwa, akiwa na ujasiri na tabasamu usoni. Ole wangu nimuulize unamaanisha nini, ndo ntachoka kabisaaa. Mkakati ungeanzia kwenye kujenga uwezo wa walimu kwanza. Hata kama walimu hawafundishi kwa kiingereza, ni vizuri uwezo wao japo wa kutafuta vitini vya ziada uwe juu.
   
Loading...