Ingekuwaje kama Mhe. Pombe Magufuli angekuwa ndio Waziri Mkuu?

Inviolata

Member
Apr 23, 2009
70
2
Pamoja na mapungufu yake ya kawaida kama binadamu mwingine, mie nafikiri ni kiongozi ambaye angalau amejaribu kuonyesha umahiri wake katika utendaji. Tumeona Wizara alizokabidhiwa na mabadiliko aliyofanya kwenye wizara hizo, ni kiongozi ambaye nafikiri angeweza kuleta mabadiliko ambayo watanzania tunayahitaji. Watanzania sasa tumechoka na porojo za kisiasa. We need to see some actions taken' ni mtu ambaye naona angalau amejaribu kile ambacho watanzania wengi tunatamani kukiona. Nchi yetu nzuri imejaa maziwa na asali lakini kwa sababu ya wachache ambao wanajali matumbo yao wameifanya kuwa nchi ya watu maskini wakati kuna rasilimali nyingi tu ambazo zikisimamiwa vizuri tutaweza kuona matunda yake hapo baadaye.
 
Akipewa uwaziri mkuu atakua kama Pinda. Atakataza vazi la jeans,taxi mjini(wote wapande mabasi);atafunga private schools, atatoa viyoyozi maofisini,etc.
 
Pamoja utendaji mzuri wa kazi, huyu ni dikteta mkubwa sana. Unajua watu wafupi wana matatizo ya kufikiri watu wengine wanawadharau. Kule Bungeni utakuwa ndio mwisho wa vyama vya upinzani.
 
akipewa uwaziri mkuu huyu atawapa vimada wake wote nyumba za serikali amabazo hazijauzwa bado
 
May be that is what we need for the time being, 'a dictator' ambaye ataweza kuwa'handle' watu kama wakina Rostam na wenzake. Dont you think so?

Dictator anaweza kuleta maendeleo pale atakapo kuwa na displini,na si kujiona anajua kila kitu lakini pia awe na nia ya kweli ya kuwakomboa watu wake.Vinginevyo mtajikuta mmeingia choo cha kike.
 
Dictator anaweza kuleta maendeleo pale atakapo kuwa na displini,na si kujiona anajua kila kitu lakini pia awe na nia ya kweli ya kuwakomboa watu wake.Vinginevyo mtajikuta mmeingia choo cha kike.

Kama ndani kutakua na mwanamke huko ****** sio mbaya mnamaliziana haja zenu ~~~
 
ni mmojawapo wa mafisadi tu huyu yapo wapi ya Rose garden
 
Last edited:
Duh, ndugu yangu wap umekuwa mkali kweeli kweli. Mfupi kuliko nani? Au mrefu anatakiwa awe na urefu gani? Tafadhali nisaidie
 
kwa sasa tunahitaji kiongozi kama john pombe magufuli, ingawa naye ana mapungufu yake.
 
ni mmojawapo wa mafisadi tu huyu yapo wapi ya Rose garden

mkuu kwa issue ya rose garden labda wewe hujui hii kitu. Wakati magufuli kawekwa wizara ya ardhi alitaka kuishughulikia ile kitu lakini lile eneo ni la kikwete/lowasa kwa hiyo ndo maana alihamishwa hiyo wizara kwani alianza kuwagusa wakubwa wake. Na kama asingekuwa mjanja ingebidi ajiuzuru, lakini alipima madhara ya kuachia keki yenye siagi na aende kula kande.
 
Dictator anaweza kuleta maendeleo pale atakapo kuwa na displini,na si kujiona anajua kila kitu lakini pia awe na nia ya kweli ya kuwakomboa watu wake.Vinginevyo mtajikuta mmeingia choo cha kike.
Je tuambie kwa mfano discipline anayo hana
 
Bwana Pombe ni mchapakazi mzuri sana lakini anakosa sifa ya kuwa waziri mkuu kwa sababu ya jazba. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali anatakiwa mbali na uchapakazi vile vile lazima awe na busara.
 
Back
Top Bottom