Ingiza mkwanja kwa kushirikisha marafiki kusoma hadithi

benny gilbert

Senior Member
Jul 4, 2018
110
65
Kama tittle linavyojieleza. Karne hii ni rahisi sana kuingiza pesa ukiwa na HOBBIES ya vitu fulani madharani unapenda kusoma vitabu vya hadithi au vya biashara. Hivyo ni kitu kinzuri kitachokufanya uwe unasoma vitabu vya hadithi au vya biashara uku ukingiza pesa mtandaoni.

Kuna hasara kubwa katika dunia hii kama kupoteza muda kusoma vitabu vya hadithi au vya biashara kwenye social media bila kutapa faidia yoyote zaidi ya burudani tu. Kwa sasa technology haitaki hivyo inataka watu wasome vitabu online na waingize pesa kwa muda wanaotumia kusoma hadithi. Epuka sana kupoteza muda mtandaoni bila kuingiza pesa, watu wengi wanajua facebook ni sehemu ya kuzurura kwa ku like na ku comment , no facebook ni sehemu ya kutafuta wateja na kuwapeleka sehemu ambao watapata huduma na bidhaa kwa matumizi yao binafsi sio sehemu ya kuzurura utakuwa unapoteza muda.

Kuna kitu tumeweka kwenye mfumo wetu kinaitwa "AFFILIATE MARKETING" kwa lugha ya kiswahili tunaita "UUZAJI WA USHIRIKA".

Kuna biashara zingine hazihitaji ata sh 10 , ni wewe na social media kwa kupost mara nyingi kuanzia saa 11 jion paka saa 3 usiku unafunga biashara. Kuna biashara inaitwa "Affiliate Marketing" au "Uuzaji wa Ushirika". Unaweza ukajiwekea kiasi unachitaka kuingiza kwa mwezi kwa kushare link kwenye social media.

Nini maana ya " BIASHARA YA USHIRIKA?",
ni njia nyepesi ya kupata pesa mtandaoni kwa kivuta watu kwenye website husika na kununu bidhaa au huduma na kupata kamisheni. Unaweza kuanzisha biashara kwa muda mchache kwa hasara ndogo tofauti na biashara zingine. Unachohitaji ni kujiweka kwenye njia ambao utakuwa katikati ya mteja na kampuni husika na kuvuna kamisheni kwa jutihada zako binafsi.
Uuzaji wa Ushirika ni biashara maarufu sana ya kuingiza pesa mtandaoni. Ni aina ya uwezo wa kimasoko ambao kampuni husika inakupa kamisheni kwa kila unayevuta kwenye mfumo wao na kulipia huduma kwa jitihada zako binafsi.

Kwa lugha nyepesi UUZAJI WA USHIRIKA ni promosheni ya bidhaa au huduma inayotolewa kwa njia ya mtandao kwa kampuni flani ambao balozi wao analipwa kamisheni.(Balozi ni wewe unaye share link social media). Uuzaji wa Ushirika ni njia ya kuvuna pesa kwa kutangaza na kuuza huduma kwa watu wengine na kupata kamisheni. Ni njia bora ya kuvuna pesa kama una watu wengi ambao unaweza kuwabadilisha kuwa pesa . Balozi anasaidia kampuni kutangaza huduma au bidhaa zao kwa kutumia link au kodi namna maalumu kama balozi.

Kwa mtu kubonyeza link na kujisajili na kununua huduma au bidhaa ambao kampuni husika inauza , balozi upokea kamisheni kwa kiasia alichonunua hiyo bidhaa au huduma kwa asimilia kadhaa ambao imeweka na kampuni hiyo. Balozi anaweza kuona kwenye mfumo kwa kila mtu aliyejiunga kwa link yake /kodi namba yake. Balozi analipwa kwa asilimia(%) kwa kila link au kodi namba yake kwa wote waliojisajili. Balozi ni nani ? Balozi ni mtu yoyote anaye uza bidhaa au huduma kwa kutangaza kwenye social media na mwisho wa siku anapata kamisheni(Salesman).

Wote wale unaowaona kwenye instagram mfano X, Y wote ni mabalozi wa kampuni flani ndio maana wanaweka matangazo yao ili wapate kamisheni, kwa bahati mbaya wale hawatumii link wao wanalipwa pesa taslimu kwa mwezi au kwa wiki. Hawapati pesa nzuri kama wangekuwa wanatumia kodi namba au link kunadi bidhaa au huduma kwa hayo kampuni(Hayo makampuni ni wajanja kwa kuwapa pesa taslimu na sio %).

Mfano X ana follower 5M, madhalan analipwa 150k kwa siku , kwa mwezi 4.5M. Kama angekuwa analipwa kwa % , chukulia 40% kwa kila mtu atakaye nunua bidhaa au huduma, chukulia tena anafanya matangazo ya duka la viatu na kiatu kimoja kinauzwa 30k. Chukulia kwenye follower 5M wamenunua hivyo viatu 1000, piga hesabu sasa 30000 x 1000 x 40% = 12,000,000 maybe kwa mwezi au kwa wiki.

Kwenye kampuni yoyote kubwa ukiwa ujui nguvu ya % , wanakupa pesa taslimu ujue unafanya kazi ya kanisa. Mfano mwingine ni Y, yeye alipewa na kampuni A pesa taslimu mamilion ya pesa, kampuni A wakamwambia wanataka episode 200 za kile anachokifanya kwa sasa kurusha kwenye TV. Ningekuwa mimi ningewaambia kampuni A wadhamin kipindi alafu mimi anilipe kwa % kwa kila kinachopatikana kwenye mauzo.

Nadhani kampuni A wangetakaa wangejua , jamaa mjanja wangesitisha mkataba na kutafuta mtu mwingine. Ndio maana unakuta wasanii wengi wanaingia mkataba na makampuni makubwa ila mwisho wa siku bado ni masikini wa kutupwa baharini. So sad so fun 😥.

Wacha tuendelea na somo...

Ni namna gani Uuzaji wa Ushirika unavyofanya kazi?
Chukulia mfano wa watu wa 3 kama wahusika.
1. Fadhili: Ana blog inadili na Hadithi au ana page au group linadili na hadithi.
2. Grace: Anapenda kusoma hadithi anatafuta sehem ambayo angesoma hadithi nyingi bila kikomo kwa bei nafuu kwa mwezi.
3. Erick: Ana website ambayo inatoa huduma ya watu kusoma hadithi kwa bei nafuu kwa siku 30. kwa lugha rahisi, Erick ana website inayo waunganisha kati ya Grace na Fadhili.

Faida na mahusiano ya hao watu 3 kuhusika:

1. Fadhili anajiunga kwa Erick kuwa balozi wa kutangaza huduma na kupokea kamisheni kwa kila anayejiunga kupitia link yake au namba yake.

2. Fadhili ataweka link yake kwenye blog yake kutangaza upatikanaji wa hadithi kwa bei rahisi kwa siku 30.
3. Grace ana tafuta google au (facebook group au page ) sehemu ambayo atapata hadithi kwa bei rahisi na mwisho wa siku akakutana na blog au group au page ya Fadhili.

4. Grace akaona tangazo la kusoma hadithi bila kikomo ndani ya siku 30 kwa sh 3000 tu. Akaamua kubonyeza ile link ya kwenye tangazo la hadithi aliloliona kwenye blog ya fadhili, na kumpeleka kwenye website ya Erick.

5. Grace akajiunga na kulipia kifurushi cha mwezi kwa sh 3000 kwa kusudi la kusoma hadithi zote zilizopo bila kikomo.

6. Kodi namna aliyotumia Grace kujiunga inaonekana kwa Fadhili kwa kamisheni aliyopata na itaonekana kwa Erick pia kujua watu wote walijiunga kupitia balozi fulani(Fadhili kwa sasa).

7. Mwisho wa siku kila mwezi mfumo utakusanya kamisheni zote kupitia kodi namba yake na kumlipa Fadhili pesa taslimu na kutumiwa kwenye Tigopesa yake.
Ni namna gani unaweza ongeza kipato kwa kutumia blog yako?
Blog nyingi zinapata mapato kwa kuwa mablozi wa kampuni zingine.

**********************************************************

UUZAJI WA USHIRIKA(AFFILIATE MARKETING)
Ni namna gani unaweza ongeza kipato kwa kutumia facebook, whatsapp na instagram bila kusahau Blog?

Blogger wengi wanapata kipato cha ziada kwa kuwa mabalozi wa "Biashara ya Ushirika" kwa kampuni nyingine.

Ni namna gani inafanya kazi pia
1. Blogger/Admin Group-Facebook anachagua kuwa balazi kwa kujisajili kampuni husika.

2. Blogger/Admin anaweza kuweka link yake kwenye blog yake au page au group lake kwa watu kuona ilo tangazo na kujiunga.

3. Blogger/Admin anaweza kunadi bidhaa au huduma ambayo inaendana na blog yake au page au group lake(Husiwe balozi wa kunadi huduma ya watu kusoma hadithi wakati wewe page yako inadili kuuza vyombo au furniture).

4. Kuwa balozi wa kitu ambacho unafanya kwa sasa mfano, una page au group au blog inadili na hadithi, jiunge na kuwa balozi wa kutangaza sehemu ambayo unaweza soma hadithi kwa mtililiko mzuri kwa bei ndogo.

5. Post hadithi fupi ambazo zipo kwenye website husika kwa nia ya kuwapeleka wakasome full hadithi kule kwenye mfumo.

6. Wabadilishe wasomaji wa page au group au blog kuwa wateja wa kusoma hadithi na kupata kamisheni kila mwezi.

Dondoo za blog/page /group kwa balozi wa uuzaji wa ushirika.
1. Tengeneza uhusiano na wasomaji wa hadithi kwa kupost hadithi nzuri na zenye kuleta hamasa kwa wasomaji , pia namna ya kupost vipande kwa ratiba.

2. Jikite kwenye kitu kimoja ukiwa kama balalozi wa uuzaji wa ushirika, kama unadili na hadithi weka hadithi na matangazo yanayodili hadithi kwa mfano promotion ya BLACK WEEKEND, kila msomaji hadithi ajue kuna promosheni kila IJUMAA kusoma hadithi bila kikomo ndani weekend (Ijumaa, Jumamosi na Jumapili) kwa sh 1000 tu. Ukichanganya mada kuna uwezekano wa kukosha kabisa likes na komenti kwa 50%.

3. Kujikita kwenye kitu kimoja ni bora zaidi kuwa mambo mengi.

4. Tafuta jukwaa bora ya watu kusoma hadithi na upatikanaji wa malipo kwa wasomaji. Usifanye kazi na jukwaa ambao malipo ni ngumu kufanyika utapoteza wasomaji na utakosa kamisheni ilo nalo ulikumbuke.

5. Jaribisha kwanza kabla ujaanza kunai huduma au bidhaa husika. Unawezaji kupiga domo jukwaa ni bora la kusoma hadithi kabla ya kulijaribu uone ili uwe na maneno mengi ya kunadi na kupata wateja wengi kujiunga na kupata kamisheni kubwa kila mwezi.

6. Jifunze kupitia wengi kwenye biashara ya uuzaji wa ushirika. Uuzaji wa ushirika ni fani na inahitaji kuwa mtaalamu wa kunadi na kufanya mauzo. Hii ni fani na sio unazaliwa nalo ila unajifunza kama ninavyowafundish mm leo.

Ni namna gani unaweza ukapata pesa kwa kutumia blog/page/group
*Kuwa kiongozi shupavu kwenye umati wa watu wengi*

Cha kwanza cha kufanya, hakikisha huduma au bidhaa unayo taka kuinadi ina vitu vifuatavyo:
1. Bei(Bei inaendana na uchumi wa sasa)

2. Faida(Kwa kuunga mtu unapata sh ngapi?)

3. Muonekano(Mfumo ni rahis watu kutumia?)

4. Upatikananji(Unapatikana muda wote?)

5. Huduma kwa wateja(Namba za simu zipo kwenye website?, wana akaunti fb, twittwer, telegram au instagram).

Jiulize
1. Kwann nataka kufanya nao biashara?
2. Nafanyaje biashara hii nakupata pesa?
3. Wapi nitafanya hii biashara?

Mtafute mwenye website na ongea nae ujue zaidi kuhusu yeye na namna ya kufanya hiyo biashara. Jilizishe kabla ya kuanza kazi kwa kumtafuta muhusika.
Tafuta wateja(Tengeneza Traffic).
1. Fungua facebook page

2. Invite your friends(Shirikisha marafiki)

3. Share page yako

Dondoo
1. Fikiri ni kitu gani wasomaji wanapenda? Picha au link

2. Shirikisha kitu ambacho weww unapenda na wasomaji watapenda tuu.

3. Ikitokea msomaji kauliza swali kwa fasta kumjibu.

4. Post mara nyingi uwezavyo, unavyopost mara nyingi ndivyo unavuozidi kuongeza idada ya wasomaji kukufuatilia na kuwageuza kuwa wateja wa hadithi baadae.

Karne hii ni kuwa na SMARTPHONE na kuwa balozi wa kampuni fulani na kuanza kunadi bidhaa za huduma zao na wewe kupewa kamisheni.

KAMA WEWE NI ADMINI KWENYE GROUP LA HADITHI, WASHAWISHI WAANDISHI WAWEKA KAZI ZAO KWENYE MFUMO WEWE WEKA LINK KWENYE GROUP LAKO NA PINNED. MEMBERS WAJIUNGE KWA KUPITIA LINK YAKO NA KUPATA SH 1200 KWA KILA MEMBER ANAYEJIUNGA NA KULIPIA HUDUMA.

UKIWA SERIOUS NA HII BIASHARA UTAONA UMUHIMU WA TECHNOLOGY NA KUWA NA SMARTPHONE, KWA SASA UWEZI KUONA UMHUMU WA SMARTPHONE PAKA UANZE KUINGIZA PESA.

ONLINE KUNA FURSA NYINGI SANA KAMA UNA MACHO YA KUONA FURSA, ILA KAMA UNA UTAENDELEA KUSHARE PAGE ZA MASTAA NA WEWE UPATI KITU.



"Chnage your thinking, Change your life".

#goodluck

1568454605663.png
 
Yale Yale ya Deci.

Ukiitwa kwenye fursa, Jua kua wewe ndio fursa.
Sidhani kama hiko hivyo, kwa jinsi nilivyoolewa mwenye huu uzi ana website ya uuzaji wa vitabu vya hadithi(sina uhakika).

Hivyo ana program ya affiliate kwa maana ukimualika mtu kutumia link na akanunua kitabu unapata kamisheni.

AMAZON e-commerce kubwa duniani wana affiliate program
https://affiliate-program.amazon.com/welcome/getstarted

Na ni moja ya njia ambayo bloggers hutumia ku-monetize blog au youtube channel badala ya adsense.
 
thesym,

Umenena vema sana, hivi vitu ni vigeni kwa watz walio wengi nitazidi kutoa elimu zaidi na kuwaelewesha watu wasipitwe na fursa kwa ufinyi wa elimu kuhusu "UUZAJI WA USHIRIKA".

AMAZON, APPLE, CLICKBANK, EBAY n.k zote zina kitwa kinaitwa "AFFILIATE PROGRAM".

Njoo PM nikupe link ya webiste .
 
Back
Top Bottom